Ndege nne kwa mpigo zilizoahidiwa na Serikali ikiwemo Boeing 787-8 Dream Liner zitaingia nchini Julai, mwaka huu

NDEGE nne kwa mpigo zilizoahidiwa na Serikali ikiwemo Boeing 787-8 Dream Liner zitaingia nchini Julai, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari katika utaratibu wake wa kila mwezi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk Hassan Abbasi alisema ndege hizo zinatengenezwa nchini Canada na zitakuwa tayari zimetua nchini miezi minne kutoka sasa.

Alisema wakati ndege hizo, zikiandaliwa kuja nchini, serikali imekuwa ikifanya ukarabati, upanuzi, urekebishaji na ujenzi wa viwanja zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali nchini ili miundombinu yake kutumika na ndege hizo. Dk Abbasi alitaja baadhi ya viwanja, vinavyofanyiwa ukarabati, kurekebishwa na kupanuliwa kuwa ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya, ambako linajengwa jengo la abiria ambalo halikuwepo siku nyingi.

“Jengo kama hilo linajengwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam maarufu kama Terminal III kwa ajili ya kuboresha huduma za abiria. Kwa upande wa uwanja wa ndege mjini Dodoma, Dk Abbasi alisema tayari ukarabati umefanyika, lakini pia kuna shughuli inafanyika katika uwanja mpya unaojengwa katika eneo la Msalato. “Viwanja vingine vinavyofanyiwa ukarabati, kupanuliwa na kujengwa majengo ya abiria ni Tabora, Mwanza, Geita, Musoma, Njombe, Lindi na vingine vingi.

Wakati huo huo, Dk Abbasi alisema serikali inaleta mabehewa 1,590 na vichwa vya treni 25 kwa ajili ya Reli ya Kisasa, inayojengwa kati ya Dar es Salaam na Morogoro na kati ya Morogoro na Dodoma. Alisema reli itakapokamilika katika kipindi cha miezi 36, mabehewa na vichwa vya treni, vinatakiwa kuwepo ili kuanza kazi ya kusafirisha abiria na mzigo mara moja. Alisema tayari zabuni ya kutengeneza mabehewa na vichwa hivyo imeshatangazwa, ambapo kampuni zaidi ya 54 zilijitokeza kuwania fursa ya utengenezaji huo.

Alisema kati ya hizo, kampuni 35 zimerudisha barua za zabuni na hizo uchambuzi wake wa kubaki na kampuni ya kutengeneza mabehewa hayo itakapopatikana. Alisema kampuni itakayoshinda zabuni, inatakiwa kutengeneza kwa miezi 24 na miongoni mwa mabehewa hayo 50 ni ya ngazi mbili, 100 ni ya mafuta, mengine ya watu mashuhuri na mengine ya kawaida. Vile vile, alisema serikali inatekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa meli za kisasa katika Maziwa Makuu nchini ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Alisema kuhusu Ziwa Victoria, serikali inatengeneza meli kupitia Kampuni ya TSX ya Korea Kusini ambayo mkataba wa kutengeneza meli hiyo ulisainiwa mwezi Machi, mwaka huu.

Chanzo: Habari leo

Jamani hizi habari mgesubiri kamanda apone kule ubelgihji.
Hivi hamumjui mnamuongezea maumivu?
 
Boeing 787 Dreamliner https://g.co/kgs/n4uakp
Ndio maajabu haya! Hata msemaji wa serikali hajui Dreamliner zinatengenezwa wapi? Basi hiyo habari yake ni kiki ya kisiasa tuu.
...kiki si ndo dili siku hizi mkuu?
Hukusikia juzi mwenyekiti wetu kaumwa kichwa, kalazwa na "kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua"?
 
Acheni porojo basi, si mzilete badala ya kila siku kupiga domo tu hapa?
 
Yaani ndege kuingia july ni habari ya march? Na july zikiingia ni kutoa taarifa tena?

Lengo la taarifa hii ni nini?
 
Kwa fedha zipi?
Serikali hiihii iliyoshindwa kuongeza mishahara kwa watoto/watumishi wake kwa miaka 2 mfululizo ndiyo ya kuleta ndege NNE kwa mpigo?
Usaniiiiiiiii
 
DEGE nne kwa mpigo zilizoahidiwa na Serikali ikiwemo Boeing 787-8 Dream Liner zitaingia nchini Julai, mwaka huu
Heading yako na hii kitu vinapingana.....subiri zifike ndio uandike heading kama hio, kiherehere cha nini
 
NDEGE nne kwa mpigo zilizoahidiwa na Serikali ikiwemo Boeing 787-8 Dream Liner zitaingia nchini Julai, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari katika utaratibu wake wa kila mwezi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk Hassan Abbasi alisema ndege hizo zinatengenezwa nchini Canada na zitakuwa tayari zimetua nchini miezi minne kutoka sasa.

