Ndege ya Fastjet yaharibika,yashindwa kuruka kwenda Mbeya,bi harusi aangua kilio kuchelewa send-off

Nchi za wenzetu hapo ushakuwa tajiri... mtalazwa hotel yenye hadhi mpaka ndege ipone huku mkipewa full treatment na bado watawapa mkwanja wa usumbufu!!!

Kibongo bongo mtaishia kupewa pole na ahadi za kurudishiwa mkwanja wenu kwenye tigo pesa baada ya wiki kadhaa
 
Huyo bibi harusi achukue superfeo tu atafika na kuunganisha ukumbini kuliko kukosa kabisa au apande magari ya magazeti.
Si karudishiwa nauli! Akodi private car impeleke au nauli ni ile ya elf 32, kama ni laki 2 basi inatosha privaTe
 
Ndeeege-ndege, Ndeeege-ndege, Ndege BONGO?
Poleni Ila,
Hii ni kero inayochekesha humohumo.
 
wanamuonea bure chenge. Yeye alikuwa anatekeleza ilani ya ccm ya kuliibia taifa...
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders
Wee una laana siyo bure
 
Wameshindwaje hata kuwakodia ndege nyingine? mambo ya ajabu kabisa.
Fastjet ni kampuni inayoendesha biashara kwa vigezo na masharti kuzingatiwa na wana haki ya kubadilisha safari endapo kutatokea tatizo bila kuingia gharama yoyote kwa abiria kikubwa ni kutoa taarifa ndani ya masaa 24 kabla ya safari. Kwa maana nyingine Fastjet ni Budget airlines na hapo ndio watu wanaoifagilia fastjet watajifunza kwa vitendo hasa wanaolalamika ATCL bei ipo juu (wamezingitia matukio kama haya ya kukodi ndege na kulaza watu hotel)
 
Pumba.fu sana weye Mleta uzi.

Hujui kuwa hapo umeepushwa na kifo!?

Pia, ndege kuwa na technical faults / technical failures ni jambo la kawaida sana.

Tena, ndege za kampuni moja Kwa safari moja kuvunjika haina maana kuwa safari zote zinavunjwa au kuchukua ndege ile ya Mwanza ukupelekeni mbeya.
Ndege siyo kama taxi ratiba zake ni fixed.

Zaidi hali hii huwa katika kampuni ile iko na ndege chache ndipo utaona changamoto hiyo.

Ila hata zile Ethad, Qatar, Turkeyshirlines,KLM wote wanashida hiyo Ila wao, wana ndege nyingi Kama unataka kuhakikisha hilo jaribu kuangalia namba za ndege kwenye tiketi na ndege utakayopanda kuna muda zinakuwa ni tofauti.

Same applies to ATCL, due to few planes and technical faults makes its operations to face some challenges to meet the market demand.

Ila utaelewa tu.

Pole Kwa safari yako na Biashara zako kutoenda vizuri.
 
Na yeye kama alijua anasherehe kwanini hakuodoka mapema hata siku 4 kabla? mbona anakuwa na akili kama za CCM.
Mimi pia namshangaa..bibi harusi unatakiwa uwe chini ya himaya ya wazazi wako si chini ya week moja kabla ya harusi..kwaajili ya usalama, kupumzika ...sasa huyu ataingia ukumbini na stress za kutosha
 
Kwanini mkuu?
Watu wana allergy na ATCL tangu miaka ile inasuasua mpaka leo....search nyuzi za ATCL uone jinsi inavyopigwa madongo ikipata matatizo ya kiufundi....wakati mwingine iliwahi kutokea Precision air ilitua kwa tumbo tairi la mbele liligoma / kuteleza lakini haikuwa ajenda ila ngoja itokee kwa ATCL kesho yake front page kwa maandishi makubwa meusi
 
wanamuonea bure chenge. Yeye alikuwa anatekeleza ilani ya ccm ya kuliibia taifa...
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders

Mkuu una hasira sana na hizi mambo.

ndio hivyo tena tushafika hapa.
 
wanamuonea bure chenge. Yeye alikuwa anatekeleza ilani ya ccm ya kuliibia taifa...
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders
Naona dish limeyumba kiongozi hukamati chanel ...........Fastjet na ccm wapi na wapi?
 
Wakuu jioni hii nilikuwa nasafiri na Fastjet ya kwenda Mbeya,nilifika mapema sana uwanjani kwa ajili ya kuwahi safari yangu

Kufika pale uwanjani,nikafanya kuchekiwa na mpaka kupewa "boarding Pass" kuelekea Mbeya.Muda ukafika tukaingia mpaka katika ndege na kukaa tayari kwa kuondoka.Baada kama ya dakika 20 tukatangaziwa kuwa ndege ni mbovu hivyo haiwezi kwenda Mbeya.

Abiria wote tukaambiwa tushuke,watu wakawa wabishi pale na kelele za hapa na pale.Tumeuliza tatizo ni nini?Wanasema tu ni "Technical Faults"...Mle ndani ikawa joto sana mpaka wakalazimika kufungua mlango wa mbele na ule wa nyuma wa kushoto na kulia.

Baada kama ya saa moja hivi,ikaamuliwa wote tushuke na tukutane pale nje ili tupewe utaratibu.Lakini ukweli ni kuwa safari ya Mbeya leo hakuna,na nasikia hata kesho pia hakuna.Ukiwauliza wanasema ndege ni mbovu.

Nilikuwa nimekaa seat moja na bibi harusi mtarajiwa,ambaye jana alishindwa pia kwenda Mbeya sababu ndege ilijaa(overbooking) na leo pia ndege ni mbovu.Huyu bibi harusi mtarajiwa ana "send off" yake kesho.Nimemuacha hapo analia kama mtoto...Hata kesho akichukua "Super Feo" lazima atafika Mbeya wakati watu washaingia ukumbini.Fastjet wanasema kwa sasa ndege ya kwenda Mbeya ipo moja tu mchana saa 1430hrs,ile ya asubuhi wameifuta.

Lakini ajabu tukiwa palepale uwanjani,tumesikia ndege ya Fastjet inaondoka kwenda Mwanza,na wanatangaza abiria wa Mwanza kwa kutumia Fastjet wapitee geti namba fulani tayari kwa safari.

Sasa huu ubovu wa ndege ni kwa safari ya Mbeya tu??Wengine tulikuwa na safari za haraka za kibiashara na kesho asubuhi tulihitajika,sasa hata kesho tena uhakika hakuna?Kumbe sio ATCL tu,hata Fastjet nao wamepaki "bombadia" yao!!Usafiri wa anga ni kiboko
MKOMEEEE KABISA DHARAU ZA ATCL ZINAWATOKEA PUANI

NUKUSAIDIE NDEGE HUPANGWA SIKUMOJA KABLA REG KADHAA ITAENDA MWANZA NA REG KADHAA MBEYA... NA ASBH WANATUMA DETAILS KWENDA TCAA NA KUTOA INFO ZA WEATHER NK..

SO KAMA YENU IMEPATA TECHN AIMAANISHI NA YA MWANZA ISIENDE MKUU..WE SUBIRIA IPONE YAKO UENDE NA SIO KUOMBA YA WENZIO....ULICHOTAKIWA KUFANYA NI KUOMBA REFUND UENDE PW AMA NDEGE ZINAZOENDA MBEYA UNAJAZIA KILICHOBAKI ELSE ...MSIKATE TAMAA NDEGE YENU PENDWA ATCL HAIFI MILELE IKO NA ITAENDELEA KUWEPO..UKIONA NDEGE IKOCHINI INA SABABU SHUKURU MUNGU
 
Viwanja vya mbeya na mtwara.......vinategemea sunset na sunrise ..kama mpwa alivyosema JUU
Havina TAA naomba tukubali hali halisi na mshukuru MUNGU KWA KILA JAMBO...
 
Back
Top Bottom