Ndege ya Air Tanzania yapata ajali ikiwa na abiria 35 Kigoma, hakuna vifo

Naililia nchi yangy Tanganyika, lakini Mungu alisema watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa. Sasa inadhihirika tz
 
wakuu nimesikia toka radio ccm_uhurufm sasa hivi kuwa ndege ilishindwa kuruka na kuacha njia na kuserereka maporini. matairi yameng'oka na bawa moja pamoja na injini vimevunjika vby. mungu mkubwa watu wote wamepona. ilianza kuwaka moto lkn zimamoto wameudhibiti moto.
 
Tusubiri tume kama kawa, na sijui huwa wanalipwaje wanaoteuliwa kwenye tume.
 
sema imeshindwa kupaa na wala haijadondoka..naona title iko so strong hapa.

Kama ni kosa basi ni hilo shirika lako la TBC ambalo wametoa hiyo taarifa. Hata mimi nimesikia tena wamerudia mara tatu, 'imeanguka' wakati ikijaribu kuruka. Ila naungana na wewe kuwa yawezekana imeshindwa kuruka na si kwamba imeanguka
 
Breaking news!!!! Ndege ya ATC yaanguka uwanja wa ndege Kigoma!source TBC1 breaking news, inasema watu 35 wamenusurika, habari zaidi baadaye. Mdau mwenye taarifa zaidi atupatie.
 
du!! hatuna ndege sisi ....nchi ya mafisadi hii wanashindwa na kenya,ethiopia......sisi tunaviongozi wahuni
 
Ndege ya shirika la ndege lapata ajali, ilikuwa inatokea Mwanza kuelekea Kigom.
Source: Mwananchi Communication Ltd
 
Source TBC1

Abiria wote wanusurika wakati ikipaa na imekadiriwa ni abiria 38

Hivi ndo hizi walizopisha bungeni zinunuliwe (mtumba) au ndo enzi za mwalimu

Kweli ng'ombe wa masikini hazai na kizaa dume na laweza kufa with no tym
 
wakuu nimesikia toka radio ccm_uhurufm sasa hivi kuwa ndege ilishindwa kuruka na kuacha njia na kuserereka maporini. matairi yameng'oka na bawa moja pamoja na injini vimevunjika vby. mungu mkubwa watu wote wamepona. ilianza kuwaka moto lkn zimamoto wameudhibiti moto.

Loh ee Mungu epusha maafa!
Tena nilikuwa nibook flight ya kenda Tabora kesho, kweli ATC ni wasi wasi mtupu!
 
Jana Lukuvi alisema JK anashindwa kutekeleza mipango yake kwani IKULU kuna MAPEPO, nadhani hayo mapepo yapo hata huko ATCL
 
Back
Top Bottom