Ndege za Malawi zafungasha virago Ziwa Nyasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndege za Malawi zafungasha virago Ziwa Nyasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Aug 9, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  SIKU chache baada ya Serikali kuzitaka ndege zinazozunguka Ziwa Nyasa upande wa Tanzania kufanya utafiti wa mafuta kuondoka mara moja, Serikali ya Malawi imetii na kuziondoa kampuni zinazofanya kazi hiyo katika ziwa hilo.

  Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake Jumatatu iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliitaka Malawi kuziondoa ndege na kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta katika eneo hilo kwa kuwa ni mali ya Tanzania

  Mbali na Waziri Membe, viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na kuitaka Malawi iache uchokozi ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa.

  Wakati Sitta akiwataka Watanzania kuendelea na shughuli zao bila hofu kwa kuwa Serikali iko tayari kwa tishio lolote, Lowassa alisisitiza kuwa Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.

  Jana kwa nyakati tofauti, Wakuu wa Wilaya nne zilizo mpakani mwa Tanzania na Malawi za Ileje, Mbozi, Mbeya, Kyela na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro walieleza kuwa mara baada ya kauli hizo, ndege hizo za Malawi ziliondoka na kampuni zilizokuwa zikitafiti mafuta katika Ziwa Nyasa zimeacha.

  "Hapa tuko cool (tulivu) kabisa tangu zile ndege zilipoacha kuruka, tofauti na hizo kauli zinazotolewa na viongozi wa Serikali (ya Malawi)," alisema Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Dk Michael Kadeghe na kuongeza:
  "Hapa niko kwenye Sherehe za Nanenane na Malawi wana banda lao nimetoka kulitembelea. Hali iko shwari, tunaendelea na uhusiano kama kawaida."

  Kuhusu mradi wa Bonde la Mto Songwe unaozihusisha Wilaya za Mbozi, Ileje, Rungwe, Mbeya Vijijini na Malawi, Dk Kadeghe alisema bado haujaathirika.

  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Vijijini, Norman Sigalla alisema mgogoro huo kwa sasa uko kwenye hatua za awali hivyo ni vigumu kusema kuwa nchi inaweza kuingia vitani au la.

  Kuhusu Mradi huo wa Bonde la Mto Songwe, Sigalla alisema bado haujaathirika kwa kuwa hakuna aliyekiuka makubaliano.

  Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sengamule alisema: "Hapa kwetu tuko shwari kabisa, hata juzi nilikuwa na viongozi wa Malawi waliokuja hapa kwa ajili ya Mradi wa Bonde la Mto Songwe tukajadiliana jinsi ya kuuendeleza. Hata jana nimepita eneo la mpakani sijaona tishio lolote, labda huko Kyela."

  Kwa upande wake, Kandoro alisema: "Mimi naona tuko shwari, hakuna tishio lolote. Nadhani ulimsikia juzi Waziri wa Mambo ya Nje akisema. Tuache diplomasia ifanye kazi yake. Uhusiano wetu wa kidiplomasia na Malawi haujaharibika."

  Kyela kazi kama kawaida

  Wakazi wa Kyela wakiwamo wavuvi wanaofanya shughuli zao katika Ziwa Nyasa wamesema wanaendelea na kazi zao za kila siku kama kawaida licha ya kuibuka kwa mgogoro huo wa mpaka.

  Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema licha ya kusikia mgogoro huo, bado wameendelea kuwa na uhusiano mzuri kati yao na Wamalawi.

  Walisema kuwa tangu kuibuka kwa mjadala kuhusiana na mpaka huo wa Ziwa Nyasa, hakuna tatizo ambalo limeonekana miongoni mwao na kwamba muda wote wanaendelea na shughuli zao za mpakani.

  Mkazi wa Kata ya Kabanga Songwe, Lusajo Mwakapisu alisema hakuna tukio lolote ambalo limeweza kuripotiwa kuhusiana na mgogoro unaoendelea baina ya nchi hizo mbili.

  Alisema wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na hakuna kizuizi chochote mpakani mwa Tanzania na Malawi na kwamba muda wote wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia nchi hiyo jirani.

  Wavuvi katika ziwa hilo walisema muda wote wapo kazini na hakuna kikwazo chochote kwao tangu kuripotiwa kwa mgogoro huo.

  "Sisi hapa kama unavyoona mwenyewe tunaendelea na kazi yetu ya uvuvi kila siku. Hakuna mgeni yeyote aliyeonekana kuja na kutusemesha lolote kuhusiana na mgogoro huo," alisema mvuvi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Joseph.

  Kiini cha mgogoro

  Waziri Membe akizungumzia kiini cha mgogoro huo, alisema ni hatua ya Serikali ya Malawi kushikilia msimamo kuwa eneo lote la Ziwa Nyasa lipo Malawi wakati Tanzania inasema mpaka upo katikati ya Ziwa.

  "Wenzetu wanadai ziwa lote lipo Malawi lakini, nyaraka zilizotengenezwa na wakoloni wa Kiingereza mwaka 1928 na 1938 zinaonyesha kuwa mpaka wa ziwa hilo upo katikati," alisema.

