Ndege ya Lowassa inayopaa, na abiria walioachwa wameduwaa!

Haya mambo yapo sana maeneo ya Tanzania vijijini. Nakumbuka nilishakutana na kundi la mgambo wenye jazba mnamo mwezi wa sita mwaka 1994, ilikuwa ni patashika nguo kuchakaa, sio kuchanika! Nashukuru nilikuwa na kitambulisho cha uanafunzi (nilikuwa mwanafunzi wa sekondari enzi hizo), nikapigwa mkwara na kuachiwa, ila ningekuwa raia wa kawaida basi ningekumbana na ghadhabu za mgambo wa wilaya, wakihimiza michango ya shule za kata.
Haya mambo yapo.
Something needs to be done!
 
Nina wasiwasi kama hizo picha ni za TANZANIA.Picha hizo zimesambaa sana kwenye e-mail za watu mbalimbali.Mara ya kwanza kulikuwa na kichwa cha habari kinachosema "Nyumba ya BOT Chief Balali,Brussels" na e-mail zilizofuatia baada ya wiki hivi ndio zimeandika kuwa ni "Nyumba ya Manji - Upanga".E-mail hizo zimesambazwa kutoka kwa Waungwana wa Standard Chartered Bank - DSM na pia watu wa Heritage Insurance Company - Dsm wamezisambaza sana picha hizo!Sasa mwenye Ukweli na picha hizo atueleze,lakini nina wasiwasi kuwa hapo si Dar!

Exactly, nakumbuka mimi kuzipata kwenye email kama miezi 6 hivi imepita mkuu, and on my own analysis, kwa kuangalia moja ya picha inayoonyesha mazingira ya nje, nina wasi wasi na hiyo vegetation kama inaweza kuwa mazingira ya dar tena upanga...ninahisi itakuwa nje ya nchi, labd auarabuni au somewhere asia kama alivosema Mwanakijiji
 
No Ngosha No! Yaani, unataka watu wadhanie mimi nimebadilika juu ya Lowassa... akapanda ndege nyingine akaipundua safari kabisa.. halafu walitaka watu tuendelee kukaa kwenye ndege isiyojulikana inakwenda wapi alimradi tuseme tumetoka Airport!

Hakika unahitaji nishani ya consistency.

Kwenye hilo hujabadilika hata chembe na maandishi yako hayaongopi.

Hayo uliyaandika zaidi ya miaka 9 iliyopita!!
 
BAK Asante sana kwa hili bandiko la mwanakijiji.. Hakika mwanakijiji ni kichwa haswa yupo miaka mingi mbele... Mliotusaliti adhabu yenu mmeshaanza kuipata. Chadema ya sasa ni chama cha mafisadi.
 
Hakika unahitaji nishani ya consistency.

Kwenye hilo hujabadilika hata chembe na maandishi yako hayaongopi.

Hayo uliyaandika zaidi ya miaka 9 iliyopita!!

Consistency! Sawasawa kabisa. Inaonekana Mwanakijiji ana chuki ya ndani kabisa juu ya Lowassa. Ni personal grudges.
 
mwawado.. hiyo katuni ilienda sambamba na ile article kwani sidhani kama article peke yake ingewafanya wakurupuke kujibu. Nasikia siku ile ya Jumatano kwenye viwanja vya Bunge wabunge walionekana wakichekea pembeni na Kiongozi wetu shujaa, hodari na mahili aliyetamba Bungeni alipoona hiyo nakala mori ulianza kumpanda.... ndipo akaamuru mvua inyeshe!
Sijui Ndege yetu ingekuwa inapasua anga zipi leo hii kama safari ya matumaini isingeishia Dodoma!
 
Back
Top Bottom