Alisema wakati ndege hizo, zikiandaliwa kuja nchini, serikali imekuwa ikifanya ukarabati, upanuzi, urekebishaji na ujenzi wa viwanja zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali nchini ili miundombinu yake kutumika na ndege hizo. Dk Abbasi alitaja baadhi ya viwanja, vinavyofanyiwa ukarabati, kurekebishwa na kupanuliwa kuwa ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya, ambako linajengwa jengo la abiria ambalo halikuwepo siku nyingi.

“Jengo kama hilo linajengwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam maarufu kama Terminal III kwa ajili ya kuboresha huduma za abiria. Kwa upande wa uwanja wa ndege mjini Dodoma, Dk Abbasi alisema tayari ukarabati umefanyika, lakini pia kuna shughuli inafanyika katika uwanja mpya unaojengwa katika eneo la Msalato. “Viwanja vingine vinavyofanyiwa ukarabati, kupanuliwa na kujengwa majengo ya abiria ni Tabora, Mwanza, Geita, Musoma, Njombe, Lindi na vingine vingi.

Wakati huo huo, Dk Abbasi alisema serikali inaleta mabehewa 1,590 na vichwa vya treni 25 kwa ajili ya Reli ya Kisasa, inayojengwa kati ya Dar es Salaam na Morogoro na kati ya Morogoro na Dodoma. Alisema reli itakapokamilika katika kipindi cha miezi 36, mabehewa na vichwa vya treni, vinatakiwa kuwepo ili kuanza kazi ya kusafirisha abiria na mzigo mara moja. Alisema tayari zabuni ya kutengeneza mabehewa na vichwa hivyo imeshatangazwa, ambapo kampuni zaidi ya 54 zilijitokeza kuwania fursa ya utengenezaji huo.

Alisema kati ya hizo, kampuni 35 zimerudisha barua za zabuni na hizo uchambuzi wake wa kubaki na kampuni ya kutengeneza mabehewa hayo itakapopatikana. Alisema kampuni itakayoshinda zabuni, inatakiwa kutengeneza kwa miezi 24 na miongoni mwa mabehewa hayo 50 ni ya ngazi mbili, 100 ni ya mafuta, mengine ya watu mashuhuri na mengine ya kawaida. Vile vile, alisema serikali inatekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa meli za kisasa katika Maziwa Makuu nchini ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Alisema kuhusu Ziwa Victoria, serikali inatengeneza meli kupitia Kampuni ya TSX ya Korea Kusini ambayo mkataba wa kutengeneza meli hiyo ulisainiwa mwezi Machi, mwaka huu.

Chanzo: Habari leo

Bila kurekebisha uedeshaji wa ATCL hizo ni hela zinatupwa baharini kwa manufaa ya papa wachache.
 
KUTOKA CHADEMA LIBRARY.

1. Lowaasa ni Fisadi sisi tuna Ushahidi.
2,Tunahitaji Rais Mkali,huyu ni Dhaifu anacheka cheka.
3.Hii inaitwa Oparesheni Sangara ya Kutokomeza Mafisadi.
4. Huko CCM jembe ni waziri Magufuli tu,wengine Wezi.
5. Lowassa ni Nabii Musa au Joshua tunakwenda Kaanani.
6.. 2015 Ushindi Saa nne Asubuhi.
7. Matokeo hayatatangazwa Lubuva anajisumbua.
8. Tutashitaki ICC hataapishwa.
9. Hatumtambui Shein na Zanzibar haitatawalika
10. Tutaenda Dodoma kuzuia mkutano wa CCM,kitanuka.
11. Tumetoka Bungeni hatutarudi Mpaka TULIA aondolewe.
12.Magufuli ni Rais wa Muhula mmoja,One term.
13. Tutajenga UKUTA liwalo na liwe.
14. Tutakata funua liwalo na liwe.
15. kwenye Madini kuna MIGA Convertion,tutanyolewa bila Maji.,
16.Tumesusia Uchaguzi hatutashiriki.
17. Tutashiriki Uchaguzi kuionyesha CCM cha Mtema kuni.
18. CCM ikishinda Siha na Kinondoni Mbowe naacha Siasa!
19. Tutashinda Kinondoni na Siha kwa kishindo
20. Tarehe 26 tutaandamana nchi nzima kupindua Nchi.

What else can I say?...kuna nililosahau?

Wapinzani bhana
 
Back
Top Bottom