Ndesamburo azindua mfuko maalum kusaidia wana-CHADEMA wanaobambikiwa kesi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndesamburo azindua mfuko maalum kusaidia wana-CHADEMA wanaobambikiwa kesi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, May 9, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mjumbe wa Kamati kuu CDM na mbunge wa Moshi mjini Philemon Ndesamburo amezindua mfuko maalum wa kuwasaidia wanachama na viongozi wa chama hicho wanaobambikiwa na kufunguliwa kesi kila mahali ili kuwakatisha tamaa.
  Ndesamburo ametaja kesi kadhaa zinazowaandama wanachama wake kama za maandamano ya Arusha na kesi polisi wanayoiandaa kumbambikia Mbunge Nassari.
  Ndesamburo alitoa tamko hilo wakati akizindua tawi jipya la CDM mjini Moshi na kukabidhi kadi zaidi ya 50 kwa wanachama waliohama CCM na kujiunga CDM katika operesheni maalum ya Vua Gamba Vaa Gwanda.

  SOURCE:ITV HABARI
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Chadema kuna mifuko mingi kuna mfuko alizindua Mbowe pale Arusha, kuna mfuko wa Bavicha wa Heche, leo tena kuna mfuko mpya wa Ndensaburo, sijui huu unaitwaje..huu sijaona namba za M-Pesa au TiGO PESA.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WARAKA WA MWIGAMBA KWA WALALAHOI WA NCHI HII:
  UJUMBE KUU NI KUSEMA KILA MMOJA WETU LEO HII VUA GAMBA HADI MOYONI, VAA GWANDA HADI MIGUUNI ILI TAIFA LETU LIPATE KUKOMBOLEWA BILA KUCHELEWA


  Ewe Ndugu yetu Mhe Kamanda Mwigamba, nakusalimu katika jina la Mungu aliye hai, Mungu mmoja kwa Waislamu, Wahindu, Wakristo na hata wale wasiokua na dini.

  Mheshimiwa mlalahoi mwenzetu, hakika NIMEGUSWA SANA TENA SANA na waraka huu ulioniandikia mimi kama sehemu ya UMMA WA TANZANIA na kunikumbusha wajibu wangu kama raia ni nini pindi ninapoona taifa langu linatafunwa bila huruma na ndugu zetu wachache waliojichagulia kugeuka mafisi kati kati yetu.

  Ndio, kwa wale wanaodhani kuwa ni kitu sifa hapa watashangaa na roho zao wenyewe: Naseme mtu USIOMBE KUONA MWENZAKO ANAPOCHAGUA KUKISIMAMIA KIDETE NA KUENDELEA KUTETEA kwanguvu zote KILE ANACHOKIAMINI.

  Jamani kitu 'KUTETEA KILE UNACHOKIAMINI' ni zaidi ya kilevi chochote kilichowahi kugundulika duniani kwa kuwa chenyewe tu kinakuimarisha mwilini wakati pombe inakudhoofisha, kinakulisha shibe ya kuona ushindi u karibu wakati bangi inakufanya uwe mharibifu, nasema kwamba pindi ntu unapotekeleza sehemu ya kile unachokiamini ndipo unapojihisi kwamba KAMA MUNGU MUUMBA WANGU HAPENDEZWI NA UFISADI, DHULUMA, MAUAJI sasa mimi nilie kiumbe chake tu nimekua nani kuhiari kuunga mikono machafu yote haya ya CCM?

  Ni kweli kwamba hadi dakika hii mara baada ya kusoma waraka huu hakika ninaendelea kusikiliza hadi mapigo ya mioyo ya walalahoi wenzetu wengine huko madongo kuinama na jinsi gani wanavyoomba kama sisi hapa kwamba WATESI WETU HATA MMOJA ASIFE LEO WALA KESHO ili nao waje wakauonje utamu wa maisha huru bila dhuluma, ufisadi wala udhalilishaji wa HAKI NA UTU WA KILA MTANZANIA.

  CHONDE USILIE KWA HAYA YOTE TUNAYOFANYIWA NDANI YA NCHI HII NA HAWA NDUGU ZETU WALIOGEUKA MAFISADI NA MANYANG'AU HUKO CCM, mwenzetu unapolia wengine ndio kwaaaanza unatupandisha mori ya MABADILIKO KWA NGUVU YA UMMA na kubakia tu kutama turuke vichwa vyetu viguse dari la huko mbinguni ili tunaporudi kukanyaga ardhini na watesi wetu wooooote wawe wamezama kwa nguvu moja hiyo hiyo tutakaotua na hapa chi.

  Naam, Ndugu yetu mwigamba kwa kweli moyo inakwenda mbio sana lakini imani yangu inaimarika ajabu huku nikiendelea kuhimiza kila mmoja wetu ndani ya nchi hii atambue wazi kwamba sisi Umma wa Tanzania wengi wetu tulio masikini wa kutupwa UWEZO TUNAO kwa namna ya ajabu mno ambapo hata mdhalimu angekuja na nini mbele yetu KAMWE HAWEZI HATA DAKIKA MOJA kuzuia azma yetu kama taifa kuamua kukaa upande sahihi wa historia kwa kujichagulia MWANGA NA KUONDOKANA NA GIZA kimoja.

