Ndege za Abiria zakatisha anga la Libya baada ya kifo cha dikteta Gaddafi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndege za Abiria zakatisha anga la Libya baada ya kifo cha dikteta Gaddafi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Jun 3, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kwa miaka kadhaa baada ya Gaddafi kuitungua ndege ya abiria ya Marekani PAN AM ambayo ilipita juu ya anga la Libya, hatimaye ndege hazikuwa huru kuvuka bahari ya kati, zimekuwa zikiambaa kupitia Palestina, Israel na kisha kuingia Ulaya. Sababu ni kumwogopa Gaddafi asijekutungua tena.

  Nimeshuhudia siku hizi ninaposafiri ndege za abiria kukatisha anga la Libya na kuvuka bahari ya kati huku tukiangalia visiwa vya Malta, Sisilia hadi tunakuwa juu ya anga la Italia.

  Gaddafi licha ya kuwafanyia mazuri Walibya, kimataifa alikuwa tishio na kukosa raha ndege zinapopita karibu na mipaka ya nchi yake.
   
 2. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 447
  Trophy Points: 180
  Mkuu nani kakuambia gaddaf ni dikteta? Hv ukipishana na nchi za magharibi tayari unakuwa dicteta?
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Ni ndege gani ya Pan Am unayozungumzia mkuu? Ni ile ''flight 103'' iliyokuwa inatoka Heathrow kwenda John F Kennedy? Mbona haikutunguliwa kwenye anga ya Libya?
   
 4. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi somo la Historia bado linafunishwa Tanzania?
   
 5. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ndege ya PANAM iliyotunguliwa na WALIBYA haikuwa inaruka juu ya anga ya nchi hiyo bali ilitunguliwa ikiwa inaruka juu ya anga ya Scotland!!
   
 6. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Kumbe unaweza kuanzisha thread itakayo fanya watu wajue uelewa wako wa history!
   
 7. next

  next JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 601
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  mkuu, ndege ya panam ilianguka scotland, unataka kuniambia ilitunguliwa libya?
  this is new findings?
   
 8. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Unajionyesha tu ulivyo kilaza mbele za umma wote huu...aibu sana
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mahali ilikotunguliwa ndege sikuwa na hakika nako, ila ni Gadafi aliyefanya hivyo na alikubali na kuwa tayari kulipa fidia kwa Marekani kwa kupeleka mafuta. Matokeo ya kutungua ndege hiyo ndiyo yaliyosababisha ndege zisitishwe kupita katika anga la Libya.

  Baada ya kifo cha Gadafi ndege zinapita katika anga la Libya na kwenda kutokea Itali kuvuka bahari ya Kati. Nimeshuhudia hilo mimi mwenyewe kwa kuvuka hapo mara mbili baada ya kifo cha Gadafi na ni ndege hizo hizo ambazo awali hazikuwa zinapita hapo. Huu ni uthibitisho wazi na dhahiri kwamba Gadafi alikuwa tishio kwa ulimwengu ndege kupita katika anga la nchi yake.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Maudhui yanabaki kwamba ndege hazikuwa zikipita huko na sasa zinapita baada ya Gadafi kufariki, ukweli huu hauondoki umebaki.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nashukuru na samahani kwa kunukuru vibaya ilipoangushwa ndege, lakini tukio hilo ndilo lililosababisha tahadhari ya kuvuka anga la Libya, na hata kama wewe umewahi kusafiri kwenda ulaya toka Afrika anga la Libya lilikuwa likikwepwa na ndege toka East Afrika ziliambaa kando ya bhari ya sham hadi mashariki ya kati kisha zinaelekea Ulaya.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
   
 13. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamaa alikuwa na uchungu sana na nchi yake na bara la africa kwa ujumla,alizisaidia nchi masikini za africa misaada ya maana,alikuwa na wazo la kupigania umoja wa nchi za africa,ni kama ule uliopo ulaya kwa sasa,kitu amabacho kingesaidia kutukomboa katika vita na umaskini kwa kiasi kikubwa kwa kukuza maingiliano ya kisiasa kibiashara na baina ya nchi zote za africa.....lakini siku zote mmarekani na nchi za magharibi wana yao waliyoyapanga kwa bara la africa!!!africa ikitajirika na kujikwamua kiujinga mzungu akale wapi???!!!tutaendelea tu kuwa wajinga ili waheshimiwa waishi kwa rasili male zetu
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wapigania haki Waafrika ni wengi, hakuna aliye mbaya tu. Hata Idd Amini alikuwa na mazuri aliyofanya kwa Waganda. Pale New York karibu na United Nation kitovu cha jiji Manhattan, kuna jumba la ubalozi wa Uganda liitwalo Uganda House. Ni Idd Amin alilinunua. Niliweza kulifahamu jumba hili nilipoulizia UN ofisi za ubalozi wa Tanzania. Nikaelekezwa niende pale Uganda House ambalo liko karibu na UN. Idd Amini aliona hitaji hilo tangu miaka hiyo ingawa mazuri yote yamefunikwa na udikteta wake.
   
 15. m

  mgadafi Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sawa nia yako ilikuwa ni kutufahamisha kama umepanda ndege hongera
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu unaishi ulimwengu gani, ndege ni kitu cha kawaida siku hizi. Hata wanaoishi Tanzania tu wanaona kitu cha kawaida sembuse kwa mtu mwenye masafa ya kimataifa mara kwa mara? Kwa taarifa tu tangu nianza masafa ya kimataifa kabla ya karne hii yaani 199---- ndege hazikugusa anga la Libya. Hata British Airline ambayo miaka ya 1995 nilipoingia Getwick London kwa mara ya kwanza na kupanda Speed link bus kuunganisha Heathrow airport kwa ajili ya transfer kwenda bara jingine baada ya Dar na Nairobi ndege iliongoza kando ya bahari ya Sham hadi Middle East na kisha kuingia Ulaya.

  Ndege zilikua huru kupita anga la nchi nyingine za kiarabu lakini si anga la Libya.
   
 17. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Bado hujani-convince na maelezo yako. Sio kweli kwamba ndege zilikuwa zinakwepa anga ya Libya. Kuna ndege nyingi sana zilikuwa ZINATUA Libya wacha kuruka kwenye anga lake. Kama uliwahi kusafiri na ndege na haikupitia anga ya Libya itakuwa ni sababu nyingine tu lakini sio kweli kwamba walikuwa wanaogopa kutunguliwa.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Vigumu kukuambia kwamba nimekunywa maji na sina kiu na wakati we umekazana kwamba bado na kiu sijanywa maji.
   
 19. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndege miaka yote zimekuwa zikipita hapo anga ya Libya, na baadae zinaingia anga ya Sudan.
   
 20. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,224
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280

  Mkuu,
  Uwanja unaitwa Gatwick (kama unaongelea ule uliopo jijini London), sio kama ulivyoandika hapo juu kwenye RED. Unless kama una refer uwanja mwingine
   
Loading...