Ndege zinahitajika sana, tupunguze siasa zisizo na faida

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,489
13,608
Wiki mbili zilizopita nilikuwa wilaya ya Karatu. Nilijionea jinsi gani watu walivyo na kasi ya kujenga nyumba za wageni (lodges).

Watu wamewekeza fedha nyingi kwenye lodges ambazo ni maalum kwa watalii wanaokuja nchini. Mandhari ya Karatu ni nzuri mno, mzungu anayekuwa amepumzika kwenye hizi nyumba anapata mtazamo mzuri sana wa milima iliyoja miti yenye rangi nzuri ya kijani.

Hii nchi imebarikiwa sana, tunayo pwani nzuri, tunazo mbuga, tunao utajiri mwingi. Ni jambo la kushangaza kumuona mtu anapinga ule umuhimu wa Tanzania kutokuwa na shirika la ndege lenye ndege nyingi.

Hata huyo Mungu pengine anatushangaa kwa jinsi ambavyo ametukirimia kila aina ya utajiri wa maliasili halafu sisi tunakuwa masikini kwa sababu ya uzembe wetu wenyewe.

Ni jambo la maana kwa Tanzania kujitangaza kupitia fulana za wachezaji wa Sunderland ya ligi kuu ya Uingereza.

Na ni jambo jema zaidi kwa nchi inayojitangaza kwenye ligi bora ulimwenguni kuwa na ndege zake yenyewe ili kuwabeba watalii wanaopatikana kupitia tangazo kubwa la kibiashara linaloendelea kuonekana kila Sunderland inapocheza mechi.

Sekta ya anga ni kama inadharaulika, lakini inao uwezo mkubwa wa kuliingizia pato la maana taifa letu.

Tunazihitaji sana ndege haswa kwa maana ya safari za kimataifa. Kupambana na umasikini ibakie kuwa ndio lengo kuu la serikali lakini uagizaji wa ndege kwa lengo la kuifanya ATCL itambe kimataifa, ni muhimu sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom