Ndg zangu kadiri mnavyoikaribia dola ndivyo mashambulizi dhidi yenu yanavyoongezeka, acheni kulialia songeni mbele

ABC ZA 2025

JF-Expert Member
May 2, 2018
1,160
706
Wanajamvi amani iwe nanyi
________________________________
Tangu kuanzishwa kwa mfumo Wa Vyama Vingi (Multiparty system) chini ya Sheria ya Vyama vingi vya siasa ya mwaka 1992 takribani miaka 26 sasa na karibu miaka 28 ifikapo mwaka 2020, Hakika huu ni Umri sahihi na hakika kwa Upinzani kupewa na kuongoza dola la Tanzania kwa amani na utulivu.
______________
Nikatika wakati huu ambapo Vyama vya Upinzani vinaweza na vinastahili kupewa na kuongoza dola kwa hisani ya vyombo/makundi yote ya nchii hii tangu lile la wananchi Wa kada na itikadi mbalimbali mpaka hili la vyombo vya Ulinzi na Usalama wa nchi yetu kama Usalama Wa Taifa ,maJeshi, na wengineo kadiri itakavyowapendeza ili kuitafsiri na kuilinda demokrasia yetu kivitendo machoni pa-mataifa ili kufufua matumaini ya kiushirika kama ni kura wapinzani wamekuwa wakishinda mara zote tangu enzi za Mzee wetu Augustino Lyatonga Mrema mpaka hizi za Mzee Edward Ngoyai Lowassa.
_________________________________
Kuna wakati Wapinzani tunapashwa kukumbuka maneno ya Rais Wa 16 Wa Marekani hayati Abraham Lincoln (1861-1865) naomba kumnukuu "My concern is not whether God is on our side; my greatest concern is to be on God's side, for God is always right." Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema,"Shida sio Mungu yuko Upande wetu au laa tunapotenda ya haki bali hatupashwi kuwaza kama tuko na Mungu au laa kwani Mungu yeye hupenda haki siku zote na yupo sahihi, Kunawakati tunapofungwa jela,tunapoteswa na wenye mamlaka,tunapopotezwa kusikojulikana,tunapouwawa kikatili,Tunaposhuhudia wenzetu wakitusaliti kwa sababu ya kutafuta haki na usawa,maisha bora kwa watoto Wa watoto wetu lazima tuwe na hakika ya kuwa hayo ndiyo yanayompendeza Mungu nani Lazima Mungu atakuwa na sisi wakati wote, Na hizo ni gharama kidogo tu tunalipa tuacheni kulialia tufanyeni kazi.
__________________
Tunaposimama na kutetea wanyonge na wanyanyaswa Wa Taifa hili lazima tuwe na hakika kuwa tuyafanyayo ni ya Mungu na kwa Mungu tutashinda, kwayo,Kuna wakati mnaweza mkaona ni kama 2020 tena hatuwezi kupewa dola baada ya kushinda ila kwa hakika niwahakikishieni huu ndio haswa mwaka wetu wa kushika na kuongoza dola hili kwa weledi na Ufanisi Wa kiwango cha juu kabisa ili kuwaletea watanzania Maendeleo endelevu kwa kasi na tabasamu na wala si kupata tabu kama wanavyotuambia sasa, na niwakumbushe tu ndg zangu Siku zote kwenye kupata roho huwa nyeusi tuchapeni kazi Tu.
_________________________________
Upinzania-Tanzania watashinda nafasi zote kwa wastani Wa 71%+ kama mambo haya yatabaki yalivyo na kama yatabadilika Ushindi utapungua kwa 20% Tu
_________________________________
( I ) UKOSEFU WA AJIRA
Kwa mujibu Wa ripoti ya "Hali ya Uchumi" toka Wizara ya fedha inatanabaisha kuwa Zaidi ya Watanzania 800,000 wanaingia katika soko la ajira kila mwaka baada ya kuhitimu masomo yao huku wengi wao wakiwa ni vijana, Lakini uwezo Wa Serikali hii ya CCM-MPYA ni jumla ya ajira 40,000 kwa mwaka ambazo hata hivyo tangu mwaka 2016 hazijatolewa kwa kisingizio cha Uhakiki wa watumishi na baadae kisingizio kingine cha Ujenzi Wa miradi mikubwa ya Maendeleo kama SGR, SG na Ununuzi Wa Ndege na mingineyo ,
___________
Tangu Serikali hii ya CCM-MPYA iingie madarakani mwaka 2015 zimepita bajeti kuu tatu yaani 2016/17,2017/18 & 2018/19 ni sawa na kusema mpaka sasa kuna wasomi mil 2.4 yaani (laki 8×3=mil 2.4) wako mtaani bila ajira rasmi.Na kama mambo yatabakia hivihivi mpaka mwaka 2020 watoto wa masikini Wa kitanzania waliohitimu masomo yao katika kozi mbalimbali zaidi ya Mil 4 hawatakuwa na ajira rasmi na hii ni kwa mujibu Wa Ripoti ya hali ya uchumi ya mwaka 2016 iliyotolewa Bungeni Jun 2017.
______________
Sikia hii kwa mujibu Wa Utafiti Wa " Nguvu kazi na Ajira" Wa mwaka 2014 kulikuwa na Vijana mil 2.3 wenye umri kati ya miaka 15-35 wasiokuwa na ajira sawa na 10.3% ya nguvu kazi yote ya wakati ule ,Hawa ni vijana waliokosa kazi awamu ya nne ya CCM hiihii ambao nao bila shaka wapo mtaani mpaka sasa ,Ukifanya hesabu za Magazijuto yaani Wale 2.3 Waliokuwapo mwishoni mwa awanu ya nne na hawa watakao kuwapo hadi mwishoni mwa-awamu hii mpaka mwaka 2020 kama hali itabakia hivihivi tutakuwa na vijana wahitimu Wa kada mbalimbali zaidi Mil 6.3 wasiokuwa na ajira rasmi,
__________
Hebu kumbukeni haya mwaka 2014/15 makusanyo ya kodi kwa mwaka yalikuwa Tsh trl 7.42 tu lakini watoto wetu walipata ajira rasmi japo hao elfu 40 kwa mwaka,Si hivyo tu hata wakati Wa Mzee Ben yaani bajeti ya mwaka 2010/11 makusanyo ya kodi yalikuwa ni Tsh trl 5.74 tu lakini ajira halikuwa tatizo kama ilivyo sasa, chaajabu kabisa CCM-MPYA imeshindwa hata kuajiri hao tu elfu 40 huu ni mwaka Wa tatu pamoja na kujinasibu kuwa inakusanya tsh trl 15.5, Ama kwa hakika hii ndio turufu pekee ya Upinzani-Tanzania mwaka 2020 kama watazichanga vizuri karata zao.
_________________________________
( II ) AHADI ZA CCM MWAKA 2015

