Ndesamburo apeleka halikopta kusaidia mahututi kwa babu loliondo@@big up baba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndesamburo apeleka halikopta kusaidia mahututi kwa babu loliondo@@big up baba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 11, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,475
  Likes Received: 5,715
  Trophy Points: 280
  Wagonjwa wagoma kuondoka Loliondo  *Wadai viongozi wanazuia baada ya wao kuponywa
  *KKKT yapeleka mafundi kuweka sawa miundombinu

  *Ndesamburo apeleka helikopta kusaidia walio mahututi

  Na Said Njuki, Arusha

  MAELFU ya watu wanaomiminika kwenda Kijiji cha Samunge Loliondo kusaka tiba ya
  magonjwa sugu wamegoma kuondoka bila kunywa dawa wakipinga agizo la serikali na kuwataka wasitishe shughuli hiyo ili kupunguza msongamano na suala la usalama.

  Habari za uhakika zilizopatikana kutoka Kijiji cha Samunge kwa Mchungaji Mwasapile zimeeleza kuwa wagonjwa waliokuwa tayari wamefika huko hawako tayari kuondoka hadi watakapotibiwa, licha ya serikali kuagiza waondoke hadi muda muafaka utakapofika kwa mchungaji huyo kuendelea na tiba.

  “Hili agizo la Serikali limekuja wakati si wake, wao walichotakiwa kufanya ni kuhakikisha wagonjwa hawaondoki majumbani mwao, lakini huwezi kumwagiza mgonjwa aliyoko katika foleni ya tiba kituoni aondoke kabla hajapata tiba bila kujali gharama alizotumia, muda wake na mbaya zaidi alichokifuata hajapata,” alilalamika mtu mmoja aliyejukana kwa jina moja la Ezekiel.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti watu mbalimbali waliohojiwa na Majira walisema uamuzi huo si sahihi kwa kuwa unakwenda kinyume na shauku ya wengi ya kupata tiba hiyo inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile.

  Miongoni mwa waliopinga uamuzi huo ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati likisema uamuzi huo utahatarisha uhusiano mzuri uliopo baina ya serikali na kanisa hilo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Arusha, Askofu wa Kanisa hilo, Thomas Laiser alisema si sawa kusitisha huduma ya Mchungaji Measapile yenye 'elementi' ya kiroho bila kuwahusisha wadau ambao ni kanisa hilo.

  Juzi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Haji Mpanda alisitisha tiba hiyo kwa maelezo kuwa wanasubiri ripoti ya Kamati ya uchunguzi wa tiba hiyo iliyoundwa na wizara hiyo mapema wiki hii hadi kamati hiyo itakapotoa taarifa yake.

  Pia Dkt. Mponda aliitaja sababu zingine kuwa ni kuweza kuichunguza dawa hiyo kisayansi na pia hali mbaya ya kimazingira yanayohatarisha afya za watu na wagonjwa waliofurika katika eneo hilo wakisubiri tiba hiyo mbadala, ya saratani, Ukimwi, kisukari na magonjwa mengineyo.

  Askofu Laiser alisema lililotokea kwa mchungaji huyo si jambo la kisayansi bali ni jambo la kiimani na kimaombi na kuhoji iwapo jambo hilo Mwenyezi Mungu amelikubali kiimani na kimaombi ni vipi utalijaribu kisayansi.

  “Mti huo kwa kabila la Kisonjo unaitwa ‘Olmorjoy’ na wanaamini kuwa una sumu kali, lakini sisi Wamasai tunauita ‘alamkriyaki’ na tulikuwa tukila matunda yak, lakini hata kama ndio huo sasa Mungu ameubariki na watu wanapona wakiwemo mawaziri na viongozi mbalimbali wametoa ushuhuda huo, lakini pia hao wachunguzi wanajua kuwa haiwezekani dawa ya kiroho kupitia maabara,” alisisitiza Askofu Laiser.

  Alishauri huduma hiyo iendelee kadri Mwenyezi Mungu atakavyoamua kwani kinachowaponyesha watu ni imani yao kupitia kikombe alichokiita cha ‘uokovu’ cha Mchungaji Mwasapile.

  “Utakapomwambia mtu yeyote aliyeteseka kwa muda mrefu kuwa tiba imesitishwa ni wazi utasababisha matatizo yasiyokuwa ya lazima, hivyo jambo muhimu ni kuhakikisha serikali inashirikiana na wadau katika kufanikisha tiba hiyo kwa utaratibu mzuri usiokuwa na madhara ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu imara itakayowahakikishia usalama…lakini kuondoa mgonjwa aliyekuwa amefika huko haikubaliki,” alisema kwa msisitizo.

