Ndege ya Air Tanzania yapata ajali ikiwa na abiria 35 Kigoma, hakuna vifo

Rwanda, Uganda hata Burundi, Kenya usipime wana ndege nyingi tu lakini TZ imeshindikana, kuna nini hapa kwetu? Ndege moja inakuwa 'over used', bila shaka huu ni mwisho wa ATCL, Wana Kigoma wameingia matatani tena. Precisionair lazima wataongeza nauli kati ya TZS 450,000 hadi 500,000 'go & return' badala ya TZS 342,000 za ATCL. Mungu ihurumie Kigoma, ATCL na TZ kwa ujumla. Amen.
 
Habari za Usafiri wa Anga kwa nchi yetu ni za masikitiko sana!
Hapa ninchosema ni kwamba serikali haina nia ya dhati ya kupata shirika la ndege lenye nguvu. Mtu yeyote angeiona ile Dash-8 ya ATCL hakika imechoka na inasikitisha!...ni chombo gani kinachowza kuhimili mikikimikiki ya safari za kila siku bila hata ya kupoozwa siku moja, wakati kimechakaa?
kAMA haiwezekani kuendesha shirika hili ni bora kulifutilia mbali kabisa kuliko kuendelea kulipa watu kuendesha maofisi yasiyokuwa na tija!
Rais ana ndege yake , nadhani haoni umuhimu wowote wa kulisimamisha shirika hili kwaajili ya watanzania.
 
Wanachojua ni kuvua ubunge ,wabunge wa CDM yaani nchi haina ndege mpya inaenda kununua mitumba ya ndege,wananchi wangeweza wangesusia kupanda hiyo mitumba period
 
ndugu zangu picha zipo ila network ipo slow sana ndege ipo mita chache kabla ya bwawa na inasemekana iliparamia katuta kadogo kalikoachwa na wanaopanuwa uwanja then ikakosa uwelekeo kama kuna mtu ana whats app naweza kumtumia picha then akaload kwa jf anibip 0784296468
 
Tanzania inahitaji marekebisho makubwa katika idara za ulinzi na usalama, ufisadi uliojengeka juu ya ubinafsi unabomoa misingi imara ya uzalendo na undugu iliyokuwepo tangu kuasisiwa kwa taifa.
Ni muhimu kufahamu kwamba katika zama hizi za utandawazi na biashara huria, mashirika ya uma kama ATC, TRC n.k yatahujumiwa kwa sababu za ushindani wa kibiashara.
Mbaya zaidi ni kwamba baadhi ya viongozi ni wanahisa katika makampuni shindani na hivyo kuwepo uwezekano wa kutumia nafasi zao kupitia udhaifu katika idara za ulinzi na usalama kuhujumu ili makampuni yao yamiliki soko.
Kwa hali ilivyo, idara za ulinzi na usalama zimeelekeza zaidi majukumu yake kwenye siasa na kusahau majukumu yake ya msingi ya kulinda wananchi, mali zao na mali za uma.
Maboresho yanahitajika katika sera ya ulinzi ili kuimarisha ulinzi wa uma kiuchumi zaidi.
 
Ule mswada wa manunuzi ya vitu chakavu kama jk alisaini matunda yake ndo haya yanaanza kuonekana, tutayafaidi sana,tukae mkao wa kula, matukio ya aina hii yatakuwa mengi zaidi!
 
Kina Lissu walipiga sana kelele Bungeni kwamba kuruhusu ununuzi wa Ndege Mitumba ni kuruhusu ajali wenyewe wakadharau. Na naomba wakinunua zingine zianguke na kuanguka ilimradi watu wanusulike. Jamani ndege si za kununua used. Ona kama hii abiria 38 tu imeshindwa kupaa. Je ingejazwa capacity yake ya abiria 120?
 
tbc ndio wamechemsha . amina mollel karudia mara tatu kwamba ndege imeanguka.
 
Kina Lissu walipiga sana kelele Bungeni kwamba kuruhusu ununuzi wa Ndege Mitumba ni kuruhusu ajali wenyewe wakadharau. Na naomba wakinunua zingine zianguke na kuanguka ilimradi watu wanusulike. Jamani ndege si za kununua used. Ona kama hii abiria 38 tu imeshindwa kupaa. Je ingejazwa capacity yake ya abiria 120?

Huu ushabiki wa siasa umetuathiri sana, kila kitu zimekuwa siasa.
Kasome vizuri technologia ya ndege, ndege inachukua muda mrefu sana kutolewa kazini, cha msingi ni matengenezo yanayotakiwa. Precisionair, KQ na hata hao qatar, emirates wanatumia ndege used na mpya cha msingi ni kuzingatia matengenezo. Precisionair ndege karibia zote ni used na mnapanda, akinunua ATC porojo nyingi.
 
da aisee nilijua tu hii ndege haitachukua round. Juzi nilitokanayo tabora ilikuwa inayumba sana na inatingishika sana wakati wa kutoa. Nilikuwa naogopa sana ila tushukuru mungu haijaleta madhara
 
Siku mmoja tulipanda hiyo ndege, wakati tunakaribia kuanza safari injini ikagoma kuwaka. Wakatwambia kwamba safari haitakuwepo na ndege inabidi ipelekwe garage. Can u imagine that?
 
kama Mtanzania.....habari za Air Tanzania zinaniuma sana.......
hasa pale ninapoona Kenya Airways, Rwanda Airways na Air Uganda......
sijui ni nani ametuloga jamani.........

NI siasa ya ujamaa na kujitegemea iliyotufikisha tulipo. Amini usiamini.

"Mali ya umma" ndio kiini cha kufa kila kitu katika Tanzania.
 
Ngoja 2chapane kwanza ndo 2taheshimiane haiwezekana hawa wapuuz wamesha2ona cc wake zao, c ndege nyingine ilidondoka ikakaa mpka buibui wakaweka mautandu yaan hata shirika binafs precision air inalizid ATCL , miviongoz inabak kuweka mi2mbo 2 kwenye ofis za umma aaarrrggghh
 
Serikali haina nia madhubuti ya kulikwamua shrika la ATCL....Ndege ilyodondoka ni aina ya DH-8 inayofanya scheduling ya Tabora to Kgoma to Dar kila siku iendayo kwa Mungu!ni ndege moja tu ndo imebaki...ipo nyingine mpaka leo nasikia ipo Hangar ya ATC ikifanyiwa matengenezo makubwa(wenyewe wanaita check-3)...kwa safari hizi ni hakika ndege moja haitoshi..inachoka na ni hatari kwa usalama wa abiria na Taifa!Ni kwanini ATC?Leo shirika binafsi la Precision linamiliki ndege kadhaa aina ya ATR45,ATR75 na BOING-733 Mbili...zinafanya safari ndani na nje ya nchi...Comoro,Nairobi adi South Africa kwanin sio ATC?Leo kuna 540.COM...Lina DH-8,CRJ-CANADIAN Kwanini sio ATC?Kwanin watu binafsi waweze halafu serikali yenye dhamana na kila amana ishndwe?kuna mkono wa Mtu na tunahtaji mabadiliko ya kweli..ni AIBUUUUUUU na uku nje ya nchi tunaaibika sana!
 
Back
Top Bottom