ndege ya saba sasa hii inaanguka!!!!!!!

Kaka Mkubwa

Senior Member
Oct 10, 2008
154
10
BREAKING NEWS - Ndege Yaanguka Iran na Kuua 150


Wednesday, July 15, 2009 12:40 PM
Ndege ya shirika la ndege la Iran, Caspian Airlines imedondoka ikiwa safarini kuelekea nchini Armenia na kuua watu wote 150 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Caspian Arlines la Iran imeanguka kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kuua watu wote 150 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

Taarifa zilizotolewa na televisheni ya taifa ya Iran ilisema kuwa ndege hiyo imeanguka kwenye mji wa Qazvin wakati ikiwa safarini kuelekea mji mkuu wa Armenia, Yereven.

Taarifa zilizotolewa na shirika la habari la Iran la IRNA zimesema kuwa ndege hiyo iligawanyika vipande vipande na mabaki yake kuwaka moto.

Watu wote waliomo kwenye ndege hiyo wamefariki dunia.

Habari zaidi tutawaletea baadae.
 
Rostam Aziz. Mwasikia harufu yake? CASPIAN? Inaweza kuwa HARUFU TU.
 
Back
Top Bottom