Ndesamburo ashitakiwa kwa Rais Kikwete, Ban Kin Moon | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndesamburo ashitakiwa kwa Rais Kikwete, Ban Kin Moon

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATANO, JULAI 25, 2012 04:45 GABRIEL MUSHI NA MARIAM AYUBU

  ALIYEKUWA mgombea ubunge Jimbo la Moshi Mjini kupitia chama cha NCCR Mageuzi, Faustine Sungura, amezidi kumkaba koo Mbunge wa jimbo hilo, Philemon Ndesamburo (CHADEMA) baada ya kumshitaki kwa Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Kin-Moon.

  Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Moshi kutupilia mbali madai ya kesi yake aliyoifungua Desemba, 2010, kupinga uteuzi wa waliokuwa wagombea wenzake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Sungura ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi za chama hicho, alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu aliyekuwa jaji wa kesi yake amemuonea.

  Alisema aliyekuwa jaji wa kesi hiyo, Jaji Moses Mzuna, aliiendesha kesi yake kwa upendeleo, kinyongo lakini pia kinyume cha sheria.

  “Baada ya tume ya uchaguzi kuwateua wagombea wenzangu katika Jimbo la Moshi Mjini mimi sikuridhika nao, nikaweka pingamizi zangu ambazo zilitupiliwa mbali na Tume hiyo na kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi nilifungua shauri N0 1/2010 la kesi ya uchaguzi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Philemon Ndesamburo.

  “Aidha kutokana na ukiukwaji wa sheria katika kesi hii, Julai 12, 2010, nilifungua maombi namba 39/2010 juu ya kiasi cha dhamana ya kulipa mahakama au kusamehewa kulipa dhamana yoyote, kwa kuwa ukifungua kesi unatakiwa kulipa dhamana ya shilingi milioni nane au kuandika mali zenye thamani ya vitu visivyopungua milioni tano.

  “Mara baada ya mahakama kuridhika kuwa sina fedha, Jaji Mzuna alitoa uamuzi akinieleza kuchangisha fedha ndani ya siku 14 kutoka kwa marafiki zangu, ingawa uamuzi huo ulikuwa ni kinyume cha sheria.

  “Kwa kuwa sikuridhishwa na uamuzi huo, niliwasilisha tena maombi yangu na kupewa namba 11/2012 lakini pasipo halali na wala sheria, Jaji alitolea uamuzi maombi hayo bila kusikiliza na kuyafukuza makamani, hii ni kinyume cha ibara ya 13 (6) (a) ya Katiba ya nchi.

  “Kutokana na hali hiyo Januari 6, mwaka huu wadaiwa wangu walipokea hati ya wito kuwasilisha nyaraka mahakamani na walitakiwa kusajili nyaraka zao kabla ya Januari 28, mwaka huu lakini badala yake walisajili Mei 9, mwaka huu ambapo pia mimi nilipewa nakala ya hati hiyo na kuipitia.

  “Hata hivyo baada ya kugundua ina makosa nililipia ada ya ukaguzi na kukagua jalada la Ndesamburo na kukuta hati ya kiapo kinzani, pia ina makosa na kuifungulia pingamizi la hati yake, lakini baada ya mahakama kugundua hilo ilimuita na kumtaka akale kiapo kwa wakili kukamilisha hati yake na kuirudisha siku hiyo hiyo ya Mei 9, mwaka huu.

  “Lakini aliirudisha Mei 10 na mahakama kusikiliza pingamizi hilo na kunituhumu kuwa nimeghushi nyaraka hizo kwa sababu zilizopo mahakamani zinadai Ndesamburo alirudisha hati ya kinzani Mei 9, lakini niliyokuwa nayo mimi inasema alirudisaha Mei 10, mwaka huu,” alisema.

  Alisema kutokana hali hiyo, ameamua kulishughulikia suala hilo kwa mbinu za kiutawala zaidi kwa kumuandikia barua Rais Kikwete na Katibu Mkuu wa UN, TAKUKURU, kwa IGP Mwema, LHRC, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa kwa ajili ya kuchunguza zaidi sakata hilo na kujionea namna alivyoonewa.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Siasa za Tanzania; zageuka kuwa za Kimataifa... Mfa Maji haachi kutapatapa?? Rais na Ban Kin Moon watamsaidiaje?

  Labda atachaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu UN - Kuiwakilisha Moshi Mjini.
   
 3. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  sasa bank moon amegeuka wizara ya mambo ya ndani? Duh
   
 4. r

  rwazi JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amesahau kumuandikia na Rais Obama,angemsaidia sana
   
 5. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Faustine Sungura mimi nilidhani ana akili kama za "Sungura" kumbe ni bure kabisa, masikini anamudhalilisha Sungura, mnyama mjanja sana.