  Askofu Laizer alisema tayari wataalamu wa ujenzi wa kanisa hilo wameondoka kuelekea kijijini huko kuandaa michoro na kutathimini gharama za ujenzi wa mahema na miundombinu mingine kwa kushirikiana na serikali kwa lengo la kuondoa ugumu wa tiba hiyo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana viongozi wa taasisi na mashirika mbalimbali ya kiraia wamedai hizo ni hila za serikali za kuzuia wananchi wake wasipate tiba hiyo, kwani kitendo cha kusitisha tiba hiyo kimefanyika baada ya idadi kubwa ya viongozi serikalini kutibiwa.

  Mkurugenzi wa Shirika la Haki za Binadamu lenye Makao Makuu yake mjini Loliondo la LARETOK, Bw. Ole Ndangoya amesema tangu tiba hiyo ilipoanza miezi kadhaa iliyopita tayari zaidi ya nusu ya viongozi wa taasisi mbalimbali na serikali wameshapatiwa dawa hiyo na anaamini ndiyo sababu ya kusitisha ghafla bila kujali idadi kubwa ya wagonjwa walioko katika foleni wakisubiri.

  Bw. Ndangoya aliyeeleza kuwa neno LARETOK ni neno la kabila la Kimasai lenye maana ya Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu, alisema anakubaliana na uwekaji wa miundombinu murua katika eneo hilo ili kudhibiti uharibifu wa mazingira unaoweza kusababisha afya za watu kuathiriwa, lakini suala la kuweka urasimu wa tiba hiyo halikubaliki na shirika hilo halitanyamazia jambo hilo.

  “Viongozi wa dini, wa serikali wameshafika huko na kunywa dawa hiyo, labda ndicho walichokuwa wakisubiri ili wasitishe tiba hiyo na kuwataka wagonjwa waliotumia fedha, muda na nguvu nyingi kuondoka bila kupata tiba hiyo, jambo hili halikubaliki,” alionya Bw. Ndangoya bila kueleza shirika lake linakusudia kufanya nini baada ya hapo.

  “Kusitisha kwa ajili ya kuweka mazingira yawe mazuri ni utaratibu mzuri, sawa, nakubaliana nao, lakini wengi wamepata dawa na kukiri kuwa wamepona, hivi hao unaowazuiliwa hawana haki hiyo?” alihoji Mkurugenzi huyo.

  Aliongeza Katiba inaainisha kuwa serikali haina dini, bali watu wake ndio wanayo dini, ndio wanaoponywa kwa imani za dini, na iwapo itang’ang’ania kuwa imsajili mchungaji huyo basi serikaili inayo dini ni vema itaje hiyo dini yake.

  Akithibitishwa kusitishwa kwa tiba hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Elias Wawa Lali alisema usitishaji huo ni wa muda ili kutoa nafasi kwa Mchungaji Mwasapile kusajili dawa hiyo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na tayari fomu ameshazipata huku taratibu mzuri za kimazingira zikifanywa ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kuhatarisha afya za watu.

  Alisema hali inazidi kuwa mbaya katika eneo hilo finyu lililoshsheni idadi kubwa ya magari na watu kiasi kwamba hakuna na hakuna njia nyingine mbadala zaidi ya kusitisha tiba hiyo kwa muda na wagonjwa waliyoko huko kuondoka.

  “Serikali haina nia mbaya na tiba hiyo, kinachotakiwa ni usajili ya tiba hiyo na tayari mamlaka husika imeshampatia fomu Mchungaji huyo ili azijaze, lakini kubwa zaidi serikali inashirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuhakikisha hali ya mazingira inaboreshwa kwa kiwango cha juu.

  Hofu yangu ni jinsi ya kudhibiti uingiaji wa wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali lakini tayari suala hilo limewekewa utaratibu wake,” alisema Mkuu huyo kwa njia ya simu jana.

  Naye Richard Konga anaripoti kuwa Mwinjilisti wa KKKT wa Kanisa la Samunge lililokuwa likiongozwa na Mchungaji Masapila, Bw. Daniel Mbario ameiomba serikali iwe bega kwa bega na babu huyo ili kuboresha mazingira na kurahisisha utoaji wa huduma na kurahisisha upatikanaji wa dawa.

  Kwa upande wao watumiaji wa dawa hiyo, akiwemo Paschal Mbise ambaye mdogo wake Philipo Mbise alikufa katika foleni kabla ya kufikia tiba ya pumu baada ya kutoka Hospitali ya Kibong’oto ameiomba serikali kuingilia kati kuboresha huduma katika eneo hi
   
 2. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mhhh!!! Kazi kweli kweli!
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Viva ndesa...
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mambo ya Ndesa Pesa hayo

  Hivi kuna kigogo huko CCM anaweza fanya hivyo?
   
Loading...