Ndesamburo kusafirisha wananchi bure kwenda Loliondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndesamburo kusafirisha wananchi bure kwenda Loliondo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Mar 14, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  MAMIA ya wakazi wa mji wa Moshi wamejitokeza kwenye ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo, Philemon Ndesamburo (CHADEMA) kujiorodhesha majina kwa ajili ya safari ya kuelekea kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, katika Kijiji cha Samunge, Loliondo anayetoa dawa ya kutibu magonjwa sugu.

  Wananchi hao wamejitokeza baada ya mbunge huyo kuamua kutoa usafiri wa bure wa kuwapeleka na kuwarudisha wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa sugu ambayo tiba yake hutolewa na ‘Babu' baada ya kuona wananchi wengi wanahitaji kwenda ila wanakwamishwa na fedha za nauli ambazo zimefikia kiasi cha shilingi 150,000.

  Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana huku nje kukiwa na misururu mirefu ya wananchi wanaojiorodhesha, Ndesamburo alisema kuwa watawapeleka wananchi hao kwa awamu ambapo kwa kuanzia leo (Jumanne) jumla ya watu 73 wataondoka majira ya saa kumi jioni kuelekea Loliondo na wakirudi wataondoka wengine.
   
 2. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ndesa ataendelea kuwa mfano wa wazalendo
   
 3. H

  HYDROCHLORIC Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu akuzidishie Mheshimiwa Ndesamburo.
   
 4. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  anajua kula na kipofu
   
 5. Mbeu

  Mbeu Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  real people like Ndesa will always live in our heart even though his life is over, live long Ndesamburo. The so call tycoons need to copy from this Mzee he is a true MZALENDO. May God Almight grant you more days on planet earth, aika mmeku!
   
Loading...