Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Wakuu jioni hii nilikuwa nasafiri na Fastjet ya kwenda Mbeya,nilifika mapema sana uwanjani kwa ajili ya kuwahi safari yangu
Kufika pale uwanjani,nikafanya kuchekiwa na mpaka kupewa "boarding Pass" kuelekea Mbeya.Muda ukafika tukaingia mpaka katika ndege na kukaa tayari kwa kuondoka.Baada kama ya dakika 20 tukatangaziwa kuwa ndege ni mbovu hivyo haiwezi kwenda Mbeya.
Abiria wote tukaambiwa tushuke,watu wakawa wabishi pale na kelele za hapa na pale.Tumeuliza tatizo ni nini?Wanasema tu ni "Technical Faults"...Mle ndani ikawa joto sana mpaka wakalazimika kufungua mlango wa mbele na ule wa nyuma wa kushoto na kulia.
Baada kama ya saa moja hivi,ikaamuliwa wote tushuke na tukutane pale nje ili tupewe utaratibu.Lakini ukweli ni kuwa safari ya Mbeya leo hakuna,na nasikia hata kesho pia hakuna.Ukiwauliza wanasema ndege ni mbovu.
Nilikuwa nimekaa seat moja na bibi harusi mtarajiwa,ambaye jana alishindwa pia kwenda Mbeya sababu ndege ilijaa(overbooking) na leo pia ndege ni mbovu.Huyu bibi harusi mtarajiwa ana "send off" yake kesho.Nimemuacha hapo analia kama mtoto...Hata kesho akichukua "Super Feo" lazima atafika Mbeya wakati watu washaingia ukumbini.Fastjet wanasema kwa sasa ndege ya kwenda Mbeya ipo moja tu mchana saa 1430hrs,ile ya asubuhi wameifuta.
Lakini ajabu tukiwa palepale uwanjani,tumesikia ndege ya Fastjet inaondoka kwenda Mwanza,na wanatangaza abiria wa Mwanza kwa kutumia Fastjet wapitee geti namba fulani tayari kwa safari.
Sasa huu ubovu wa ndege ni kwa safari ya Mbeya tu??Wengine tulikuwa na safari za haraka za kibiashara na kesho asubuhi tulihitajika,sasa hata kesho tena uhakika hakuna?Kumbe sio ATCL tu,hata Fastjet nao wamepaki "bombadia" yao!!Usafiri wa anga ni kiboko