Ndg. Patrobas Katambi anahitaji tiba ya haraka sana (Seriously)

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,872
2,000
Amani iwe kwenu wakuu!

Kama mada inavyojieleza hapo juu kama kuna mtu anawafahamu wazazi, kaka au dada wa huyu aliyekuwa DC wa Dodoma mjini bwana katambi basi naombeni huyu ndugu yao awahishwe hospitalini maana kama ni malaria basi imeingia kichwani na muda si mrefu anaweza kupelekwa mirembe. Nimeona video clip fulani nikamuonea huruma sana. Kati ya aliyoyasema ni haya.

1. TL ni mwanaharakati anayeleta mabadiliko hasi
2. Lissu alipopigwa risasi ni yeye ndiye aliyemtaarifu Mbowe kuwa TL kapigwa risasi akiwa DSM na mbowe akiwa huko dodoma alichukua muda kumjibu
3. Yeye ndiye aliyetoa wazo la TL kutibiwa Kenya maana alijua gharama za hospitali za Kenya akiwa Sahara Media
4. Mbowe aligombana na familia ya TL aking'anga'a hela zilizokuwa zinatolewa na serikali kwa matibabu ya TL
5. Mbowe ndiye aliyekataa serikali isimtibu TL
6. TL hakupelekwa Ubelgiji na CDM bali familia fulani ambayo hajaitaja.
7. Yeye katambi akiwa na Mbowe na Mashinji walienda bunge la ulaya (ubelgiji) na baadaye wakaongea na Angela Markel kama wanabisha waseme (japo hicho walichokisema huko hajakisema sasa sijui CDM wapinge nini)
8. TL ana uraia wa nchi mbili (ametafuta political asylum huko ubelgiji)
9. TL ametumwa kuvuruga amani ya nchi kwanini alikuwa anaomba ulinzi katika nchi ya amani kama Tz
10. Watu wanajaa kila alipo si kwamba wanampenda bali wanamshangaa kama wanavyoshangaa helicopter
11. Operation UKUTA ilikuwa ni Idea yake
12. TL anadanganya kuwa JPM alitoa hongo Ikwiriri wakati alikuwa hajachukua fomu ya NEC (TL ni muongo mjanja mjanja wa sheria)
13. Baada ya kununua ndege hakuna ndege ya mabeberu inayokuja hapa Tanzania , ndege zote ni ATC (Precision ya mabeberu imeondoka)
14. Mashirikia ya umma yote yanapata faida na kutoa gawiwo
15. Ukimuondoa JPM umerudisha ukoloni mambo leo nchini
16. CDM hata wakipata urais wataenda wapi wakati hawana hata ofisi (sijui Ikulu ni mali ya chama au ya watanzania)
17. Salum Mwalimu kwanza si mzanzibari aligombea Kinondoni akiwa anaishi tu kwenye nyumbani ya kupanga tena aliyopangiwa na mwanamke fulani.

Haya ni machache aliyoyazungumza katambi kwenye video clip hiyo, shida yangu si hayo maneno ambayo huenda yana ukweli au hayana maana kila mtu ana mtazamo wake. Shida yangu ni jinsi alivyokuwa anapresent hoja zake. Yaani hana utulivu, hapangi hoja, haamini anachokisema, anatumia nguvu nyingi kuliko hoja, anataka kujimilikisha yote mazuri yalifanywa na CDM. Kwakweli huyu ndugu kama hatafuti huruma ya jina lake kurudi kwenye ubunge basi awahishwe hospitalini.

Kindikwili
 

Miss Madeko

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
4,122
2,000
Toka aambiwe aoe kumbe hawezi kuwa na mwanamke maana yeye ni Toashi ndio hivyo amebaki kubwabwaga tuu. Nape si amesema ukiongea bila kujibiwa jiulize kumbe sio kujibiwa tuu hawajui nini waseme. Nawaambia this time hata wake zao wataongea
 

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,872
2,000
CCM wanataka taifa la wajinga ili watawale vizuri! wako tayari kujenga shule na kuongeza madarasa na kuchonga madawati halafu hutaki kuajiri waalimu! Hutaki waongezewe mshahara. Hizi kizazi cha kuanzia 2000 zitawatoa madarakani
Huyu njaa kali ndiyo maana anajitoa ufahamu
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,118
2,000
Mti wenye matunda ndio wenye kupigwa mawe. Tutashuhudia majuha wengi kweli mwaka huu. Ila mpambano kati Sauli na wapambe wake dhidi ya Daudi na watu wake bado inaendelea.

Kichwa cha Goliathi kilichukuliwa siku ile ya tukio la jaribu la mauaji kushindikana. Naam! Siku ile ya uvuli wa mauti. Ukishindana na mpakwa mafuta wa BWANA, ni sawa na kutaka kujiangamiza mwenyewe.
 

Craig

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
1,071
2,000
Hebu iweke hapa tafadhali
Mkuu kuiweka hapa Ni kuendelea kumpa Kiki huyo Jamaa, Binafsi niligundua kuna kitu hakipo sawa Hasa Muonekano wake Bandia,

Pia Uelewe anavyosema kuwa anamjua sana TL nikana kwamba anashoboka kwake, Ila niwazi huyoJamaa anatia huruma kwa maneno yake.
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
13,933
2,000
Point No.17 nimeipenda,
Ni Salum Mwalimu aligombea Kinondoni, lakini mgombea wa CCM Zanzibar alikuwa mbunge wa Mkuranga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom