Ndege ya Lowassa inayopaa, na abiria walioachwa wameduwaa!

jamboonormal_kasungura.jpg

Unaweza kujisomea makala iliyotangulia kikatuni hicho HAPA

teh teh teh teh teh.....

Mkjj..... No wonder bi senti 50 alikuambia kuwa hii makala ya kasungura imeleta sokomoko huko juu.

Poor Lowassa, mara kichina kifundishwe mashuleni, mara ndege inapaa, mara visungura, huyu baba anakazi kweli....

teh teh.......
 
Naona hii itakuwa ya mwisho kwa mwezi huu.. nitawaachia wengine sasa. Maana ukionywa mara nyingi lazima usikilize.. huwezi kujua wengine wanakutakia mema.
 
Mzee Mkjj,

Hii katuni itakuwa imempandisha mori huyu muheshimiwa. Huyu ngo'mbe alipitishwa mlango wa nyuma nini mbona hatukumuona?
 
Naona hii itakuwa ya mwisho kwa mwezi huu.. nitawaachia wengine sasa. Maana ukionywa mara nyingi lazima usikilize.. huwezi kujua wengine wanakutakia mema.

Poor Mwanakijiji,

Ninaamini MUNGU atakulinda kwa sababu unawasemea wale wanaoonewa huko nyumbani. Unawasemea wale wanaopikiwa pilau wakati wenzao wanapewa vipande vya dhahabu.

Maombi ya wananchi wa Buzwagi kwa MUNGU yatakulinda na mafisadi Rostam Azizi na wanamtandao wenzake.
 
MKJJ Embu Muonee Huruma huyu Mzee ataanguka kwa pressure,Si umesikia Vumbi lililotimka Abuja (Nigeria)?.Waziri kaanguka Bungeni baada ya kuandamwa na Shinikizo la kutetea wala Rushwa,kabla hajafikishwa Hospitali, jina lilishabadilika na kuanzia na Marehemu!!Sasa naona na kwa EL hali si nzuri sana,na haswa baada ya Waasisi wa CCM kuwakalia kooni,nafikiri wanajuta kuwepo kwenye Madaraka....(Joke), katuni nzuri message delivered!!!!

Mwawado...

Mimi naona Lowasa anastahili kupata anachopata sasa hivi. Wanamtandao walitumia kila aina ya mbinu chafu dhdi ya wapinzani wao kina Dr Salim ndani ya ccm kwa uroho tu na ulafi wa madaraka.

This is the time for them to be responsible and lead the country na sio kuleta misemo na usanii wa ajabu kuwa hawajui kwanini nchi ni masikini au kuwa wamepata kasungura kwa kuwapatia wananchi.

Lowasa anadeserve everything ya hii katuni nasioni sababu ya kumhurumia mtu fisadi na mwizi kama lowassa.
 
MKJJ Embu Muonee Huruma huyu Mzee ataanguka kwa pressure,Si umesikia Vumbi lililotimka Abuja (Nigeria)?.Waziri kaanguka Bungeni baada ya kuandamwa na Shinikizo la kutetea wala Rushwa,kabla hajafikishwa Hospitali, jina lilishabadilika na kuanzia na Marehemu!!Sasa naona na kwa EL hali si nzuri sana,na haswa baada ya Waasisi wa CCM kuwakalia kooni,nafikiri wanajuta kuwepo kwenye Madaraka....(Joke), katuni nzuri message delivered!!!!
Kama zile katuni za Sanifu zilizompa pressure mzee Nyanda(RIP)...Ila kama EL hajui ndio faida za utandawazi na demokrasia wacha apewe 'shavu' kwa makala na katu.
 
Lowassa hatumtaki,kala ng'ombe halafu anatuletea kasungura, sisi wengine ni wasabatho,sungura hatuli,sio kitoweo kizuri
kwa afya.Sisi tunamtaka ng'ombe tu.
 
Mzee Mwanakijiji,

Wee mhuni sana!... Duh, nimechokaa maanake haka Kasungura kalikogawanywa kamekuja na mengi.
Tatizo la Lowassa sii mswahili, lugha na mifano haiwezi kabisa. Pili, Usemaji ni kipaji sio darasa la mtu, huyu El hana kipaji hicho kabisa pia hana maneno ya mvuto na hajui anachozungumza kinaweza tafsrika vipi. Kiboko walikuwa Mwalimu na Al hajj maanake hawa watu walikuwa wakijiandaa kikamilifu wanatembelea wananchi hata kama walikuwa na makosa (wrong) lakini kisiasa walijua kupandikiza maneno kwa usahihi.
Hata hivyo Mzee mwanakijiji, huyo N'gombe mjomba wameisha mla wote, hivi sasa wanafuta midomo na kufyonza nyama zilizokwama ktk fizi za meno. Kama kawaida yao watakuuliza ushahidi unao?.. Hiyo mifupa mnayoiona inawezekana kuwa ya Faru aliyeliwa na Simba sio wao..
Kifupi, hili swala la Kasungura na n'gombe ni mtihani mkubwa ktk uchumi wa Tanzania na hakika naweza kuutumia ktk utunzi wa essay moja kubwa ya kuwajibika.
Viongozi wetu wamechukulia makuzi ya uchumi wa Tanzania kama vile faru aliyeko Serengeti. NI jukumu letu sisi wananchi kwenda mwituni na kumwinda huyo Faru kwa hiyo tusije lia njaa hata siku moja ikiwa nchi imebarikiwa kuwa na wanyama pori wengi.
Hii ndio kauli ya viongozi wetu nimekuwa nikiisikia toka wakati wa Mkapa hadi leo JK anaposhangaa kuona wananchi bado wanlalamika na Umaskini wakidai wapewe zana za kuwindia. Ndio maana anauliza hata pinde na mishale mnashindwa kutengeneza wenyewe?.(Ukulima wa majembe ya mkono).
Upande wa wananchi wanachokiona ni mazizi binafsi ya n'gombe yanayozidi kujengwa na viongozi wao. Kumezuka tabaka kati ya walalahoi kutakiwa kula nyama za faru na nyumbu ambazo zinahitaji nguvu kubwa sana na tabaka jingine la viongozi wanaofaidika kula nyama za n'gombe bila kupitia mbinde za mlalahoi. Na wakiulizwa hudai kuwa n'gombe hao ni wa maziwa tu.
Huu ndio mgogoro mkubwa tuliokuwa nao na kamwe hatuwezi kuuweka sawa ikiwa hatutaweza kuzungumza lugha moja!..
Viongozi wetu wanatazama maendeleo ya Tanzania kama ni jitihada za mwananchi kwenda kuwinda porini. Yaani wajishughulishe zaidi ktk kilimo, biashara na kadhalika hata kama hawana zana za kuwindia. Na wanachotakiwa kuifahamu ni kwamba hao n'gombe wanaowaona ni msingi wa kuzalisha maziwa. (miundombinu, vitega uchumi n.k). Maziwa hayapatikani bila kuwa na n'gombe jike aliyedungwa misindano na wataalam wa kizungu ili kutoa maziwa zaidi.
Kwa hiyo wakati wananchi wanadai kutaka kujua hesabu ya ng'ombe hawa wanaodaiwa kuwa wa maziwa, viongozi wetu wanajibu hesabu ya nini kwani kinachotakiwa hapa sii maziwa?.. Hii ni ktk kuficha ufisadi wa kula n'gombe hawa wa maziwa. Kisha basi huongezea maneno kama:- Mkitaka kula nyama, faru na Nyumbu wamejaa serengeti kazi kwenu!.. wanachokula wao sii kazi yenu kwani ni kuingilia maisha yao binafsi!.. watawapeleka mahakamani.
 
Mwkjj, kama unampuzisha EL, tafathari aliye na data za Pesatatu, No, i mean Pesambili B, M. Si mnakumbuka alikuwa ni W/F wakati wma awamu za fisadi mkaa na -jeuri. Yawezekana nae yumo kwenye kiwira, nk
 
Mwkjj, kama unampuzisha EL, tafathari aliye na data za Pesatatu, No, i mean Pesambili B, M. Si mnakumbuka alikuwa ni W/F wakati wma awamu za fisadi mkaa na -jeuri. Yawezekana nae yumo kwenye kiwira, nk

hapa hapumzishwa mtu,wewe ulishaona wapi mcheza ngoma anapumzishwa?tunaendelea kumkoma giladi mchana kweupe..

haya ni mapambano ya kifikra na hakika tutashinda..

rpg kama unazo data za mramba wewe lete,na kuanzia Bunge lijalo tutakuwa tunafuatilia kila movement ya mbunge yeyote,hawawezi wakawa wanakula good time wakati hawachangi hoja yeyote...maeneo ya chako ni chako na club villa pale uzunguni ambao huwa kuna madudu tu,wanajua kuchangia mambo ya maendeleo ya vimada wao huku wakiacha maendeleo yetu yakidorola

simmpendi makamba sababu anakula kodi yangu bila kazi,
simpendi Rostam sababu anadhamini uzandiki na haki yangu,
Simpendi EL sababu Mwalimu hakumtaka,
simpendi msabaha sababu anahusika na Richmond,
simpendi masha sababu alitumiwa na EL katika RDC,
simpendi karamagi sababu ananifanya mimi zuzu,

Muungwana bado unaota?watoe hawa tafadhali
 
EL anataka kuiga wasanii wa maneno kina mwinyi wakti yeye kiswahili hakijui sawa sawa.

yeye angebakia na data tu, mambo ya kutolea watu mifano naona angewaachia wenye uwezo mvuri wa kufikiri zaidi yake.

akichemsha na jengine asiwache, ahurumiwe kwani yeye huwa wananchi wake anatuhurumia ??
 
shame on you MwanakJJ! how dare you? uhuru wa mawazo siyo kufanya ulivyofanya yaani umechukua mstari mmoja na kuigeuza ili kumdhalilisha Waziri wetu Mkuu. Sijui inakupa furaha gani wewe huyo mzee kila akiamka anataka kujua magazeti yameandika nini kuhusu yeye. Umeshamsema inatosha anza wengine!

asante.
 
shame on you MwanakJJ! how dare you? uhuru wa mawazo siyo kufanya ulivyofanya yaani umechukua mstari mmoja na kuigeuza ili kumdhalilisha Waziri wetu Mkuu. Sijui inakupa furaha gani wewe huyo mzee kila akiamka anataka kujua magazeti yameandika nini kuhusu yeye. Umeshamsema inatosha anza wengine!

asante.
Bi Senti 50,
Si na yeye Lowassa ameshaongoza vya kutosha, inatosha na awaachie wengine?
 
Waziri Mkuu anafanya kazi kwa ridhaa ya Rais na hadi hivi sasa hakuna utata kuwa Rais anaridhika na utendaji wake wa kazi. Kama Bunge linaona Waziri Mkuu hafai linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani naye. So, huyo ndiyo Waziri wetu Mkuu na anastahili heshima zote kama Waziri mkuu.

asante.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom