Mwalimu Makini
Member
- Dec 5, 2009
- 65
- 23
Haya Moshi kumekucha.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Moshi Mjini kimefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Kaloleni iliyoko pembezoni mwa mji wa Moshi.
Kata hiyo inaongozwa na Mhe. Diwani Mwita ambaye alishinda udiwani kwa kupitia tiketi ya CCM mwaka 2005. Kwa kweli CCM walikuwa wameiimarisha ngome yao katika kata hii ya Kaloleni.
Naam leo majira ya saa 10 jioni msururu wa viongozi wa CHADEMA ulianza kuhutubia mkutano huo wa hadhara ambao ulikuwa umehudhuriwa na watu wengi sana kinyume na ilivyozoeleka katika mikutano ya CCM katika mji wa Moshi.
Aliposimama Mzee Ndesamburo, mkutano ulilipuka kwa shangwe kiasi cha kumlazimisha kusubiri kwa muda watu watulie.
Ndesamburo alianza kwa kuwataja watu mashuhuru walioamua kujiunga na CHADEMA na kujiondoa CCM. Aliyekuwa wa Kwanza kupokelewa ni aliyekuwa Katibu wa CCM na mwanamikakati mkuu katika kata ya Kaloleni Ndg. Shaban Omary Msuya.
Bwana Msuya alifuatiwa na kundi lote la vijana wa CCM wa kata ya Kaloleni ambao walikabidhi kadi za CCM na kupokea za CHADEMA wapatao 33. Baada ya hapo viongozi kadhaa wa matawi wa CCM walitokeza na kudai kadi na hivyo kulazimisha mkutano kubadilika kuwa duka la kadi za CHADEMA.
Hadi mkutano unafungwa kadi zote 350 zilizopelekwa katika mkutano huo zilikuwa zimeisha hivyo kuwalazimisha maofisa wa CHADEMA kata ya Kaloleni na Wilaya ya Moshi kubaki wakiorodhesha majina ya wahitaji wa kadi.
Hata hivyo Mhe. Ndesamburo hakutamka kuridhia kugombea tena ubunge katika jimbo la Moshi Mjini katika mkutano huo, licha ya kupambwa sana na viongozi wengine wa chama waliomtangulia kuzungumza
Ama kweli Moshi kumekucha.