  Alisema hoja ya Tanzania ina nguvu kulingana na sheria za kimataifa kwa vile tatizo kama hilo linafanana na mgogoro uliokuwapo baina ya Cameroon na Nigeria. Alisema katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Dunia, iliamuliwa kuwa mpaka baina ya nchi hizo mbili upite katikati ya Ziwa Chad ukifuata msitari ulionyooka.

  Chanzo: MWANANCHI
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Tanzania tunapaswa kulitatua swala hili mpaka tuone mwisho wake na siyo kukaa kimya tena huwezi jua wanajipangaje usikute wameona mziki wa tanzania kwa sasa hawauwezi hivyo wanajipanga upya..
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Mimi nilivokuwa nafuatilia kwenye media na hata bungeni nilihisi kuwa kuna tension kubwa sana kiasi hata labda shuguli za uvuvi zimesimama na wananchi mpakani wanahamishwa kumbe haikuwa hivo, vyombo vya habari wakati mwingine wanaongeza chumvi mno!
   
 4. l

  leloson Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jaman hali kule si shwari, kuna jamaa angu yupo maeneo ya ileje anasema zile ndege bado zipo around.
  gazet la mwananchi sio principo lazima tupate "updates from the ground......"
   
 5. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  I believe Diplomatic means rather than the WAR games in my computer which is full on Viruses and can corrupt with any body at any time.
   
 6. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Kutoziona ndege za Wamalawi zikiruka haimaanishi kuwa wameufyata na hivyo wameziondoa. Inawezekana wakawa wamemaliza utafiti wao, au pengine wamehamia upande mwingine au wameamua kupumzika kidogo. Sijapenda sana mwandishi kutumia statement ya RC wa Mbeya kuthibitisha Malawi kuondoa ndege zake (eti kwakuwa wananchi wa mwambao wa Ziwa wamemwambia hivyo) na kusitisha utafiti, kwakuwa RC wa Mbeya sio msemaji wa Serikali ya Malawi. Hapa Serikali yetu kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje inabidi ipate msimamo/statement kutoka kwa wenzao wa Malawi kuhusu hili. Vinginevyo tutadanganyana tu hapa.
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mimi ningeamini kama tu maneno hayo yangetolewa na viongozi wa nchi hizo mbili. Vinginevyo ni porojo tu. Retreat is not a surrender.
   
 8. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Hawa ma-RC ni chumia tumbo wanataka kumridhisha JK kwani wanamjua ni DHAIFU akiambiwa mambo shwari anajua kweli.Kazi Jk ANAYO tunataka mipaka yetu iwe salama vinginevyo hatoki 2015 kwa usalama
   
 9. k

  kundaseni meena Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa tugeukie upande wa migomo na kuanza kuwachimbisha mafisadi wa tanesco.
   
 10. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Godffrey Kahango, Kyela na Elias Msuya, Dar | Wednesday, 08 August 2012 | Mwananchi

  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe

  SIKU chache baada ya Serikali kuzitaka ndege zinazozunguka Ziwa Nyasa upande wa Tanzania kufanya utafiti wa mafuta kuondoka mara moja, Serikali ya Malawi imetii na kuziondoa kampuni zinazofanya kazi hiyo katika ziwa hilo.

  Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake Jumatatu iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliitaka Malawi kuziondoa ndege na kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta katika eneo hilo kwa kuwa ni mali ya Tanzania.

  Mbali na Waziri Membe, viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na kuitaka Malawi iache uchokozi ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa.

  Wakati Sitta akiwataka Watanzania kuendelea na shughuli zao bila hofu kwa kuwa Serikali iko tayari kwa tishio lolote, Lowassa alisisitiza kuwa Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.

  Jana kwa nyakati tofauti, Wakuu wa Wilaya nne zilizo mpakani mwa Tanzania na Malawi za Ileje, Mbozi, Mbeya, Kyela na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro walieleza kuwa mara baada ya kauli hizo, ndege hizo za Malawi ziliondoka na kampuni zilizokuwa zikitafiti mafuta katika Ziwa Nyasa zimeacha.

  "Hapa tuko cool (tulivu) kabisa tangu zile ndege zilipoacha kuruka, tofauti na hizo kauli zinazotolewa na viongozi wa Serikali (ya Malawi)," alisema Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Dk Michael Kadeghe na kuongeza:

  "Hapa niko kwenye Sherehe za Nanenane na Malawi wana banda lao nimetoka kulitembelea. Hali iko shwari, tunaendelea na uhusiano kama kawaida."

  Kuhusu mradi wa Bonde la Mto Songwe unaozihusisha Wilaya za Mbozi, Ileje, Rungwe, Mbeya Vijijini na Malawi, Dk Kadeghe alisema bado haujaathirika.

  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Vijijini, Norman Sigalla alisema mgogoro huo kwa sasa uko kwenye hatua za awali hivyo ni vigumu kusema kuwa nchi inaweza kuingia vitani au la.

  Kuhusu Mradi huo wa Bonde la Mto Songwe, Sigalla alisema bado haujaathirika kwa kuwa hakuna aliyekiuka makubaliano.

  Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sengamule alisema: "Hapa kwetu tuko shwari kabisa, hata juzi nilikuwa na viongozi wa Malawi waliokuja hapa kwa ajili ya Mradi wa Bonde la Mto Songwe tukajadiliana jinsi ya kuuendeleza. Hata jana nimepita eneo la mpakani sijaona tishio lolote, labda huko Kyela."

  Kwa upande wake, Kandoro alisema: "Mimi naona tuko shwari, hakuna tishio lolote. Nadhani ulimsikia juzi Waziri wa Mambo ya Nje akisema. Tuache diplomasia ifanye kazi yake. Uhusiano wetu wa kidiplomasia na Malawi haujaharibika."

  Kyela kazi kama kawaida

  Wakazi wa Kyela wakiwamo wavuvi wanaofanya shughuli zao katika Ziwa Nyasa wamesema wanaendelea na kazi zao za kila siku kama kawaida licha ya kuibuka kwa mgogoro huo wa mpaka.

  Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema licha ya kusikia mgogoro huo, bado wameendelea kuwa na uhusiano mzuri kati yao na Wamalawi.

  Walisema kuwa tangu kuibuka kwa mjadala kuhusiana na mpaka huo wa Ziwa Nyasa, hakuna tatizo ambalo limeonekana miongoni mwao na kwamba muda wote wanaendelea na shughuli zao za mpakani.

  Mkazi wa Kata ya Kabanga Songwe, Lusajo Mwakapisu alisema hakuna tukio lolote ambalo limeweza kuripotiwa kuhusiana na mgogoro unaoendelea baina ya nchi hizo mbili.

  Alisema wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na hakuna kizuizi chochote mpakani mwa Tanzania na Malawi na kwamba muda wote wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia nchi hiyo jirani.

  Wavuvi katika ziwa hilo walisema muda wote wapo kazini na hakuna kikwazo chochote kwao tangu kuripotiwa kwa mgogoro huo.

  "Sisi hapa kama unavyoona mwenyewe tunaendelea na kazi yetu ya uvuvi kila siku. Hakuna mgeni yeyote aliyeonekana kuja na kutusemesha lolote kuhusiana na mgogoro huo," alisema mvuvi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Joseph.

  Kiini cha mgogoro

  Waziri Membe akizungumzia kiini cha mgogoro huo, alisema ni hatua ya Serikali ya Malawi kushikilia msimamo kuwa eneo lote la Ziwa Nyasa lipo Malawi wakati Tanzania inasema mpaka upo katikati ya Ziwa.

  "Wenzetu wanadai ziwa lote lipo Malawi lakini, nyaraka zilizotengenezwa na wakoloni wa Kiingereza mwaka 1928 na 1938 zinaonyesha kuwa mpaka wa ziwa hilo upo katikati," alisema.

  Alisema hoja ya Tanzania ina nguvu kulingana na sheria za kimataifa kwa vile tatizo kama hilo linafanana na mgogoro uliokuwapo baina ya Cameroon na Nigeria. Alisema katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Dunia, iliamuliwa kuwa mpaka baina ya nchi hizo mbili upite katikati ya Ziwa Chad ukifuata msitari ulionyooka.
   
 11. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi inawezekana Malawi walikua moto, au sisi ndio tulipata moto zaidi yao.?
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  hizi ndio habari njema bwana....mambo ya vita wapi na wapi?? meza ya mazungumzo ndio suluhu kubwa na vita ni last option
   
 13. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Bora vita iepukwe!
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  tuzipige tu ili heshima iwepo....si ajabu wanatulia mingo taimingi hapo.....ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria....hawa hawana akili dawa yao ni kuwaonyesha kuwa dharau na kiburi si maungwana.
   
 15. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,063
  Trophy Points: 280
  Duuh naogopa kupinga yako kauli maana ukinigundua mimi ni nani utanitafuta na kunipa kipondo ili heshima iwepo
   
 16. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Naona wenye mada hii bado wamelala tuwasubiri tu, watakuja na Data zao kibao kuonyesha bado waTZ tuna makosa kuidanganya Dunia na Bunge ambalo leo spika alikuwa na ujumbe maalum toka Malawi saa 5 asubuhi
   
 17. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hahaha, nikikukamataa! utantambua....chezea mutz veve
   
 18. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hii ni hatua nzuri kuelekea mwafaka
   
 19. j

  jackline JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  sijui ni kweli au uongo.Maana hata Ebola vyombo vya habari baadhi vilisema haijafika TZ wakati wakazi wa karagwe wanasema vingine..
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa vizuri kama jeshi letu lingeitungua moja ya ndege zilizokuwa zinaruka ktk anga letu zikifanya utafiti.
  Nadhani ujumbe ungefika vizuri zaidi.
   
Loading...