Ndege za ATCL zaanza kuhujumiwa na wafanyakazi. Waziri atoa onyo

Kwa hiyo unataka kutuambia huyo waziri ni muongo sio, ametunga tuhuma kwa watumisha atcl kwamba wanahujumu shirika kumbe bei zao ziko juu !!, nililisikia hili sikusadiki lakini kwa kuwa wewe umetoa ushahidi na namba hawa atcl wajihoji kama wanweza hii biashara, but tuliambiwa na serikali ya ccm kwamba ndege zake zitakuwa na bei za wanyonge, hii ikoje jamani ?
Mkuu si uende tu kufanya booking kwani tatizo ni nini??
 
Mi nadhani, management nayo ina mambo ya kizamani sana, kwanini wasitengeneze utaratibu wa mteja kukata tiketi mwenyewe online kama ilivyo fastJet!? Hivi wanataka hata hili nalo hadi waambiwe na mhe rais!!!!!? Ukiingia website ya FastJet unajua kabisa kama ndege imejaa au laa, sasa wao kinawashinda nini!? Hicho kinacho fanywa na wafanyakazi au mawakala wa ndege wala sio kitu cha AJABU (though hao wafanyakazi wana stahiri ADHABU kali sana) kwenye ulimwengu wa biashara ya USHINDANI, zinaitwa fitina za biashara, tengenezeni software rafiki kwa wateja wenu.
Halafu, hivi ni kwanini ATCL walifuta root ya Mwanza to KIA!? na au KIA to Mwanza!? Na hili nalo hadi mkubwa wa serikali aseme!? Ukweli mnaboa sana, sijui mpewe nini ili mfanye kazi! Sometimes mhe anaposemaga, "fukuza wote na ajili wengine, na wenyewe waki boa nao fukuza" hua binafsi namwelewaga sana tu!
 
View attachment 967786

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, amekemea tabia ya hujuma inayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Tanzania-ATCL huku akikitaka kitengo cha masoko cha Kampuni hiyo kuhakikisha kinaangalia na kuondoa hujuma hizo.

Hujuma hiyo inatajwa kuwa ni ndege kusafiri bila kujaza abiria kwa manufaa ya ndege za mashirika mengine.

Naibu Waziri huyu alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa ATCL, akisema hujuma hizo zinazofanywa na baadhi ya watoa huduma wa ndege hizo si nzuri na kwamba lengo la Serikali ni kuwekeza kwa Watanzania wote ambao utazaa matunda.

Alisema amekuwa akipokea simu kutoka maeneo mbalimbali kuwa ndege zinaondoka bila kujaa hasa za mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya kutokana na baadhi ya watoa huduma hususan mawakala wa tiketi kuwa na tabia ya kuonwa na uongozi wa mashirika mengine ya ndege, hivyo kuacha kuuza tiketi za ATCL na kudai ndege imejaa na baadae ndege kuondoka na abiria pungufu.

“Baadhi ya mawakala huwa wanaonwa na viongozi wa ndege zingine na kudai ndege zao yaani ATCL zimejaa wakati hazijajaa ili ndege zingine zijae,” alifichua Nditite na kuongeza:

“Sasa najiuliza kwanini hawajali ajira na mshahara wao na kutegemea fedha za muda mchache, na hawana uzalendo na nchi yao, tunahitaji tija na sio hujuma.”

Aidha, alisema ATCL imepewa dhamana ya kuhudumia Watanzania wote na kwamba na ndege mpya zinatoa huduma nzuri, chakula na maji bure wakati ndege zingine hazifanyi hivyo.

Alisema, Serikali imeweka kipaumbele katika uendeshaji wa ATCL ambapo hadi sasa imeshapewa ndege nne ambazo ni Dash 8 Q400 tatu, Boeing 787 Dreamliner moja na hivi karibuni wanategemea kupeleka ndege nyingine mbili aina ya Airbus 220-300 huku wakitegemea kupokea ndege nyingine mpya ya Boeing 787 Dreamliner mwakani.

Hivyo alisema ni mategemeo ya Serikali kuona ATCL inafanya vizuri na kwa viwango vya kimataifa kwa kuwa ni fahari ya Tanzania.

