Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Shirika la ndege la Malaysia, Rayani Air, linalozingatia misingi ya dini ya kiislaam katika biashara zake, limepigwa marufuku na idara ya safari za nchini humo baada ya ukaguzi kuuonyesha halijakidhi viwango na vigezo vya kiusalama.
Rayani Air ilianzishwa December ikinadi kuendeleza desturi za kiislaam katika huduma zao zote zikiwemo za Chakula cha wateja, kutouza pombe na wafanyakazi wanaovalia nguo ndefu na hijab kwa wanawake.
Shirika hilo linamiliki ndege mbili aina ya Boeing na lina wafanyakazi wapatao 60 wakiwemo marubani 8 na ina ofisi katika kisiwa cha Langkawi na pia husafiri sana Kuala Lumpur na mji wa kota Bahru.
BBC NEWS..