Mtapata taabu sana awamu hii...!!!Nina uhakika 100% ununuzi wa hii ndege ni upuuzi mtupu. Ni hasara juu ya hasara. Mkuu amekurupuka mnoo. Hakuna tofauti yoyote na mradi wa kile kivuko cha Dar ambacho kilinunuliwa ili kupunguza msongamano na kikazinduliwa na Magu mwenyewe, lakini mwisho wa siku kikayeyuka.
Hata hili la ndege ipo siku wanaobisha hapa watakuja kuelewa na hata mkuu mwenyewe atakuja kulikana hilo dege.
Tujipe muda na tuwe na subiri tu. Ukweli huwa haujifichi, unaweza kucheleweshwa lakini ipo siku utakuwa wazi tu.