Pia aliutaka uongozi wa ATCL kuimarisha kitengo cha biashara ili hujuma hizo zidhibitiwe mara moja.

Kadhalika, aliwataka viongozi na wafanyakazi kufanya kazi kwa weledi na bidii kubwa hasa katika kipindi hiki chenye changamoto nyingi na ushindani kibiashara kwa kuzingatia kutoa huduma bora, kuitii Serikali, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa umma, kuheshimu sheria zilizopo na kutunza siri za Serikali.

Alisema ikiwa baraza hilo litazingatia kufanya kazi kwa weledi litaweza kwenda sambamba na soko lililopo ili uwekezaji wa Tanzania uliokusudiwa uweze kuzaa matunda.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi, alisema watahakikisha kitengo cha masoko na usalama wa ndani kinakuwa salama katika mifumo mbalimbali na kuendelea kuchukua hatua kwa mujibu wa maelekezo ya Waziri.

Matindi ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo, alisema, mikakati ya shirika hilo ni kufanya biashara kwa kutoa huduma za kuvutia wasafiri.

Source: Ndege za ATCL Zaanza Kuhujumiwa Na Wafanyakazi....Waziri Atoa ONYO | MPEKUZI
Mh. Waziri fanya uchunguzi uwatumbue hao wafanya kazi sio wazalendo kwa Nchi yao, tupo wazalendo wakuisaidia Nchii yetu ipate maendeleo, tupo tayari kuyapigania maendeleo ya nchii yetu usikuu na mchana hao, ambao sio wazalendo fyekelea mbali na kama wamepewa rushwa sukuma ndani, aliyetoa, sukuma ndani aliyepokea na hata sukuma ndani aliyeona.
 
Please,lets be serious,hope everybody in license is in business and that should be well understood!
The deputy minister has to employ some marketing tools to help the Company compete and sail fairly good.
Complaining that there are people doing this and that is like failing yourself because if you already know your setbacks then why dont you take action!

İ personally praise the efforts to revive the airline but should you know that you are coming to business and know what it all means as doing business!

İ can gues that routing is all what is eating your margines,I hope when you add up the fleet and do a proper route mapping then you will start realizing something...!

Merry Xmas

I think the problem comes from way long during staff recruitment process for most of public entities, most are GPA au kamlete/vimemo based recruitment and while disregard TALENT based recruitment, unaanzisha vipi huduma za ndege karne hii huna digital platforms za kukupatia wateja na mapato ya ziada? Wacha waendelee kuajiri wale wenye GPA za 3.5 na zaidi tu wakidhani ndo wanauwezo pekee katika dunia ya leo.
 
Mimi sioni mantiki ya hizo lawama wakati kizuri kinajiuza, siku hizi ticket za ndege watu wanakata online
 
You have a point. Politics, popularity.. two things that are destroying atcl silently.
I said the same in the first leg of the story when they planned to land in Kampala, no one could listen. The routes they opted, many are not economical, yes we love our airline but the politics has taken its place in every angle of this country, poor we!
 
And maybe hatuna watu ambao wana uzoefu wa kuendesha hii biashara. Idea yangu nyongine ni kujarib kuajiri lets say Mo, since yeye ni experienced CEO.. maybe anaweza akatumia nafasi hiyo tuendako. Then akishatufikisha mahali flani tuna break ties.
Mashirika ya umma ni vigumu sana kufanya vyema Tanzania.

Historia ya nchi hii inatuonesha kuwa elimu yetu imetujenga kuwa watumwa na si watuma.

Mpeni Bakhresa au MO au Manji muone litavyotia faida shirika hilo.

Tutakamatana uchawi kila siku lakini ukweli ni mfumo wetu wa elimu, upo kwenye kuharibu si kutengeneza.
 
Waziri unapaswa kuwafukuza kama umeshawabaini hilo onyo halitabadili tabia ya mtu. Kuna vijana wengi tena wazalendo wanatamani hizi ajira.
 
View attachment 967786

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, amekemea tabia ya hujuma inayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Tanzania-ATCL huku akikitaka kitengo cha masoko cha Kampuni hiyo kuhakikisha kinaangalia na kuondoa hujuma hizo.

Hujuma hiyo inatajwa kuwa ni ndege kusafiri bila kujaza abiria kwa manufaa ya ndege za mashirika mengine.

