NDG Bernad Camilius Membe - Huu ndiyo wakati muafaka kwako kuomba radhi

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,205
4,695
Naandika uzi huu kwa nia nzuri kabisa ya kuwasilisha ushauri kwa Ndg Bernard Membe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi

Sote tunafahamu maneno ya dharau na kebehi yaliyotoka kinywani mwa Ndg Membe kabla na hata baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020

Kiuhalisia kebehi zake dhidi ya Serikali & Chama cha Mapinduzi ziliongozwa na hisia chafu zilizotokana na uroho wa madaraka pamoja na ubinafsi mkubwa uliotawala nafsi yake

Ndg Membe alipewa sifa nyingi ikiwamo kuitwa Jasusi Mbobezi na yeye kujaa kiburi kwa kujiona yupo juu zaidi ya Chama na Serikali yake

Ndg Membe almaarufu Jasusi Mbobezi alisahau malezi na makuzi mazuri alipewa na Serikali ya CCM na ndiyo kiini cha ndiyo mafanikio aliyonayo!

Hekima ya hali ya juu ilitumika kumruhusu bila bughuda wake kujiunga na Upinzani pamoja na kugombea Urais ili kuthibitisha ujabari wake!

Matokeo ya Uchaguzi huo yalimpa somo kubwa sana kuwa hakuwa na umaarufu au uwezo alioamini kuwanao hapo awali!

Nitumie fursa hii kumuomba Ndg Bernard Membe kumuomba radhi Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhesh Dkt John Pombe Magufulu, kuwaomba radhi Wana CCM wote na Watanzania kwa ujumla

Ndg Bernard Membe bado hujachelewa, jishushe, usione aibu na omba radhi urejeshe heshima yako.

Wasalaam!
 
Membe lacks [or rather lacked] self-awareness.

Under the current state of affairs, no opposition candidate can win the top job.

You would think Membe should have known that, especially since he is considered by some to be a seasoned security apparatchik.
 
Membe moja ya watanzania ambao hakupitia maisha magumu kabisa yani anamaliza kidato cha sita akiwa tayari ni muajiriwa wa idara nyeti........He is jasusi mbobezi na muaminifu saana kwa Rais

kiufupi wewe ni mweupe hujui siasa za Tanzania
 
Mmemshinda Membe kwenye urais, lakini hilo mnaona halitoshi bado?

Aombe radhi kwa kitu gani specifically?

Kugombea urais?

Kuusema vibaya utawala wa Magufuli?
 
Middle class wa kitanzania hovyo kabisa!Ndg.Membe aombe radhi kwa kosa gani alilolifanya?ccm ni chama dola ,bila dola sio chama cha kisiasa
 
"Bora ufe ukiwa umesimama! Kuliko uishi ukiwa umepiga magoti" Huu msemo utadumu milele! Mh. Bernard Membe , natambua upo humu jukwaani.

Kamwe usiwasikilize hawa misukule wasio jitambua. Siku zote simamia kile unacho kiamini! Wewe ni mtu unaye jiamini. Na bila shaka ulikuwa ni chaguo la JK kabla ya kukutoa sadaka na kutuletea huyu mungu mtu.
 
Back
Top Bottom