Ndege ya Abiria yapigwa na Radi na kuanguka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndege ya Abiria yapigwa na Radi na kuanguka!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, Aug 19, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  abiria 130 wanusurika Send to a friend Tuesday, 17 August 2010 21:35

  [​IMG]Ndege iliyoanguka bila kusababisha kifo cha abiria waliokuwa wakisafiri

  Andrew Msechu na mashirika ya habari

  ABIRIA 131 waliokuwemo katika ndege ya Boeing 737 hawakuamini macho yao, kila mmoja akitioka na kushuhudia akiona muujiza baada ya ndege waliyokuwemo kuanguka na kuvunjika vipande vitatu bila wao kuathirika.

  Gavana wa mji wa mji wa San Andres, Pedro Gallardo alielezea tukio hilo kuwa ni muujiza baada ya ndege hiyo iliyokuwa na abiria 125 na wahudumu sita kuanguka na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine sita kujeruhiwa.

  “Huu ni muujiza, tunatakiwa kumshukuru Mungu,” alisema Gallardo.

  Madhara ya ajali hiyo ni kinyume na mazoea, kwani ajali nyingi za ndege za abiria zimekuwa zikisababisha vifo vya abiria wote na kama wakiwepo walionusurika basi ni idadi isiyozidi mtu mmoja, mara nyingi watoto.

  Kutokana na ajali hiyo iliyowashangaza wengi, mamlaka nchini humo zilieleza pia kwamba ilitokea ghafla kwa kuwa hata rubani wake hakuweza hakuweza kutoa taarifa kwenye kituo cha kuongozea ndege kwenye kisiwa hicho cha San Amdres, Colombia.

  Abiria aliyeripotiwa kufariki dunia katika ajali hiyo alitajwa kuwa ni Amar Fernandez de Barreto, 68, ambaye hata hivyo kifo chake kimeripotiwa kuwa huenda kimetokana na ugonjwa wa moyo.

  Kwa mujibu wa taarifa, abiria wengine kadhaa waliwahishwa hospitali kwa matibabu ta majeraha madogo madogo, baada ya ndege hiyo kuanguka ardhini ilipukuwa ikijiandaa kutua baharini baada ya kutokea hitilafu ya kiufundi.

  “Rubani alitueleza kwamba tunakwenda kutua kwenye uwanja wa San Andres, tulifunga mikanda yetu na kutulia, sekunde kadhaa baadaye, tukasikia kishindo kikubwa. Mimi na mke wangu tulipogeuka nyuma tuliona upande wa nyuma wa ndege haupo,” alisema mmoja wa manusura, Alvaro Granados ambaye alikuwa akisafiri pamoja na mkewe na watoto wao wawili.

  Wakala wa ndege hiyo, Erika Zarante alisema miongoni mwa abiria waliokuwemo katika safari hiyo ni raia wanne wa Brazil, Wajerumani wawili, raia wawili wa Costa Rica na Wafaransa wawili.

  Kanali David Barrero wa jeshi la anga la Colombia alieleza muda mfupi baadaue kwamba wanafanya uchunguzi kuhusu taarifa kwamba ndehe hiyo ilipigwa na radi ilipokuwa ikikaribia kwenye kisiwa cha San Andres.

  Mara tu baada ya kuanguka kwa ndege hiyo abiri waliripotiwa kuhangaika kujinasua katika viti vyao na muda mfupo polisi wa doria waliweza kufika Katina eneo hilo na kwuasaidia, ikiwemo kuzima moto uliokuwa umeanza kuwaka katoka injini za ndege hiyo.

  AFP
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Sifa kwa BWANA kwani ametenda muujiza.
   
Loading...