CCM-Tanzania wakubali wakatae mpaka sasa wametekeleza ahadi zao chini 30% kitu ambacho ni turufu nyingine kwa Upinzani-Tanzania,

Hebu tujikumbushe juu ya hizi ahadi 10 za CCM-MPYA kwa leo
__________
i/ Ununuzi Wa Meli 5 za Uvivi zitakazotoa ajira za moja kwa moja elfu 15,Ninachofahamu Wizara hii haina fungu la Maendeleo kwenye bajeti zake hasa 2017/18 haikupata hata senti,Hii ni turufu kwa Upinzani 2020.
__________
(ii) Ujenzi Wa Bandari ya Uvuvi itakayotoa ajira za moja kwa moja elfu 30, Ni mwaka Wa tatu sasa hiyo bandari haipo na habari ya Mjini ni nyavu haramu"
__________
(iii) Tuliahidiwa mialo 9 kwenye maziwa ya Tanganyika ,Nyasa & Victoria watu wakatoa kura hadi Leo hawaamini macho yao.
__________
(iv) Tuliahidiwa viwanda Viwili vya Ngozi pale kanda ya kati bila hiana tukatoa kura zetu.Mikoa ya kanda ya kati mnaahidiwa kiwanda cha ngozi wakati mnafahamu fika kuwa 80% ya ngo'mbe wrote mnaowafuga wanaliwa Dar es salaam, Sasa hicho kiwanda/Viwanda ni kwaajili ya ngozi ya punda Wa wanchina au ndio mmezoea kudanganywa na CCM, Huu uongo pia ni turufu kwenu Wapinzani acheni kulialia pigeni kazi.
__________
(V) Tuliahidiwa meli kubwa nne za abiria na mizigo katika maziwa ya Tanganyika, Nyasa & Victoria tukatoa kura kama zimefika nitumieni picha.Kwa Msiofahamu bei ya Meli ya Mizigo na abiria ya kawaida ni €2.8mil sawa na Tsh bill 7.42 zikiwa 5 tunahitaji kuwa na bill 37.1, Kwa Serikali inayokusanya bill 1,400 kwa mwezi sidhani kama wameshindwa kutekeleza hili ndio sababu nasema CCM inawadharau sana waliga kura Wa nchi hii, Wapinzani tumieni fursa hii ya chama tawala kuwadharau wapiga kura wake ninyi iwe turufu kwenu 2020.
__________
(Vi) Mliahidiwa kujengewa bandari mpya za Bagamoyo na Mwambani Tanga mkatoa kura kwa raha zenu.Watani zangu Wa Tanga na Bagamoyo hii imekula kwenu naamini 2020 mnayo sababu ya kuinyima kura CCM.
__________
(Vii) Walimu-Tanzania mliahidiwa 80% mtaanza kufundisha kwa kutumia TEHAMA, Yaani Vilaptop kura mkatoa kwa roho safi ila poleni sana, Kwa mujibu Wa TAMISEMI kati ya mwaka 2016/17 katika shule za Serikali za Sekondari &Msingi tulikuwa na Jumla ya walimu 268,658 kama tungewanunulia Vifundishio/TEHAMA 80% ya walimu hawa kama ilivyoandikwa kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2015 ingeligharimu Taifa hili Tsh bil 322.4 kwa walimu hao 214,927 ambao ni sawa na 80% ya walimu wote nchi kwa wakati ule ,Lakini Ninyi walimu wakati mnaahidiwa haya yote mwaka 2015 na mkakubali kutoa kura na mnajua zaidi ya nusu ya shule zenu hazina Umeme mmewahi kujiuliza hili? ,Je hii ni ahadi halisi au Utapeli kwenu walimu wetu? Walimu acheni uteja Wa CCM wanafunzi wenu wanawacheka sana, Wapinzani hii pia ni turufu nyingine muhimu kwenu acheni kulialia chapeni kazi yajayo yanafurahisha sana.
