Ndesamburo amshangaa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndesamburo amshangaa JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 20, 2007.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,880
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Ndesamburo amshangaa JK

  na Grace Macha, Moshi
  Tanzania Daima

  MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), amesema inashangaza kuona nchi iko katika mgogoro, lakini Rais (Jakaya Kikwete) anaikimbia anakwenda kwenye ziara nje ya nchi.
  Ndesamburo aliyewahi kufanya kazi serikalini wakati wa Awamu ya Kwanza ya utawala wa Mwalimu Julius Nyerere aliyasema hayo jana nyumbani kwake mjini Moshi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

  Alisema, Rais alipaswa kutulia nchini na kushughulikia tatizo lililopo alilodai ni kubwa, kwani kelele za tuhuma za ufisadi zinazopigwa sasa nchini si jambo la kupuuzwa, bali linapaswa kupatiwa ufumbuzi.

  ‘Nchi iko katika mgogoro, nashangaa rais wetu anakimbia nchi wakati huu…anapaswa kulivunja baraza la mawaziri ikibidi afanye kazi kwa muda na makatibu wakuu wa wizara …siyo alivunje leo aliunde kesho, atakuwa hajapata muda wa kutosha kutafakari,” alisema mbunge huyo.

  Hata hivyo, alisema rais anapaswa kutumia muda kutafakari kabla ya kuteua mawaziri wengine ambapo alishauri aunde baraza la mawaziri litakalokuwa dogo, atakaloweza kulimudu.

  Kwa kauli hiyo, Ndesamburo anaingia kwenye mwelekeo unaofanana na kundi la wazee nchini wakiwemo Joseph Butiku (Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere), Joseph Warioba, John Malecela (Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara) na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi waliojitokeza kutoa tamko juu ya tatizo la ufisadi na ukiukwaji wa maadili ya uongozi nchini.

  Septemba 15 mwaka huu, viongozi wa vyama vinne vya upinzani vya CHADEMA, NCCR, TLP na CUF vilitoa tamko jijini Dar es Salaam ambapo Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alitaja majina 11 ya viongozi waandamizi serikalini aliowatuhumu kuwa mafisadi.

  Tangu kutolewa kwa tamko hilo, baadhi ya waliotuhumiwa wamejitokeza hadharani na kukanusha shutuma hizo na kuahidi kulifikisha suala hilo mahakamani, lakini mpaka sasa hakuna aliyekwenda kufungua mashitaka.

  Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete akizungumza kwenye hafla ya harambee iliyoandaliwa jijini Arusha na Kanisa la KKKT, alisema serikali itawachunguza wote waliotuhumiwa kwa rushwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria iwapo watabainika kuhusika.

  Katika hatua nyingine, Ndesamburo alishauri serikali kuacha kutoa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa, badala yake fedha hizo zipelekwe kwenye majimbo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

  Alisema vyama vya siasa ni mali ya wanachama, hivyo vinapaswa kujiendesha kwa kile alichosema fedha zinazoingizwa kwenye vyama hivyo hutumiwa kwa masilahi yao wenyewe na si ya taifa.
   
 2. B

  BroJay4 JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2007
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kingwendu tumempa muda,ngoja atalii tu,siku akirudi akute ikulu haipo asimlaumu mtu,yaani nimeamini JK bin Kingwendu ni zuzu sijawahi kuona,mnafiki mkubwa,.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Oct 20, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kuvunja baraza la mawaziri na kujunda jipya bado ni Usanii mtupu. Wananchi wanataka kuona waliohujumu uchumi wetu wakichukuliwa hatua kisheria.
  Tuhuma zifanyiwe uchunguzi na kikao maalum cha bunge letu ambacho hakitakuwa na wajumbe wenye uhusiano na watuhumiwa, kama vile wanavyochagua member of the Jury...
  Kuwaondoa madarakani hawa jamaa bado kutawapa Utajiri haramu ambao ni lazima uchunguzwe!..
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  NDESA na wewe ulisema kuwa lowassa alihonga wabunge akishirikiana na manji, uchunguzi haujaisha bado?

  watetezi wa kuwa tumpe muda JK je mnakumbuka kesi hii ilivyuomalizwa kihuni na TAKUKURU pamoja na bunge yaani spika?

  Msishangfae na huu ufisadi nao wakaja na majibu kuwa rais amefunga mjadala basi huu ndio uwe mwisho wa mambo.

  Kama anashauriwa na huyu ......... bin mzee unategemea aweze kufanya maamuzi ?
   
 5. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2007
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Kwani ndesa hajui kuwa JKM ni msanii?
  JK anatafuta nchi ya kukimbilia hapo baadae na ndio maana anakwenda zile nchi ambazo huwa haziruhusu wahalifu kukabidhiwa nchi zenye sheria za kihivyo ataponea vatican bila shaka.
   
Loading...