Ndege waliyopanda "Boyz II Men" 1995 ni Ya Rostam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndege waliyopanda "Boyz II Men" 1995 ni Ya Rostam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Mar 9, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  nakumbuka kwamba boyz to men walivyowasilisha fomu za uraisi 1985, walikwenda kwa ndege, na ndege hiyo ilitolewa na Rostam azizi kama sikosei, kwa kampuni iliyo Kenya, hivyo inabidi tuanzie huko ili kupata Mzizi wa Madudu yanayo tokea Leo
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu inaonekana huyu jamaa alitafuta sana remote control, sasa hivi ameishika na anaitumia kwelikweli.
   
 3. n

  nzala Member

  #3
  Mar 9, 2009
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Heshima mbele,mkuu hiyo ndege walipanda 1995,sio 1985.usijali lakini ni typing error!!!
   
 4. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Inamaana walienda kwa ndege ya kukodi?
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  asante kwa kunisahihisha ni kweli 1995,
   
 6. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni kweli walitua dodoma kwa kidege. ila ushahidi zaidi kwamba ilikuwa ya Rostam.
  Najua Rostam alitumia fedha nyingi kumuingiza JK ikulu akishirikiana na Rostam.
   
 7. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka vizuri kipindi hicho .......Lakini sikufahamu kuwa Ndege ile iliyolakiwa na Wazee wa CCM wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mzee Pancras Ndejembi ilikuwa imekodiwa na RA.Nakumbuka pia siku mbili baada ya hawa Waungwana kurudisha form,Mwalimu alikuwa anaondoka kwa ziara ya Nje ya Nchi,aliita Press conference pale nyumbani kwake Msasani,na kuna Muandishi Mmoja Mwandamizi wa Daily News alimwambia Mwalimu anawaonaje "Kikwete na Lowassa,kwani ni vijana wenye mvuto na inaonekana kuwa ni Viongozi wazuri,ambao wana uwezo mkubwa wa kuliongoza Taifa la Tanzania" Mwalimu kwa jibu la Mkato alimwambia Mwandishi huyo kuwa hana wasiwasi na utendaji kazi wa Wana-ccm hao lakini suala la Uzuri (Mvuto) Mwalimu alisema kama umewapenda waalike ukanywe nao chai.......watu walicheka, lakini maneno hayo ya mwalimu yalionekana alikuwa hakubaliani na yeyeto kati ya watajwa kuingia katika kinyang'anyiro kile kwa tiketi ya CCM.

  Leo hii wote wawili tunawaona katika siasa za kila siku za Tanzania.....Mmoja kaachia manyanga baada ya madudu ya Richmond...Huyu Mwingine anazunguka kila pande na usanii usiokwisha,Kila siku kuna jipya (Kashfa) serikali inaendeshwa kama kikosi cha zimamoto...Natamani Nyerere aamke huko aliko na akumbane na yule Mwandishi aliyeona Mvuto/Uzuri ni sifa ya kuongoza watu,Wallahi Mwalimu angemtukana yule Mwandishi!!!
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Mbona hii imekaa kana kwamba 'unabifu' na mmoja wapo? Nimekuwa nikisoma michango yako mingi lakini huu nikiusoma ninaona uko nje kabisa na standards zako nilizozizoea? nimekuwa nikikuona mara nyingi ukisistiza constructive criticism...kulikoni... au hasira?
   
 9. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi hakuna muungwana anayefanya kazi JKNIA (DIA) au Dodoma Airport akatutafutia data za ile ndege ili tuanze kudodosa mpaka mahusiano kamili ya JK na Rostam yawekwe wazi?

  Huko bungeni na ndani ya CCM wameshashindwa kumuweka Kikwete kiti moto, lakini tukiweka data mtandaoni, wanamagazeti wanaweza kutusaidia angalau kumfanya JK asiendelee beyond 2010.
   
 10. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Hapana ...wala sio hasira, Hawa waungwana imefika wakati sasa wanapoteza muelekeo kabisa..Na kama kweli tunawatakia Mema ni bora kueleza wazi kuwa wanakosea kuliko kuwapamba kwa uongo!!!Sina Bifu na Muungwana ni mtu ninayemuheshimu sana tu....Lakini uwezo wake wa Uongozi umekuwa unapungua kwa kasi mno...mwanzo nilifikiri kuwa labda ni uoga na ushikaji ndio unamfanya awe na unyonge....lakini sasa nafikiri kuna tatizo kubwa zaidi ya hayo....Mwenzangu kama huoni basi mapenzi yako yatakuwa yamekutia upofu.....
   
