Ndege ya Air Tanzania yapata ajali ikiwa na abiria 35 Kigoma, hakuna vifo

mgadafi

Member
Feb 27, 2012
54
18
Air Tanzania iliokuwa inaondoka leo Kigoma nusura kuanguka wakati ikiruka na imejipiga chini ndani ya bwawa ila hakuna abiria aliyepoteza maisha.
========

Habari zaidi..

Ndege pekee ya Shirika la Ndege la Tanzania "Air Tanzania" imepata ajali wakati ilipokuwa inajiandaa kuanza safari ya kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam, kupitia Tabora.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumatatu milango ya saa 4 na robo asubuhi kwa saa za eneo hilo, ikiwa na abiria 35 na wafanyakazi wanne.

Ndege hiyo iliteleza wakati ilipokuwa inajitayarisha kuruka. Wanawake wawili wazee wamekimbizwa hospitalini kutokana na mshituko waliopata.

Kuna taarifa mbalimbali zimetolewa kuhusu sababu ya ajali hiyo huku baadhi wakisema kuwa barabara ya kurukia ndege ilikuwa inateleza sana huku wengine wakisema kuwa kufeli kwa injini ya ndege ndiko kulikosababisha ndege hiyo ilale upande wa kulia na kuharibika sehemu ya mbele, bawa na injini ya pangaboi.
atc-kigoma.jpg
 
mkuu upo kigoma?
Niliona hizo ndege zikifanyiwa ukarabati dar..niliogopa hakika
Mbuzi wa masikini hazai labda atage mayai
 
Kila sekta nchi hii matukio ya kizembe kwa jina la ajali ni mengi.Tuna wataalam kama hatuna,tuna sheria kama hatuna,tuna uongozi kama hatuna! Kila tukio twajisemea ni mpango wa Mungu.Mimi siamini kama hatuna kinga katika yote tunazoita ajali.?
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana,hata kama ni itirafu sio kama hii,huu ni uzembe fukuza kazi safu yote ya technical.
 
Wabongo tumezidi kumsingizia Muumba kila mapungufu yetu tunayaihifadhi kwa Muumba. Tuwe wakweli wanafsi zetu kama kuna uzembe/kutojali watu wanastahili kuwajibika. Katika hili namshukuru Mungu kunusuru maisha ya waja wake ambayo uhenda yangepotea kwa kusababishwa na uzembe wa watu flani. Usishangae Bongo ukipigia simu ZIMA MOTO ukiwajulisha kuwa nyumba inaungua usishangae kukushauri baki ndani ua nyumba hadi tutakapofika kukuokoa!!!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: tz1
kama Mtanzania.....habari za Air Tanzania zinaniuma sana.......
hasa pale ninapoona Kenya Airways, Rwanda Airways na Air Uganda......
sijui ni nani ametuloga jamani.........
ccm na watendaji wake wa type ya mataka
 
kama Mtanzania.....habari za Air Tanzania zinaniuma sana.......
hasa pale ninapoona Kenya Airways, Rwanda Airways na Air Uganda......
sijui ni nani ametuloga jamani.........

Lawama yote ni ya serikali tawala! Hakuna

aliyetuloga (Ni mafisadi tu)
 
kudadadekiiii, aibu gani hiii , ndege zenyewe zipo mbili tu , then zinatushindwa kutunza,
IVI SISI TUNAWEZA NINI JAMANI?????
Juzi treni limezima njiani kisa WESE hakuna ...

sisi kama tumelogwa. nakumbuka ******- alikwenda kusaini mkataba wa anga huru nchini uturuki , sasa sijui hii MIKANGAFU yetu kama inaweza kupaa anga za KIMATAIFA

Poleni watanzania WENZANGU
 
Ndio maana ni muhimu kabisa kwenye katiba mpya inayokuja madaraka ya rais yapunguzwe. Hatuwezi kupiga hatua kama rais anakuwa anateua hata MD wa mashirika kama Air Tanzania. Matekeo tunakuwa na makada badala ya watu wenye uwezo wa kufanya maauzi ya kibiashara.
 
kama Mtanzania.....habari za Air Tanzania zinaniuma sana.......
hasa pale ninapoona Kenya Airways, Rwanda Airways na Air Uganda......
sijui ni nani ametuloga jamani.........

Tumelogwa na MAGAMBA
 
Wabongo tumezidi kumsingizia Muumba kila mapungufu yetu tunayaihifadhi kwa Muumba. Tuwe wakweli wanafsi zetu kama kuna uzembe/kutojali watu wanastahili kuwajibika. Katika hili namshukuru Mungu kunusuru maisha ya waja wake ambayo uhenda yangepotea kwa kusababishwa na uzembe wa watu flani. Usishangae Bongo ukipigia simu ZIMA MOTO ukiwajulisha kuwa nyumba inaungua usishangae kukushauri baki ndani ua nyumba hadi tutakapofika kukuokoa!!!!!!!
nakuunga mkono mkuu!
 
Source TBC1

Abiria wote wanusurika wakati ikipaa na imekadiriwa ni abiria 38

Hivi ndo hizi walizopisha bungeni zinunuliwe (mtumba) au ndo enzi za mwalimu
 
sema imeshindwa kupaa na wala haijadondoka..naona title iko so strong hapa.
 
Back
Top Bottom