  Aliyepindisha SHERIA kwa mtazamo wake ni JAJI MZUNA, ambaye anateuliwa na RAIS kuwa JAJI. Refer Hotuba ya Lissu JK siku hizi anateua MAJAJI bila kufanyiwa VETTING na tume ya mahakama, hivyo majaji VIHIYO JK amewateua.

  Sasa badala ya kumshitaki JK kwa Ban Ki-Moon kwa kuteua Majaji vihiyo bila kufuata sheria za nchi, yeye anamshitaki Ndesamburo,a s if ndiye aliye hukumu hiyo kesi.

  Kuonesha kwamba SUNGURA si SUNGURA eti unamuandikia Kikwete (mteuzi wa Mzuna) kumlalamikia kuhusu pingamizi la kesi yake. It reminds me kesi ya Tumbili kupeleka kwa Ngedere.

  Mbona JK hapa atakuambia kwamba MAHAKAMA ni MUHIMILI mwingine hivyo hawezi kuuingilia. Sungura ndugu yangu una jina nzuri lakini matendo yako hayaendi ki-Sungura Sungura!
   
 6. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hivi haoni 2015 ni kesho kutwa tu asubiri agombee tena yaani toka 2010 linngangana mahakamani.uchu wa madaraka !!!!!!!!!
   
 7. r

  rwazi JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete alivyomteua mbatia akadhani nayeye anaweza kumteua, hivyo akaona njia ya kujipendekeza, afadhali atumie akili ya sungura kuonekana anamshtaki mtu kumbe ni kujitambulisha.
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Tangu lini Raisi akawa muamuzi wa Mhimili wa mahakama? Angoje tuu 2015 kama ana ubavu
   
 9. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Duania kuna majuha , kukata rufaa lazima ifuate nagzi za kimahakama sasa bankimoon, ni mahakama ya rufaa tanzania?mgombea ubunge gani asiyejua sheria namna hiyo?hafai hata kuwa mbunge.Pia kimstkabali un huwa haiingilii masula ya ndani ya nchi.Uchaguzi wa mbunge ni masula ya ndani ya nchi hayawezi kuamliwa na umoja wa mataifa.
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  huyo mtu anapoteza tu mda wake kwa sababu hata uchaguzi ukibatiliwa kukawa kuna uchaguzi lile jimbo hatapita...pale ni pa ndesamburo atake asitake...aanzishe tu shuhuli zingine za kibiashara jamani kwani ni lazima kua mbunge? si akaajiriwe kama wengine
   
 11. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Huyu ndio sungura kweli kweli! Sasa juhudi zote hizi ndio analenga kufanya nini? kwamba akifanikiwa pingamizi dhidi ya Ndesa yeye ndio atakuwa next-in-line ama? pale hapawezi, mi naona kama hawezi kufanya mambo mengine na anafikiri ni lazima awe mbunge, angeanza kujipenyeza maeneo mengine nchini ambapo hapana prominent opposition figures ili aweke himaya yake. Lakini huenda anajaribu kujitambulisha kwa JK ili kutupa karata ya uteuzi viti maalum kama alivyosema mchangiaji mmoja hapa!
   
 12. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  Hao wote aliowapelekea hiyo barua (JK,UWT,IGP,TISS,TAKUKURU) ni washitakiwa pia kwa mwenyezi mungu kwani si watanzania tumemshitakia mwenyezi mungu tunasubiri hukumu yake.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,200
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kwanini asiende kuwashtaki na NATO pia ili wampige na mabomu ndesamburo
   
 14. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni vyema afuata utaratibu aliofanya mwenyekiti wake.
   
 15. Wild fauna

  Wild fauna JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 427
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Sungura naona unatafuta publicity. Sungura naona huna kazi ya kufanya,nenda kakodi shamba huko matombo ukalime matikiti maji.jina zuuuri kumbe kichwan ni upepo tuu
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani sijaelewa..JK atamfanya nini ndesamburo...
   
 17. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 884
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Yaani naiona Ban Ya Maisha inanichungulia kutoka nyuma ya kichaka. Nasepa.
   
 18. V

  Vonix JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Daa!!!wewe umenifurahisha sana ubarikiwe,hivi we sungura kweli unajua taratibu za kesi???umewezaje kwenda kwa bankimoon???sheria za kiamataifa unazijua kweli???huna lolote wewe ni kilaza tu jipanga upya.
   
 19. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Sasa kama huyo jaji alimuonea, kwa nini hasitafute haki kwenye mahakama za juu? Sasa JKilaza atamsaidiaje hapo, si ndiyo mambo ya kuingilia vyombo huru, anyway...walishazoea.
  Ningempa krediti kama angesema kuwa ameamua kukataa rufaa, hili la Ban Kin Moon ....mmmh hata kuku angeweza kufikiria kwanza.
   
 20. kay 18

  kay 18 Senior Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbna kang'ang'ania sana,anania gan na hlo jimbo huyooo,kawageuza jk mahakama ya mwanzo,ban ki moon mahakama kuu
   
Loading...