Ndege ya ATCL Yapasuka Kioo; yazuiwa kuruka KIA

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Habari za uhakika zinadokeza kuwa ndege ya ATCL namba TC 100 ambayo ilikuwa imeondoka Dar mapema asubuhi hii kuelekea Mwanza ikipitia KIA imepasuka kioo na hadi hivi sasa haijajulikana kama kilipasuka ndege ikiwa angani au baada ya kutua KIA. Kioo kilichopasuka ni kile cha pembeni kwa rubani upande wa kushoto kwa mujibu wa vyanzo vyangu JNIA.

Ndege hairuki sasa hivi hadi hali itengemae... kuna delay ya muda usiojulikana..

NB: NIlisema sitaki kugusa tena mambo ya ATCL lakini this one I couldn't pass to inform you.

Updated:

Kioo kilipasuka wakati wanajiandaa kuondoka KIA kwenda Mwanza...

Ndege inaonekana haiwezi kuondoka tena KIA leo; abiria wanatafutiwa usafiri mwingine.. (msiniulize wa chombo gani!)
 
Nimewai kuwaambia rafiki zangu kuwa Mwakyembe kapewa ile wizara hili kumfuta kabisa kwenye ramani ya siasa. Ukweli ni kuwa Mwakyembe hataweza kuimili hujuma dhidi ya ile wizara. Utaweza kuimarisha reli ya kati wakati kuna familia za vigogo wanamiliki malori ya mizigo kama njugu? Utawezaje kuimarisha ATCL wakati kuna familia za wakubwa wana hisa kenye airways, precision airways nk. Hakika Mwakyembe atachemsha.
 
Nawapongeza waliozuia isiruke kuepusha madhara kwa watanzania wasio na hatia 'shame on th'z govrnmnt'
 
Moderator ondoa hii kitu ,usione soo,haihusiani na siasa ,haki sawa kwa wote !
 
Habari za uhakika zinadokeza kuwa ndege ya ATCL namba TC 100 ambayo ilikuwa imeondoka Dar mapema asubuhi hii kuelekea Mwanza ikipitia KIA imepasuka kioo na hadi hivi sasa haijajulikana kama kilipasuka ndege ikiwa angani au baada ya kutua KIA. Kioo kilichopasuka ni kile cha pembeni kwa rubani upande wa kushoto kwa mujibu wa vyanzo vyangu JKNIA.

Ndege hairuki sasa hivi hadi hali itengemae... kuna delay ya muda usiojulikana..

NB: NIlisema sitaki kugusa tena mambo ya ATCL lakini this one I couldn't pass to inform you.

Mhh!! Mwanakijiji....kupasuka kioo angani?? Ndege iende mpaka itue kwenye kiwanja sawia??? Sijasoma sana elimu hii ya anga, ila kwa uelewa wangu fuatilia ni anga gani au wakati ndo inatua??....Hebu tujuzane pressure itakayokuwa ndani ya ndege kwenye anga (above 4k feet) kwa ndege kubwa ya abiria....lazima itajipeleka inapotaka na siyo rubani aipeleke anapotaka
 
Ingekuwa angani halafu kioo kikapasuka I'm sure huyo rubani angekuwa SUCKED OUT. Ndege ikiwa angani pressure ndani ya cabin inakuwa ndogo kuliko pressure nje ya cabin.
 
Uhakika utajulikana maana hicho ni kioo cha rubani wa ndege na bila shaka rubani ndio aliyeripoti hitilafu hiyo.
 
ATCL haikuwa na ndege nzima hata moja (Baada ya ile ya mwisho kuangukia pua).. Hii iliyopata ajali ni iliyokodiwa au ni ipi?
 
Nimewai kuwaambia rafiki zangu kuwa Mwakyembe kapewa ile wizara hili kumfuta kabisa kwenye ramani ya siasa. Ukweli ni kuwa Mwakyembe hataweza kuimili hujuma dhidi ya ile wizara. Utaweza kuimarisha reli ya kati wakati kuna familia za vigogo wanamiliki malori ya mizigo kama njugu? Utawezaje kuimarisha ATCL wakati kuna familia za wakubwa wana hisa kenye airways, precision airways nk. Hakika Mwakyembe atachemsha.

Analijua hilo. anajua Mabasi karibu yote ni ya wabunge na si..pi..ka.
 
Ngoja tusubiri wataziba kwa nylon na wataandikia wametumia mamilioni kufanya matengenezo.
 
Back
Top Bottom