Ndege Zimbabwe zarejesha safari nchini

BabuK

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
1,845
329

Ndege ya Zimbabwe.


USHIRIKIANO wa Tanzania na Zimbabwe katika utalii utaongezeka zaidi baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Zimbabwe kurejesha tena safari za kuja nchini, baada ya kuacha kuja kwa takribani miaka saba sasa.

Kwa mara ya mwisho ndege ya nchi hiyo ilikuja nchini mwaka 2009 huku ile ya Tanzania (ATCL) ilitua katika ardhi ya Zimbabwe kwa mara ya mwisho mwaka 2004, ikiwa ni miaka 12 sasa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora aliyemwakilisha Waziri wa Ujenzi, Profesa Makame Mbarawa alilipongeza Shirika la Ndege la Zimbabwe kwa kuanza tena safari zake huku ikiinua sekta ya utalii.

Alisema ndege hiyo itasaidia wanaotaka kutembelea vivutio vya utalii kama Maporomoko ya Victoria, Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro sasa wataweza kusafiri moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili. Ndege hiyo itakuwa inakuja nchini mara mbili kwa wiki, Jumanne na Jumamosi.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Maendeleo ya Miundombinu wa Zimbabwe, Dk Jorum Gumbo alisema kuanza tena safari za ndege hiyo kutasaidia kukuza utalii na kuinua uchumi wa nchi hiyo.

Alisema watalii wanaokuja Tanzania na Zanzibar sasa watakuwa na nafasi ya kwenda moja kwa moja Zimbabwe kwa kutumia ndege, tofauti na huko nyuma iliwabidi kupitia nchi nyingine, kitu ambacho ni gharama kubwa.

Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Edzai Chimonyo alisema ndege hiyo itasaidia sana kusafirisha watalii, wafanyabiashara na watu wa kawaida kusafiri kati ya nchi hizo mbili kwa shughuli mbalimbali.

Alisema Wazimbabwe wamekuwa wakitumia sana bandari ya Dar es Salaam, ambapo mbali na shughuli nyingine, pia wamekuwa wakiingiza magari zaidi ya 300 kwa mwezi kupitia bandari hiyo.

Chanzo: HabariLeo
 
Hao Air Zimbabwe nawapa mwezi mmoja watakusanya vyao! yaani kabisa Mtanzania asafiri toka hapa kwenda Zimbabwe, kwenda Victoria Falls! au hata kama ni biashara ipi? maana wafanyabiashara wetu wengi ni "Wauza Juisi" wengi huishia fastjet. Hata kama ni connections Air Zimbabwe zaidi ya Johannesburg labda Lusaka & Kariba (Zambia) tu.
 
Pamoja na vikwazo ilivyowekewa Zimbabwe kiasi cha kusababisha kuyumba kwake kwa uchumi,kumbe bado ina miliki Ndege za masafa marefu,Tanzania inashindwa nin? au inakosea wapi kumiliki Ndege zake
 
Back
Top Bottom