Ndege yaanguka sumbawanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndege yaanguka sumbawanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kidagaa, Aug 31, 2010.

 1. K

  Kidagaa Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu naomba niwahabarishe kwamba ndege ndogo iliyokuwa imebeba watu wanne imeanguka mara baada ya kupaa kutoka katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga, leo mnamo saa kumi kasoro jioni. Kizuri ni kwamba wote waliokuwemo wamepona. Chanzo cha ajari hakijawekwa wazi. Ndege hiyo yasemekana ilikuja kumchukua mgonjwa mmoja kumpeleka hospitali ya rufaa. Cha kushangaza ni kwamba hawa jamaa wa zimamoto (firefighters) wamefika baada ya nusu saa. Pongezi ziwaendee jamaa wa ambulance ambao wamefika baada ya muda mchache kama dakika 7. Hali ya uwanja mbaya kama nini labda ndo maana mgombea kigoda ameahidi kama kawaida yake kuujenga. Tusubiri tuone.
   
 2. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hawa jamaa mara nyingine tunawalaumu bure tu, hivi wataota kama kuna tukio bila kujulishwa?wamefika baada ya nusu saa walijulishwa baada ya muda gani, inaweza kuiwa response yao ni nzuri, labda dakika moja toka walipotaarifiwa. haijalishi hata kama wangefika baada ya wiki moja so long as ndiyo muda waliopata taarifa. ushauri wa bure kunapokuwa na tukio linalowahitaji wazimamoto tuwe wepesi kutoa taarfifa badala ya kusubiri watafika baada ya muda gani withou notifying them...
   
 3. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh zimamoto huyu!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwanza wamejitahidi kufika mapema!! Ile ajali ya moto jengo la mkuu wa mkoa Dodoma gari ziko karibu lakini zilichukua muda kibao kuonekana tena moja tu kati ya matatu likiwa na maji kiduchu kabisa. Cha kumshukuru Mungu hao abiria wamepona. Kwa ajali ya ndege most of the time ni miracle ukiokoka kufa!!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Sumbawanga bwana... Huenda hiyo ndege imeangushwa na m chawi aliye mroga huyo mgonjwa.
   
 6. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,918
  Likes Received: 1,027
  Trophy Points: 280
  Poleni sana wahanga.
  Pia twashauri uwanja uwekwe katika hali nzuri.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ndugu Kidagaa!

  Taarifa yako ni njema sana, lakini inakosa vipengele vya muhimu sana ili kuikamilisha!
  -Je ndege hiy ni mali ya nani?...ya serikali...ya kibinafsi... ya mashirika ya Hifadhi za Taifa au Msalaba mwekundu?
  -Je namba za usajili(registration No and Marks) ni zipi?
  -Ilikuwa ikielekea wapi?
  Nadhani ukitufahamisha hayo utakuwa umeboresha sana habari hii, unless kama nia yako ilikuwni kuwang'ong'a zimamoto!

   
Loading...