  Hakika hadi hivi sasa WaTanzania TUMESHAAMUA KWA YETU SAFARI YA KUJIKOMBOA NI MBELE DAIMA BILA FUJO NA KWAMBA KATU NYUMA hakuridiki tena. Bai bai Mafisadi, bai bai CCM huku tukitumia fursa hii hii hapa kukaribisha HAKI, HESHIMA, na UTUNZAJI WA UTU NA HADHI YA MTANZANIA kwa ajili ya kujiletea maendeleo zaidi, kujijengea zaidi upendo wa kweli, amani na utulivu usiolazimishwa katika shingo yetu.

  Hivyo kwa kila mlalahoi wa nchi hii bila kujali chama chako, dini yako, kabila wala kanda, hebu kaseme maneno haya mara tatu kisha ukayaweke katika dau kwa Mwenyezi Mungu ili yakapate kibali na baraka zake:

  KASEME MANENO HAYA KISHA UKAYAOMBEE DUA YA KHERI:

  a. JUKUMU LA KULIKOMBOA TAIFA LETU NI JUU YETU BILA KUBEMBELEZWA NA MTU,
  b. UTETEZI WA HAKI NA UTU WA KILA MTANZANIA NI MILIKI YETU NA
  c. AZMA YA KUUNG'O MFUMO FISADI KWA NJIA ZA KIDEMOKRASIA NI WAJIBU WETU,


  na ukamalizie kwa kuliambia moyo wako mwenyewe kwamba UKOMBOZI WA TAIFA kuondokana na mfumo FISADI tangu sasa ni LAZIMA UANZE NA MIMI HAPA NA KUKAMILISHWA NA MIMI MWENYEWE kwa kucheza sehemu yangu ipasavyo!!!

  EWE MUNGU WA MBINGUNI TUSAIDIE KWANI KATIKA WEWE WATANZANIA TUNAYAWEZA YOTE KWA KUWA UWEZO TUNAO KATIKA WEWE USIEPENDEZWA NA KITU DHULUMA.

  Utaifa mbeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeele kama tai lakini katika haki kwa wote ndani ya taifa hili bila kubaguliwa kitu!!!!!

   
 4. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mungu akusamehe
   
 5. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mradi huo,

  wenye akili wameshatambua.
   
 6. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Soma signature yangu.

  Hii NGO ndugu yangu, waulize pesa zilizochangwa arusha kwenye kampeni ya nasari zimeishia wapi?

  Ndio ujasiriamali huo.
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wewe sio mchangiaji wa CDM lakini ndio unakuwa wa kwanza kulalamika, maajabu!! Hata Mwl Nyerere alipokuwa anachangiwa kwenda UN kudai uhuru wa Tanganyika watu kama wewe wenye kupenda kukatisha tamaa walibeza na kuwashangaa waliokuwa wanachanga but uhuru ulipopatikana wote walishangilia. Hata wewe Ritz1 utafaidika tu na maendeleo yatakayoletwa na CDM ikiingia madarakani, kama sio maji safi basi barabara au zahanati...
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Vua Gamba, Vaa Gwanda!
   
 9. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mna hasira, watu wameshashtuka miradi imekuwa mingi na hakuna marejesho.

  Ukiuliza wanakuita msaliti, unavuruga chama.
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu unalalamika hujatoa shilingi hata moja mbona Ndesamburo halalamiki wakati alitoa milioni 20 kwenye M4C?
   
 11. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu CDM inajitahidi kupanu "Fund Base" yake kadiri iwezekanavyo, tofauti na chama cha mshua, ambapo mkitaka ela mnaenda kuchota serikalini, au kubadilisha vifungu vya matumizi... mmeona haitoshi, sasa havi vikao vya chama mmeamua kuvifanyia ikulu kwa gharama ya kodi za wananchi...
   
 12. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nasikia una gwanda la moyoni
   
 13. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,889
  Trophy Points: 280
  ungeona hizo namba ungechangia????
   
 14. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi nilikuwepo kwenye huo mkutano wa ndesamburo na nilitupia hapa jf, aliahidi kugharamia barabara ya mdawi na kuwa huo mfuko ataugharamia pia na watu wenye nia nzuri na nchi hii atawakaribisha kuchanga.kwa maelezo zaidi tafuta sredi inayosema KATA NZIMA YAHAMIA CHADEMA.
   
 15. n

  ngaranumbe Senior Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unauliza zilizochangwa zilienda wapi, hivi unaakili kweli! kwani ulitoa ngapi kama unashaka urudishiwe. Chama kimetulia na wanachama wanahabarishwa juu ya matumizi yake, mwone EPA, RICHMOND,GAMBA MKUBWA WE!
   
 16. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CAG tuma vijana wakakague mifuko ya CDM kuna harufu ya ufisadi
   
 17. Marcopolo

  Marcopolo Member

  #17
  May 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  gamba kazini
   
 18. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Edmund


  Ndesapesa asiwadanganye. Hakuna barabara iliyojengwa na CDM hizo zilizopo pamoja na uchochoro wa Mdawi ni pesa za Halmashauri isipokuwa ya Shia nasikia ilipata ufadhili wa Tasaf. Huyo Diwani wa CDM wa Kimochi ananuka Rushwa.
   
 19. h

  hans79 JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  online ndo namba za kuchangia,acha umbeya wakati chadema wanapotumia helkopta ulidai wanafadhiliwa na nchi za nje ili kuleta machafuko. Leo wanapita kwa wananchi kuomba michango unalala,lipi jema kwako? Acha wivu jifueni kwanza magamba.
   
 20. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Kwani CCM wanamiradi mingapi na wanaiba vingapi kukiimarisha chama????
   
Loading...