Ndesamburo aipasua CCM Moshi

Dec 5, 2009
65
23
Haya Moshi kumekucha.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Moshi Mjini kimefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Kaloleni iliyoko pembezoni mwa mji wa Moshi.

Kata hiyo inaongozwa na Mhe. Diwani Mwita ambaye alishinda udiwani kwa kupitia tiketi ya CCM mwaka 2005. Kwa kweli CCM walikuwa wameiimarisha ngome yao katika kata hii ya Kaloleni.

Naam leo majira ya saa 10 jioni msururu wa viongozi wa CHADEMA ulianza kuhutubia mkutano huo wa hadhara ambao ulikuwa umehudhuriwa na watu wengi sana kinyume na ilivyozoeleka katika mikutano ya CCM katika mji wa Moshi.

Aliposimama Mzee Ndesamburo, mkutano ulilipuka kwa shangwe kiasi cha kumlazimisha kusubiri kwa muda watu watulie.
Ndesamburo alianza kwa kuwataja watu mashuhuru walioamua kujiunga na CHADEMA na kujiondoa CCM. Aliyekuwa wa Kwanza kupokelewa ni aliyekuwa Katibu wa CCM na mwanamikakati mkuu katika kata ya Kaloleni Ndg. Shaban Omary Msuya.

Bwana Msuya alifuatiwa na kundi lote la vijana wa CCM wa kata ya Kaloleni ambao walikabidhi kadi za CCM na kupokea za CHADEMA wapatao 33. Baada ya hapo viongozi kadhaa wa matawi wa CCM walitokeza na kudai kadi na hivyo kulazimisha mkutano kubadilika kuwa duka la kadi za CHADEMA.

Hadi mkutano unafungwa kadi zote 350 zilizopelekwa katika mkutano huo zilikuwa zimeisha hivyo kuwalazimisha maofisa wa CHADEMA kata ya Kaloleni na Wilaya ya Moshi kubaki wakiorodhesha majina ya wahitaji wa kadi.

Hata hivyo Mhe. Ndesamburo hakutamka kuridhia kugombea tena ubunge katika jimbo la Moshi Mjini katika mkutano huo, licha ya kupambwa sana na viongozi wengine wa chama waliomtangulia kuzungumza

Ama kweli Moshi kumekucha.
 
Ukiondoa ushabiki wa kuuza kadi...kuna sera yoyote iliyowakuna wana wa Karoleni?

aliyekuambi watu wanataka kusikiliza sera nani?mbona sera ya kasi mpya hamuilewi lakini bado mnajipanga barabarani kumshangilia mwenyekiti wenu
 
Ukiondoa ushabiki wa kuuza kadi...kuna sera yoyote iliyowakuna wana wa Karoleni?

Sidhani kama watanzania wanataka sera (maneno matupu), watanzania wanataka maendeleo yanayo pimika. Wakienda shule wakute walimu, vitabu, maabara n.k. Wakienda hospitali wakute madawa, madaktari n.k.

Hizo sera za CCM za miaka 33 hadi leo ni maneno tu.
 
Ukiondoa ushabiki wa kuuza kadi...kuna sera yoyote iliyowakuna wana wa Karoleni?

Sera ni nini katika nchi hii, tulishaambiwa maisha bora kwa kila mtanzania je Sera hiyo inatekelezeka. tumeshapata hayo maisha Bora? ni mwaka wa tano sasa!!! unataka NDESA-PESA aseme nini? acha aendelee kupokea kadi na sasa atapokea mpaka Bendera nini kadi
 
haya moshi kumekucha.
chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) katika jimbo la moshi mjini kimefanya mkutano wa hadhara katika kata ya kaloleni iliyoko pembezoni mwa mji wa moshi.

kata hiyo inaongozwa na mhe. Diwani mwita ambaye alishinda udiwani kwa kupitia tiketi ya ccm mwaka 2005. Kwa kweli ccm walikuwa wameiimarisha ngome yao katika kata hii ya kaloleni.

naam leo majira ya saa 10 jioni msururu wa viongozi wa chadema ulianza kuhutubia mkutano huo wa hadhara ambao ulikuwa umehudhuriwa na watu wengi sana kinyume na ilivyozoeleka katika mikutano ya ccm katika mji wa moshi.

aliposimama mzee ndesamburo, mkutano ulilipuka kwa shangwe kiasi cha kumlazimisha kusubiri kwa muda watu watulie.
ndesamburo alianza kwa kuwataja watu mashuhuru walioamua kujiunga na chadema na kujiondoa ccm. Aliyekuwa wa kwanza kupokelewa ni aliyekuwa katibu wa ccm na mwanamikakati mkuu katika kata ya kaloleni ndg. Shaban omary msuya.

bwana msuya alifuatiwa na kundi lote la vijana wa ccm wa kata ya kaloleni ambao walikabidhi kadi za ccm na kupokea za chadema wapatao 33. Baada ya hapo viongozi kadhaa wa matawi wa ccm walitokeza na kudai kadi na hivyo kulazimisha mkutano kubadilika kuwa duka la kadi za chadema.

hadi mkutano unafungwa kadi zote 350 zilizopelekwa katika mkutano huo zilikuwa zimeisha hivyo kuwalazimisha maofisa wa chadema kata ya kaloleni na wilaya ya moshi kubaki wakiorodhesha majina ya wahitaji wa kadi.

hata hivyo mhe. Ndesamburo hakutamka kuridhia kugombea tena ubunge katika jimbo la moshi mjini katika mkutano huo, licha ya kupambwa sana na viongozi wengine wa chama waliomtangulia kuzungumza

ama kweli moshi kumekucha.


hizo ni mbio za skafuni huishia ukingoni
 
Tunamsubiri Ngawaiya alisema kuwa atamwondoa Ndesa Moshi. Sijui kama ataweza
 
Ukiondoa ushabiki wa kuuza kadi...kuna sera yoyote iliyowakuna wana wa Karoleni?

Nidhahiri kwamba kadi ya chama cha siasa sii pambo useme mtuananuanua ili akaweke ndani au amtumie mpenzie ka zawadi ya valentine. Hawa waheshimiwa wametafakari utendaji na uwajibikaji wa chama na viongozi wao na hasa kwa kuzingatia kwamba chama chao ndicho kinashuikilia serikali ya kaloleni.
Mkuu utakua umeteleza na utakua umewakosea hesma kama utataka tuamini watu hawa 350 wamejiunga na chama hadharani hasa kwenye nchi hii ambayo mpinzania anaonekana muasi.
Hongera chadema, hongera Ndesa na hongereni wana wa kaloleni na moshi kwa ujumla. hili liwe fundisho kwa sisi sote popote tulipo. Nikweli haina maana yoyote kupiga kelele bila kuchukua hatua.Wakati wa kuchukua hatua ni sasa. wewe na mimi popote tulipo tuwe chachu ya mabadiliko.

"Mabadiliko ya kweli hayataletwa na watu wale wale, wa chama kile kile cha mafisadi atai kwa kasi na ari mpya" Tusitegemee miujiza bali tuwe sehemu ya kuileta miujiza
 
Back
Top Bottom