Ndege ya Air Tanzania yapata ajali ikiwa na abiria 35 Kigoma, hakuna vifo

Ndege ya shirika la ATC iliyokuwa na abiria 35 imeanguka wakati ikiwa inapaa kutoka uwanja wa ndege Kigoma.Abiria wote wako salama.
Source : TBC - Habari Mpasuko saa 5:00 asbh
 
Nimewahi kuruka na hiyo ndege siku moja kutoka kigoma kwa kweli ilikua safari ngumu sana maana kwanza kuruka ilikua kasheshe sana....ikayumba mbayaa...sasa tatizo nchi hii ukisema ukweli ni shida..nchi ina ujinga mwingi sana..
 
2mekupata kk pole sana kwa majeruhi wote ndiyo maisha bora kila mtanzania yalivyo 2nasafiria mabomu bila kujijua.
 
Ilikuwa nimeshaacha ardhi au ilikuwa runway? Make kuanguka ni kutoka juu na kupiga ardhi
 
Toa maelezo sahihi imeshindwa kuruka au vipi kama ilisha paa lazima ingelipuka
 
Du hizi ndege za ATCL ni hatari jamani kuweni makini, Mungu awatangulie ndugu zetu waliokuwa katika hiyo ndege kama wamepata majeraha wapone haraka.
 
Kulikuwa na debate kali sana kuhusu mipango ya kununua mitumba. Na Waziri Nundu akang'aka sana huku akitetea azma ya serikali ya kubadili sheria ili tununue mitumba. Ningetaka kujua kama hii ndege ni miongoni mwa mitumba ya serikali?
 
Tumenunua RADA kwa bei mbaya kwa ajiri ya kungalia ndege zetu mbovu zitakapoanguakia. lkn hata ndege zenyewe haziruki zinaaanguka viwanjani na macho yetu ya kawaida ndo yanaziona. Ha ha ha ha....
 
Back
Top Bottom