Ndege nne kwa mpigo zilizoahidiwa na Serikali ikiwemo Boeing 787-8 Dream Liner zitaingia nchini Julai, mwaka huu

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,483
2,000
NDEGE nne kwa mpigo zilizoahidiwa na Serikali ikiwemo Boeing 787-8 Dream Liner zitaingia nchini Julai, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari katika utaratibu wake wa kila mwezi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk Hassan Abbasi alisema ndege hizo zinatengenezwa nchini Canada na zitakuwa tayari zimetua nchini miezi minne kutoka sasa.

Alisema wakati ndege hizo, zikiandaliwa kuja nchini, serikali imekuwa ikifanya ukarabati, upanuzi, urekebishaji na ujenzi wa viwanja zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali nchini ili miundombinu yake kutumika na ndege hizo. Dk Abbasi alitaja baadhi ya viwanja, vinavyofanyiwa ukarabati, kurekebishwa na kupanuliwa kuwa ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya, ambako linajengwa jengo la abiria ambalo halikuwepo siku nyingi.

“Jengo kama hilo linajengwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam maarufu kama Terminal III kwa ajili ya kuboresha huduma za abiria. Kwa upande wa uwanja wa ndege mjini Dodoma, Dk Abbasi alisema tayari ukarabati umefanyika, lakini pia kuna shughuli inafanyika katika uwanja mpya unaojengwa katika eneo la Msalato. “Viwanja vingine vinavyofanyiwa ukarabati, kupanuliwa na kujengwa majengo ya abiria ni Tabora, Mwanza, Geita, Musoma, Njombe, Lindi na vingine vingi.

Wakati huo huo, Dk Abbasi alisema serikali inaleta mabehewa 1,590 na vichwa vya treni 25 kwa ajili ya Reli ya Kisasa, inayojengwa kati ya Dar es Salaam na Morogoro na kati ya Morogoro na Dodoma. Alisema reli itakapokamilika katika kipindi cha miezi 36, mabehewa na vichwa vya treni, vinatakiwa kuwepo ili kuanza kazi ya kusafirisha abiria na mzigo mara moja. Alisema tayari zabuni ya kutengeneza mabehewa na vichwa hivyo imeshatangazwa, ambapo kampuni zaidi ya 54 zilijitokeza kuwania fursa ya utengenezaji huo.

Alisema kati ya hizo, kampuni 35 zimerudisha barua za zabuni na hizo uchambuzi wake wa kubaki na kampuni ya kutengeneza mabehewa hayo itakapopatikana. Alisema kampuni itakayoshinda zabuni, inatakiwa kutengeneza kwa miezi 24 na miongoni mwa mabehewa hayo 50 ni ya ngazi mbili, 100 ni ya mafuta, mengine ya watu mashuhuri na mengine ya kawaida. Vile vile, alisema serikali inatekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa meli za kisasa katika Maziwa Makuu nchini ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Alisema kuhusu Ziwa Victoria, serikali inatengeneza meli kupitia Kampuni ya TSX ya Korea Kusini ambayo mkataba wa kutengeneza meli hiyo ulisainiwa mwezi Machi, mwaka huu.

Chanzo: Habari leo
 

samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,564
2,000
Hizo ndege Zingefaa kipindi kile cha JK, kwa sasa hata kula yetu tu ni shida ndege wamebaki kupanda wafanyakazi wa asasi za kiraia na mashirika makubwa.. wananchi wa kawaida wanaoweza kujikamua wamebaki wachache mno. Nilipanda fast jet week mbili zilizopita tulikua nusu..ndege ya watu 96 tulikua kama 45 hivi
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,179
2,000
Hii familia bwana inashangaza! Yaani imeshindwa kulea watoto wawili alafu inafurahia ujio wa watoto wengine wa nne tena kwa mpigo (mapacha wanne)!!

Mimi kama jirani yao, safari hii wakinigongea hata chumvi naapa siwapi.

Baba fulani zingatia uzazi wa mpango utaua watoto.
 

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
3,742
2,000
Wanavyo sema utafikiri julai mbali ..ngoja tuone iyo july ikifika maana ata mwanzo walisema julai iliyo isha
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,974
2,000
Alisema kampuni itakayoshinda zabuni, inatakiwa kutengeneza kwa miezi 24 na miongoni mwa mabehewa hayo 50 ni ya ngazi mbili, 100 ni ya mafuta, mengine ya watu mashuhuri na mengine ya kawaida.
Kumbe kutakuwa na matabaka ............ akina Bashite na sisi akina Kaka Miye!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom