Ndege za kivita?

Jahmercy

Senior Member
Sep 19, 2010
116
78
Ndugu wana jamii kuna jambo limenishtua kdogo ktk sherehe ya kuapishwa rais mteule wa NEC, mh jakaya kikwete, had najiuliza hiv ndege za kivita ni za nini ktk sherehe kama ile?
 
Naona ni formality mimi nashukuru zilipita salama si unajua kuna mwaka ziliwai anguka na nilikuwa uwanjani nimebebwa na mama alinisimulia miaka ya 70 uko
 
Ndugu wana jamii kuna jambo limenishtua kdogo ktk sherehe ya kuapishwa rais mteule wa NEC, mh jakaya kikwete, had najiuliza hiv ndege za kivita ni za nini ktk sherehe kama ile?
Zilipita ndege ngapi na kwa formation gani??
 
Ile ni kufikisha ujumbe kuwa jeshi limemis kutumia siraha zake ambazo nyingine hulipuka ovyo maghalani kwa sababu hazijatumika muda mrefu.
"Any volunteer!??"
 
Zimepita mbili toka mashariki kukatiza nje uwanja kwenda kusini.....na kurudia tena hivyo hivyo....ni salute to the new President
 
Hizi ndege leo ni siku yatatu nimekuwa nikiziona sasa sijajua kama ni salamu kwa wale wanaopanga kuleta fujo au ilikuwa mazoezi kwa ajili ya sherehe ya leo ngoja tuone kama itaendelea kutoke.
 
Zimepita mbili toka mashariki kukatiza nje uwanja kwenda kusini.....na kurudia tena hivyo hivyo....ni salute to the new President

Walikosea sana, hivi watajifunza lini juu ya ile vacuum ya measurements upande ule wa mashariki????
 
Walikosea sana, hivi watajifunza lini juu ya ile vacuum ya measurements upande ule wa mashariki????
mkuu wanaaaijua hiyo vacuum ndio maana wamefanya mazoezi ya kutosha week nzima .....na wameogopa kupita karibu na uwanja....wanajuaa sana maana wachina wanakaa anao full time
 
Ndege zenyewe zinaonekana za kizamani sana, hazikimbii kwa kasi ya ajabu! Nadhani hata jiwe la manati linazishinda speed!
 
Ni heshima za kijeshi kwani JK ni amirijeshi mkuu na rais mteule wa NEC ivo ni lazima zingefanya hivo hata akifa wakati akiwa bado madarakani ni lazima zifanye hivo. Hii ni kwa sheria za kijeshi tuu..Nasema hivi kwa mtazamo, upeo, uelewa na utashi wangu japo naweza kuwa tofauti na wewe
 
Dah zile ndege Nazo? na Obama ana nini? ni bora ziwekwe makumbusho tu haina haja ya kuwa na ndege za kichovu kama zile
 
Dah zile ndege Nazo? na Obama ana nini? ni bora ziwekwe makumbusho tu haina haja ya kuwa na ndege za kichovu kama zile

japokuwa jeshi imara ni lenye vifaa bora, lakini pia jeshi imara ni lenye Askari imara, wakakamavu na waliokuwa tayari kujitoa muhanga
Wamarekani waliingia Somalia na Ndege na vifaa vya kisasa na matokeo yake Wamarekani hawawezi kuwasahau wale Askari wa somaliawaliokuwa na AK47 tu huku wakiwa wamevaa misuli tu
 
WADAU, ukweli wa mambo ni kwamba sijaona relevance na mantiki ya hii thread.

Au ndio kuelimishana?

Mbona wakati wa Mwalimu, Mwinyi na Mkapa zilifanya hivyo pia?
 
Mbona vindege vyenyewe vilikua vimechoka vile??? vile ni vya mapambo sio vya vita!!! nafikiri ndo vile vilivyonunuliwa kwa mlungula, mmhh, walikua wanajaribu kututisha!!!
 
Back
Top Bottom