Ndege zisizo na rubani kutoa msaada wa kitabibu nchini

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Wana jamvi
Salaam.Amani iwe kwenu.

Serikali ya Uingereza inajiandaa kufadhili mpango wa kutoa huduma za afya nchini kwa kutumia ndege zisizo na rubani aina ya Ziplines au "zip
drone"huduma hizo ni kusambaza damu na dawa mbalimbali katika maeneo mengi kwa muda mfupi, Aidha lengo la kufanya hivyo
linasemekana ni kupunguza umbali wa kuwafikia walengwa na kwa wakati muafaka, watalaamu wa Uingereza
wamepongeza hatua hiyo.

Aidha wameonya ndege hizo zina ukoma wa kutoa huduma kwa binaadamu, Aidha, huduma hizo pia zinalenga kutolewa
katika nchi nyingi za Afrika zikiwemo Rwanda,
Tanzania halafu Botswana na nchi nyingine.

Chanzo: BBC
 
Wasiwasi wangu wasije wakawa wanaanza kuangalia mipaka yetu ili waliumue wenyewe kwa wenyewe Waafrika, maana utasikia ooh chemchem fulani ipo Rwanda mara ziwa x lipo kwa Y ngoja tuone.
 
Duhh, kwahiyo wanakuja na Damu zao? Masela tuchangamkie Damu za kizungu hizo, labda tutaweza fikiri kama Binadamu wa Dunia yaleo, kama tukuwa na damu za kizungu kwenye body system zetu.
 
Duhh, kwahiyo wanakuja na Damu zao? Masela tuchangamkie Damu za kizungu hizo, labda tutaweza fikiri kama Binadamu wa Dunia ya yelo, kama tukuwa na damu za kizungu kwenye body system zetu.

Hahahahahaha we jamaa wewe hahahhaha duuh kwahiyo mkono mmoja tutaondoa za kibongo mkono mwingine zinaingia za kizungu dwiiiii dwiiii dwiiii
 
Duhh, kwahiyo wanakuja na Damu zao? Masela tuchangamkie Damu za kizungu hizo, labda tutaweza fikiri kama Binadamu wa Dunia yaleo, kama tukuwa na damu za kizungu kwenye body system zetu.
Komenti ya kitwana kabisa kupata kuisoma ndani ya mwaka huu..utwana wa hali ya chini kabisa.
 
Hiyo ni poa Rwanda walishaanza bado hatujachelewa .
c6b1ab205012af5c70a63c2493c27701.jpg
 
Kama tunawaza na tuko bize na Bombadia wakati wazungu wamevuka Bahari na milima kuja kutasidia kwenye afya maana wameona kunatatizo - kweli ni Inferior.
Sasa wewe kila kichopostiwa humu unakichulia serious halafu unajiabisha na kujitukana very sad.
 
Did we ask for this au ni ile tabia ya kukubali chochote kwakuwa tu ni msaada?
Was it in our plans or we just take because the idea looks interesting?
Is it good for our national security?
Do we have the 'said' blood and medicines at the volume where we need drones to dispatch. ?
Are there any cost sharing or it's help 100%?
Do we take part in the event in terms of human resource ? Are they handing us the drones or they operate them themselves?

We have to ask some questions at least maana nimeshakata tamaa na IQ ya mtu anayetuongoza.
 
Wataoperate wenyewe lakini wakwetu afya watakuwepo Kuangalia visivyoonekana Watacheka visivyochekesha, Watasikia visivyosikika
 
Sasa wewe kila kichopostiwa humu unakichulia serious halafu unajiabisha na kujitukana very sad.
Wewe ndie uliyechukilia serious na ukanitukana kwa post yangu, wakati mimi nimeposti kama utani kwahali halisi tuliyonayo.
 
Hizi ndege (Zips) aka Drones nadhani wazungu hawataki athari kwao. Sisi Tz, Malawi , Nepal na Rwanda ndio wanatufanyia testing ground kwao.
Sijawahi sikia huko kwao.

Hizi ndege zina iwezo wa kubeba mzigo wa 1.5kg.

Issue ya damu, hawa wazungu ni wa kuangaliwa sn. Kuna kipindi zilikuja Condom shehena ya meli zina HIV (planted). Je issue ya damu itakuweje? Hawawezi kuzamisha virus? Hawawezi kuwa na box 2 , moja feki?

Tusikurupukie vitu. Tufanye tafiti kwanza. Siyo kila kitu YES!!
 
Back
Top Bottom