Naibu Waziri huyu alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa ATCL, akisema hujuma hizo zinazofanywa na baadhi ya watoa huduma wa ndege hizo si nzuri na kwamba lengo la Serikali ni kuwekeza kwa Watanzania wote ambao utazaa matunda.

Alisema amekuwa akipokea simu kutoka maeneo mbalimbali kuwa ndege zinaondoka bila kujaa hasa za mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya kutokana na baadhi ya watoa huduma hususan mawakala wa tiketi kuwa na tabia ya kuonwa na uongozi wa mashirika mengine ya ndege, hivyo kuacha kuuza tiketi za ATCL na kudai ndege imejaa na baadae ndege kuondoka na abiria pungufu.

“Baadhi ya mawakala huwa wanaonwa na viongozi wa ndege zingine na kudai ndege zao yaani ATCL zimejaa wakati hazijajaa ili ndege zingine zijae,” alifichua Nditite na kuongeza:

“Sasa najiuliza kwanini hawajali ajira na mshahara wao na kutegemea fedha za muda mchache, na hawana uzalendo na nchi yao, tunahitaji tija na sio hujuma.”

Aidha, alisema ATCL imepewa dhamana ya kuhudumia Watanzania wote na kwamba na ndege mpya zinatoa huduma nzuri, chakula na maji bure wakati ndege zingine hazifanyi hivyo.

Alisema, Serikali imeweka kipaumbele katika uendeshaji wa ATCL ambapo hadi sasa imeshapewa ndege nne ambazo ni Dash 8 Q400 tatu, Boeing 787 Dreamliner moja na hivi karibuni wanategemea kupeleka ndege nyingine mbili aina ya Airbus 220-300 huku wakitegemea kupokea ndege nyingine mpya ya Boeing 787 Dreamliner mwakani.

Hivyo alisema ni mategemeo ya Serikali kuona ATCL inafanya vizuri na kwa viwango vya kimataifa kwa kuwa ni fahari ya Tanzania.

Pia aliutaka uongozi wa ATCL kuimarisha kitengo cha biashara ili hujuma hizo zidhibitiwe mara moja.

Kadhalika, aliwataka viongozi na wafanyakazi kufanya kazi kwa weledi na bidii kubwa hasa katika kipindi hiki chenye changamoto nyingi na ushindani kibiashara kwa kuzingatia kutoa huduma bora, kuitii Serikali, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa umma, kuheshimu sheria zilizopo na kutunza siri za Serikali.

Alisema ikiwa baraza hilo litazingatia kufanya kazi kwa weledi litaweza kwenda sambamba na soko lililopo ili uwekezaji wa Tanzania uliokusudiwa uweze kuzaa matunda.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi, alisema watahakikisha kitengo cha masoko na usalama wa ndani kinakuwa salama katika mifumo mbalimbali na kuendelea kuchukua hatua kwa mujibu wa maelekezo ya Waziri.

Matindi ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo, alisema, mikakati ya shirika hilo ni kufanya biashara kwa kutoa huduma za kuvutia wasafiri.

Source: Ndege za ATCL Zaanza Kuhujumiwa Na Wafanyakazi....Waziri Atoa ONYO | MPEKUZI
Sasa kweli suala kama hili linahitaji mtu aonywe kweli fukuza harafu waziri ukitumbuliwa ww unalalamika kuna vitu vya kuonywa sio ujinga wa mtu anafanya kusudi.
 
Please,lets be serious,hope everybody in license is in business and that should be well understood!
The deputy minister has to employ some marketing tools to help the Company compete and sail fairly good.
Complaining that there are people doing this and that is like failing yourself because if you already know your setbacks then why dont you take action!

İ personally praise the efforts to revive the airline but should you know that you are coming to business and know what it all means as doing business!

İ can gues that routing is all what is eating your margines,I hope when you add up the fleet and do a proper route mapping then you will start realizing something...!

Merry Xmas

Muandike kiswahili sio ukiandika kiingereza utaonekana msomi wengine wazazi wenu walikuwa wanahela mkapelekwa shule nzuri ukajua kiingereza akafilisika ukarudi st kayumba ukaishia 4 mbaya sikunyingine vingereza vingi havisaidii
 
Back
Top Bottom