Rwanda,Burundi na DRC hizo nchi unakuta mtu mmoja tu anasababisha tafrani nchi haikaliki, watu mamilioni wamemkimbia nchi zao, wameenda kuishi uhamishoni, au kwenye makambi ya wakimbizi. Lakini EU na USA kupitia UNHCR wana discuss namna ya kuwasaidia wakimbizi hadi mara zingine wanakosa pesa wanaomba msaada kutoka nchi zenye makambi kusaidia.
Kwanini huwa hawa shughuliki na mtu anaye sababisha kuwepo tafrani au anayezalisha wakimbizi?!
Mtu mmoja ana sababisha shida kwa mamilioni lakini anaachwa tu, sielewi demokrasdia wala diplomasia huwa zinafanyaje kazi ikifika hapo.
Solution ilitakiwa ifikiwe kwa kuondoa chanzo cha tatizo ili wananchi waendelee kufurahia kuishi nchini mwao. Enzi za Yugoslavia mliona Slobonan Milosevic aliondolewa akashitakiwa akafungwa akafariki Maisha safi. Huku kwetu wanasubiri mpaka tuuane, tukimbie nchi sasa ndio waanze kuongea demokrasia na diplomasia. Tatizo ni rangi zetu au matatizo yetu hayawahusu?!