__________
(Viii) Tuliahidiwa kila kijiji/mtaa tutapata mil 50 (revolving fund) kura tukawamwagia kwa wingi tulichoambulia mpaka sasa Mungu anajua hii ndio CCM yenye turufu kwa Upinzani 2020. Ni mambo ya ajabu CCM wanawalaghai wapiga kura zaidi ya 63% waishio Vijijini kwamba watapewa mitaji, Tanzania inakadiriwa kuwa na vijiji 19,000 kama wapewa mil 50 itaigharimu serikali hii ya CCM tsh bill 950 kitu ambacho siamini kama wameshindwa kutoa hizo fedha au hawana dhamira njema na watu waishio Vijijini au nidharau tu kwa wapiga kura Wa Vijijini? Upinzani mnazo fursa 1001 za kushinda uchaguzi 2020.
__________
(IX) Tuliahidiwa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa kila mwaka kama wakati wa JK, Mfano wakati anaondoka alitupa bill 299.3 2014/15 cha ajabu leo bajeti nzima ya Maendeleo ya kilimo 2017/18 ni bill 27.231 yaani 9.1% ya fedha za ruzu tu wakati Wa JK. Wakati 100% ya chakula,65% malighafi zote za viwandani,30.1% ya GDP la Taifa,75% ya ajira zote nchini vyote hivi vinategemea Kilimo ambacho kinapewa 18% kama bajeti ya Maendeleo kwa mwaka mzima, Upinzani tunayo turufu ya kushinda uchaguzi 2020 twendeni mbele japo naamini tutafika wachache.
__________
(X) Kuna watu waliahidiwa nyongeza ya Mishahara na marupurupu lukuki na wakatoa kura ila mpaka sasa hata lile tu ongezeko la lazima la mwaka(Statutory annual increment) ambalo tangu Uhuru Wafanyakazi wamekuwa wakipatiwa nalo ni gaaa,Ukisoma Mfumo Wa Bajeti kwa mwaka 2016/17-2020/21 Bajeti ya Mishahara na marupurupu mwaka 2020/2021 inakadiriwa kuwa tsh trl 10.11 toka trl 7.63 ya mwaka 2018/19 ikiwa ni ongezeko la tsh trl 2.5 sawa na 33% ambayo nayo ukiigawanya kwa miaka 5 ni sawa na ongezeko la 7.7% kwa mwaka ambayo ni juu kidogo ya annual increment stands ya (1-5)% Kwa lugha rahisi CCM imeamua kuwakusanyia wafanyakazi wake ongezeko lao la kila mwaka la lazima kwa miaka mitano ili kuwapa kwa mkupuo mwaka 2019/2020 lengo likiwa ni kuwahadaa, CCM inacheza na akili zetu sawasawa hii ni turufu kwetu 2020 jipangeni sawasawa huu ni mtaji wenu,
__________
Tukutane Buyungu kwa Elia,
Emmanuel Allute
Kada Wa Chadema
__
Alluteemmanuel@gmail.com
 
Duh, umenifanya nizaliwe upya!!
 
Back
Top Bottom