Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,023
- 1,609
NDEJEMBI: WATUMISHI WA UMMA 1,477 WASIMAMISHWA KAZI 2015-2022
Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deogratius Ndejembi amesema Watumishi wa Umma 1,477 wamesimamishwa kazi kwa kukiuka Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia nidhamu katika Utumishi wa Umma kuanzia mwaka 2015 hadi 2022
Ameyasema hayo leo Jumatatu Aprili 11, 2022 wakati akijibu Swali la Nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi aliyehoji sababu za mashauri yanayoendelea kusikilizwa na Tume ya Utumishi wa Umma kuchukua muda mrefu sana
Ndejembi ameongeza kuwa Watumishi 598 wamekata rufaa Tume ya Utumishi wa Umma, ambapo rufaa 411 zina maelezo yaliyokamilika na 187 hazina vielelezo na zimerudishwa kwa Waajiri kwa Mamlaka za Nidhamu ili ziweze kufanyiwa kazi