 11. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hukuwa tayari kuanzisha mada?
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,318
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Ile ndege nakumbuka ilikuwa kama si Zanair basi ilikuwa Coastal Travel
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Siri nyingine ambayo hadi leo baadhi yetu hatuifahamu ni jinsi EL alivyochujwa kwenye mchakato ule wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM 1995. Mwalimu alimwambia nini EL? Kwa nini baadaye 2005 EL hakuchukua fomu? Ni nini hasa kilimsukuma JK kumpa EL uwaziri mkuu pamoja na yote yaliyosemwa 1995?
   
 14. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mwawado the way ulivyo react ktk hii thread unanifanya nihisi wewe ni Comrade Mnali nini?!!!
  Hahahaaaaaaaaa, just kufurahisha baraza tu mtaalam Mwawado. Endelea kuwa huru ndg yangu.
   
 15. Companero

  Companero Platinum Member

  #15
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ndio. Walisubiri mpaka dakika ya mwisho. Hivyo wangepanda gari wangechelewa. Kwa Kiingereza wanasema 'Saving the Best for the Last'!
   
 16. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haya yote yanatokana na dhambi ya kuwaponda wengine kuwa huyu ni mpemba mara hisbulaa,sasa dhambi hii itawatafuna hadi mwisho kwani ndio mbegu waliyopanda.RA,EL na JK wasingekuwa wanajuana angekwisha kuwashughulikia kitambo.Waziri wake na Mkurugenzi wa TANESCO wanashabikia mitambo chakavu na yenye kashfa halafu hachukui hatua.Tulishamshauri JK awabadilishe wakuu wa Wilaya na Mikao na Wakurugenzi mbalimbali waliowekwa na EL kwa maslahi yake, lakini hadi leo ameziba masikio.Sasa nchi kwanini isiendelee kuyumba wakati una wasaidizi wenye maslahi ya wengine lazima utaongoza kwa tabu.
   
 17. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kamwe timu iliyobebwa kwa namna yoyote ile haishindi mbeleni, Hao EL, RA, Karamaji, Vijisenti, Bangusilo etc ni watu waliompiga tafu na ni haohao wamezungukwa na karibu uozo wote tulionao hivi sasa, ngoja tuone uchaguzi 2010 utatupa majibu ambayo hatuna hivi sasa
   
 18. t

  tk JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ninyi mnachekesha kweli kweli. Mnapoteza muda kutafuta uhusiano wa JK, EL na RA wakati kuku na ndege wanajua kuwa hao ni marafiki wakubwa wa miaka mingi. Hamkumbuki kuwa hata kabla JK hajateuliwa kuwa mgombea maneno yalikuwa mtaani kuwa EL atakuwa waziri mkuu na RA atakuwa waziri wa fedha. Na JK mwenyewe akakiri katika kampeni zake kuwa hao ni marafiki zake. Sasa hizo data mnazozitafuta ni za ku prove nini. Kwani JK amekataa kuwa hao si maswahiba zake?

  Sijui objective ya hii thread ni nini? Mimi naona haina maana yeyote. Kusema JK ataondolewa 2010 sahauni. CCM bado inamtaka na hao ndio watakao amua.
  Kelele za mpangaji hazimnyimi usingizi mwenyenyumba.
   
 19. A

  August JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  tk, kwanza nashukuru kwa mchango wako hapo juu, pili ningependa kueleza madhumuni ya hii thread
  1. kuunganisha matukio ya baadhi ya characters kama el, ra etc na yanayo tokea nchini
  2. mtu anavyoweza kuwa sponsored na mafsadi ili agombe uongozi, na baada ya hapo kuwa mtumwa wa walio mfadhili.
  3 ni kuangalia au kuona ni kweli huyu kiongozi hawezi kujitoa kwenye hiyo minyororo ya mfadhili? au wananchi wanaweza vipi kukabiliana na jambo kama hili?
   
 20. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Kwa Tarifa zenu Rostam He is a Men ,strong man and no one can touch him when I say no one I mean not even single person in TANZANIA not to day and not tomorrow .hii itakuwa ni kumbukumbu nitakuja kukumbusheni wasomaji wezangu ni vizuri kuwa mnatowa maoni yenu lakini jamaa ni Realy Master
   
Loading...