Ndege zimeshatumia tril 1.8 mpka sasa, hiyo faida ya bil 30 ina ukweli? Washarudisha hasara ya bil 223.1 na manunuzi hadi kupata faida?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mwenyekiti wa Kamati bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Albert Ntabaliba ameeleza kuwa kwa miaka miwili mfululizo tangu serikali inunue ndege mbili aina ya Bombardier, zimeleta hasara ya Shilingi Bilioni 109.3 + Bilioni 113.8 = Bilioni 223.1.

Yaani, mwaka wa fedha 2015/2016 taifa limepata hasara ya Shilingi Bilioni 109.3 na mwaka wa fedha 2016/2017 (uliomalizika Septemba 2017) tumepata hasara ya shilingi bilioni 113.8.

Mwaka 2018 tukaambiwa imepatikana faida ya bil 28 lakini shirika hili halikukaguliwa wala taarifa ya fedha haikutolewa mpaka leo.

Mwaka huu 2019 tunaaambiwa lina faida ya bil 30 najiuliza haya na mauzo ghafi au faida?

Hili shirika wame breack even lini? Yaani manunuzi ya tril 1.8 hizi ndege zimeshazalisha kwa miaka mitatu hii ya hasara?

Yaani kwa miaka mitatu hayo madeni (hasara) isharudi? Manunuzi ya ndege. Yamesharudi hadi kupata faida ya bil 30? Na kwann hataki kukaguliwa?
 
Watu wanataka faida ya Direct. Mbona hamuhoji hizi barabara zinazojengwa kila siku zitarudisha faida baada muda gani! ?
Hivi mnadhani serikali ipo kupata faida zaidi.

Je,mmejiuliza indirect profits kwa wafanyabiashara wa bidhaa za Kilimo na ajira zingine.

Biashara gan ya ndege hapa bongo ya kutumia ndege kusafirisha mizigo?
 
Kutupatia taarifa ya faida ya hizo ndege ni sawa na kujifunga goli. Lengo la kufufua shirika la ndege ni kusisimua sekta ya utalii. Faida ya kuwa na ndege huwa inajificha ktk mafanikio ya sekta zingine. Sasa hii faida mnayotuaminisha sitashangaa kama ni ya kupika.
 
Mwenyekiti wa Kamati bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Albert Ntabaliba ameeleza kuwa kwa miaka miwili mfululizo tangu serikali inunue ndege mbili aina ya Bombardier, zimeleta hasara ya Shilingi Bilioni 109.3 + Bilioni 113.8 = Bilioni 223.1.

Yaani, mwaka wa fedha 2015/2016 taifa limepata hasara ya Shilingi Bilioni 109.3 na mwaka wa fedha 2016/2017 (uliomalizika Septemba 2017) tumepata hasara ya shilingi bilioni 113.8.

Mwaka 2018 tukaambiwa imepatikana faida ya bil 28 lakini shirika hili halikukaguliwa wala taarifa ya fedha haikutolewa mpaka leo.

Mwaka huu 2019 tunaaambiwa lina faida ya bil 30 najiuliza haya na mauzo ghafi au faida?

Hili shirika wame breack even lini? Yaani manunuzi ya tril 1.8 hizi ndege zimeshazalisha kwa miaka mitatu hii ya hasara?

Yaani kwa miaka mitatu hayo madeni (hasara) isharudi? Manunuzi ya ndege. Yamesharudi hadi kupata faida ya bil 30? Na kwann hataki kukaguliwa?
Pascal Mayalla tusaidie kujibu
 
Back
Top Bottom