Ndege ya tatu aina ya Bombardier Kuwasili nchini Mwezi huu

Wewe kama ulisha laaniwa ulilaaniwa tu kamwe laana hiyo haita kutoka mtu mmoja amesimama kwaajili ya Watanzania na Taifa kwa ujumla bado mnashindwa kumsapoti hakika nimeamini Nabii hapati heshima kwao Nchi ilikuwa haina ndege hata moja huyu amethubutu bado tunamdhihaki hakika wenzetu mataifa mengine wanamtamani sisi tunaleta dhihaka hakika MUNGU Atusaidie Sana tumejisahau tunashabikia kuliko ukweli.

Umsapoti kwa kununua ndege? Kuna wanafunzi wamekosa mkopo baada ya serikali kutoa pesa kidogo. Unategemea hiyo ndege itamsaidia nini?
Kuna watu wanakosa madawa hospitali,unategemea hiyo ndege itamsaidia nini?
70% ya shule za sekondari za serikali hazina maabara,unategemea hizo ndege zitamsaidia vipi uyo mwanafunzi?
Kuna wilaya hazina maji wala barabara,unategemea hizo ndege zitawasaidia vipi?
Shule hazina vitabu,badala ya kuwekeza kwenye elimu anaenda kuwekeza kwenye mradi usiokua na tija kwa taifa. Bora treni wananchi wataweza kupanda hila sio hizo ndege.
 
Dah Kuna Haja Ya Spika Wa Bunge Kujiuzulu,nabunge Kuvunjwa Kabisa Hakuna Haja Yakuwa Na Bunge Wanaokula Fedha Zetu Dodoma Nawakati Kuna Mtu Anafanya Purchusing Nakutunga Sheria Mwenyewe?
 
Bombadier nyingine ya 3 kuwasili nchini mwezi huu, Serikali imeshatenga Sh. Bilioni 500 kwa ajili ya malipo ya awali ya ndege nyingine 3. [HASHTAG]#Tuliahidi[/HASHTAG] [HASHTAG]#Tunatekeleza[/HASHTAG]
View attachment 526212
Asante kwa taarifa.Ila kwa nia njema kabisa naomba taarifa kuhusu ile ambayo ilikuwa parked,tayari inakata mawimbi? Maana haitakuwa busara kuongeza zingine wakati hii bado haijatengemaa. Who knows, labda ndege zenyewe, yaani make ina an inherent shortcoming.
 
Biashara ya ndege hailipi kwa sasa(labda baadae) ,kwanza angejikita kwanza kwenye kilimo cha umwagiliaji(Ujenzi wa mabwawa), pili ubia wa Ujenzi wa smelter (Makinikia yanalipa kuliko abiria wa ndege kwa sasa) tatu, Ujenzi wa conference centres kubwa za kisasa na wawekezaji kwny mahoteli (ili kupata mikutano ya kimataifa) then nne, ndiyo angenunua hizo ndege. Yote heri kwa sasa hongera kwa Mheshimiwa Rais, anaweza sana tu.
 
Watanzania tuna hitaji Somo linaitwa critical thinking. Ni rahisi sana kusombwa na matukio. Imagine upinzani ulivyokua na kelele Leo kimya na mtu keshasombwa hafikirii twice. Leasing was the best option. We would have more than 10 fleet
 
Hii itakua ya pili maana moja tumeshaambiwa imeharibika tayari.
Dah nasikia moja haiwezi ruka, inaletwa nyingine tena!??
Asante kwa taarifa.Ila kwa nia njema kabisa naomba taarifa kuhusu ile ambayo ilikuwa parked,tayari inakata mawimbi? Maana haitakuwa busara kuongeza zingine wakati hii bado haijatengemaa. Who knows, labda ndege zenyewe, yaani make ina an inherent shortcoming.
 
Back
Top Bottom