UZUSHI Ndege ya Malaysia iliyopotea miaka 9 iliyopita yaonekana ndani ya maji ikiwa haina abiria

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Salaam Wandugu,

Nimepata taarifa mtandaoni kuwa ndege ya Malaysia iliyopotea miaka tisa iliyopita imekutwa kwenye maji ikiwa haina abiria.

Habari hiyo ilichapishwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Twitter linaonesha picha ya mbele ya ndege yenye kutu inayosomeka: “Ndege ya Malaysia MH370 iliyotoweka miaka 9 iliyopita imepatikana chini ikiwa haina abiria. Ndege hiyo ilikuwa na abiria 239.”

Je, kuna ukweli wowote?

1683053466720.png

Picha inayoenea kwenye mitandao
1683096584698.png

Picha ya ndege ya Lockheed Martin L1011 Tristar kwa upande wa pembeni
Source: Deepbluedivecenter



Video credit: Deepbluedivecenter
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na madai kwenye baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii kwamba Picha ya ndege iliyo chini ya maji (hapo juu) ni mabaki ya ndege ya abiria Malaysia Airlines Flight 370 iliyopotea mwaka 2014.

JamiiForums imepitia ripoti mbalimbali ili kujua uhalisia wa madai hayo kama ifuatavyo:

Kwa mujibu wa utafiti wa AP wanaeleza kwamba madai ya kuwa picha hiyo ni ndege ya Malaysia si ya kweli. Wanaeleza kuwa picha hiyo (hapo juu) ni ndege ya zamani iliyoitwa Lockheed Martin L1011 Tristar katika Bahari Nyekundu (Red Sea).

AP wanabainisha kuwa picha hiyo inayosambaa inatoka kwa video iliyowekwa mtandaoni na Deep Blue Dive Center (Tazama hapo juu), ambayo ni kampuni ya kupiga mbizi ya huko mjini Aqaba, Jordan. Kwahivyo, Ndege ya shirika la ndege la Malaysia Boeing 777 iliyotopotea mwaka 2014 bado haijapatikana.

Kampuni ya Deep Blue Dive iliyotoa video na picha hiyo inabainisha kuwa hiyo ni Ndege ya Tristar ambayo imeanguka katika Bahari Nyekundu, Aqaba JO. Wanaeleza kuwa ndege hiyo ilizamishwa makusudi na inatumika kwa utalii wa Wazamia majini na kama mwamba bandia katika eneo hilo.

Je, vipande au mabaki ya vipande vya ndege ya Malaysia vimewahi kuonekana?
Mnamo tarehe 20 Machi, 2014 ikiwa ni siku 12 baada ya kutoka taarifa ya kupotea kwa Ndege ya abiria ya Malaysia zilitoka taarifa kutoka nchini Australia zikieleza kuonekana kwa vipande viwili vya ndege ambavyo vilikisiwa kuwa ni vya ndege hiyo iliyopotea.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia mwaka huo 2012, Tony Abbott alitangaza kuwa picha za Satelite za wataalam wa nchi yake zilionesha vipande viwili vya vitu vinavyokisiwa kuwa vya ndege ya Malaysia iliyotoweka na zaidi ya abiria 230.

Tangazo hili lilitoka siku chache baada ya meli za kivita za Australia kuanza kuitafuta ndege hiyo Kusini mwa bahari ya Hindi.

Hivyo kutokana na vyanzo hivyo ambavyo JamiiForums imevipitia, uvumi unaoenea kuhusu kuonekana kwa mabaki ya ndege ya Malaysia ni uzushi.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom