Ndege ya tatu aina ya Bombardier Kuwasili nchini Mwezi huu

Wewe kama ulisha laaniwa ulilaaniwa tu kamwe laana hiyo haita kutoka mtu mmoja amesimama kwaajili ya Watanzania na Taifa kwa ujumla bado mnashindwa kumsapoti hakika nimeamini Nabii hapati heshima kwao Nchi ilikuwa haina ndege hata moja huyu amethubutu bado tunamdhihaki hakika wenzetu mataifa mengine wanamtamani sisi tunaleta dhihaka hakika MUNGU Atusaidie Sana tumejisahau tunashabikia kuliko ukweli.
wanaomtamani waje wamchukue tu,tutawaongeza na makinikia.
 
Biashara ya ndege hailipi kwa sasa(labda baadae) ,kwanza angejikita kwanza kwenye kilimo cha umwagiliaji(Ujenzi wa mabwawa), pili ubia wa Ujenzi wa smelter (Makinikia yanalipa kuliko abiria wa ndege kwa sasa) tatu, Ujenzi wa conference centres kubwa za kisasa na wawekezaji kwny mahoteli (ili kupata mikutano ya kimataifa) then nne, ndiyo angenunua hizo ndege. Yote heri kwa sasa hongera kwa Mheshimiwa Rais, anaweza sana tu.
Hawatembei kwenye sera, bali mihemko toka ndotoni
 
nafikiri hadi 2020 watu tutaenda kwenye kampeni huku tukizolewa na ndege sio mabasi kama 2015 ili kujaza umati
 

Sawa, tumesikia kwamba ni kweli ndege moja kati ya Bombadier mbili tulizo nãzo ni mbovu.Tunachotaka ni kwamba wote waliohusika katika wizi huu wawajibishwe. Haitakuwa busará kuwashikia bango akina Barrick huku mchwa wa ndani tunawaonea haya.Call a spade a spade.
 
Hadi sasa hatujapewa update zile mbili zimeingiza faida sh ngapi na kiasi cha kodi kilicholipwa serikalini.
 
Akitoka na yeye atashangaa mawaziri wake tunawapandisha kisutu! Ananunua ndege zilipe madeni......hafuati utaratibu wa manunuzi wala hapitishi bungeni..hazina ameweka mpwa wake!!! Only in Tanzania
 
Unajua bei ya ndege yaani tatu ziwe 50 billion si kila mtu angekua nazo!

sikukuelewa mkuu, kumbe ni ndege zote 3 kwapamoja sawa mkuu kama ni hivyo. Mie nilifikiri bobandia moja ndo bei yake hiyo. Kama ndivyo, nafuta kauli ya awali.
 
Back
Top Bottom