Ndege ndogo ya Kilimoanga yauzwa kwa tshs 500,000/-

King’asti

Platinum Member
Nov 26, 2009
27,823
24,779
Ndege ndogo ya kutumika kunyunyizia pesticides kwenye taasisi ya serikali ya kilimo anga imeuzwa kwa tshs laki tano kwa madai kuwa hakukuwa na vipuri.

Wafanyakazi wasio na mkataba wa kudumu nao hawajalipwa mishahara kwa miezi 17.

Hayo yameelezwa kwa waziri wa kilimo leo hii, alipowatembelea.

Source: Taarifa ya habari tbc1
Na Mussa Juma, Arusha | Januari4 2013


WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza jana alishikwa na butwaa, pale alipopewa taarifa ya kuuzwa ndege tatu za Serikali, ambazo zilikuwa katika Kituo cha Kilimo Anga kwa kiasi cha Sh500,000 kwa kila moja.

Ndege hizo, tatu zilikuwa zikitumika katika udhibiti wa wadudu waharibifu wa mazao.


Akisoma taarifa ya kituo hicho mbele ya Waziri Chiza, Mhandisi Mkuu wa Ndege wa kituo hicho,Gideon Mugusi,alizitaja ndege hizo kuwa ni 5H-MRN, Cessna 185 nyingine ni 5H-MRF, Cessna 185 na nyingine aina ya 5H-MRP piper Super Cub ambazo zilianguka katika vipindi tofauti.

"Ndege zote tatu ziliharibika lakini Shirika la Bima la Taifa(NIC), walilipa Serikali kupitia katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo, kulingana na viwango vya bima vilivyokuwa vikilipwa na wizara"alisema Mugusi.

Hata hivyo alisema tangu kuanguka na kuuzwa kwa ndege hizo,shughuli za kituo hicho, Kimekuwa zikidorora kwani marobani karibu wote wameondoka na kituo kimebaki na ndege moja tu ambayo pia ni mbovu na kibali cha kuruka angani kimekwisha.

Alisema kwa sasa kutokana na kukosekana kwa ndege, gharama za uendeshaji wa shughuli za kituo zimekuwa ni kubwa mno kwani wanalazimika kukodisha helikopta na gharama zake zimekuwa zikipanda mwaka hadi mwaka.


Waziri aja juu:
Kutokana na maelezo hayo, waziri Chiza alikuja juu na kuhoji iweje ndege hizo, ziuzwe kwa Sh 500,000 kila moja.


Waziri huyo, pia alihoji iwapo ndege hizo, zilifutwa kwenye orodha ya kumbukumbu za Serikali kama hazifai kwa matumizi pia kama ufutwaji wake ulifuata sheria na kanuni za Serikali.


"Leo sikuja kukamata mchawi, ila mimi binafsi nitafuatilia ili kuona kama sheria zilifuatwa au kama ndege zimeuzwa bila kufuata sheria" alisema Chiza.

Awali alisema Serikali ina mpango wa kufufua kitengo hicho na kwa kuanzia tayari imetoa fedha za kununua ndege moja.


"Naagiza mfanye mchakato haraka wa kununua ndege hii, hatutaki tena ukiritimba kwani nia ya Serikali ni kufufua kituo hiki,"alisema Chiza.

Alisemakituo hicho ndiyo pekee katika nchi za Afrika ya Mashariki chenye uwezo wa kutoa huduma hiyo ya kilimo anga na kama ndege zikianza kufanya kazi, basi zitaweza kukodiwa na nchi jirani.


Kituo cha Kilimo Anga kilianzishwa na wizara ya kilimo ,ikishirikiana na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la UNDP na FAO mnamo mwaka 1979 na lengo kubwa lilikuwa ni kuimarisha utoaji huduma katika sekta ya kilimo katika kupambana na visumbufu vya mimea wahamao(migratory pest control).
 
laki5???

mshahara wangu mwl wa mwez na chenchi inabaki??
ama kweli sasa mtambo kama huo ulikuwa na wafanyakazi wa nn kama thamani yake ni iyo?? ni sawa na mtu uwe na maabara yenye uwezo wa kusterilize kwa bunsen burnner tu halafu uajiri watu wanaolipwa mamilion kwasabbu ya kusterilize.
 
Ndege ndogo ya kutumika
kunyunyizia pesticides kwenye taasisi ya serikali ya kilimo anga imeuzwa
kwa tshs laki tano kwa madai kuwa hakukuwa na vipuri. Wafanyakazi wasio
na mkataba wa kudumu nao hawajalipwa mishahara kwa miezi 17. Hayo
yameelezwa kwa waziri wa kilimo leo hii, alipowatembelea.

Source: taarifa ya habari tbc1

Unashangaa hilio, ninda pale TFDA, kuna kalakana ya wizara flani kuna mgari mapya kabisa, maVX, yamepasuka tairi tu, yanaachwa hapo, muda ukipita, wanauziana kwa bei cheee...
 
Unashangaa hilio, ninda pale TFDA, kuna kalakana ya wizara flani kuna mgari mapya kabisa, maVX, yamepasuka tairi tu, yanaachwa hapo, muda ukipita, wanauziana kwa bei cheee...
aisee. Yaani this is beyond. Na mfanyakazi kibarua ambae hajalipwa 17 months ina maana anajikimu na vipuri ama inakuwaje? Nangojea ikulu iuzwe labda ntanunua.
 
aisee. Yaani this is beyond. Na mfanyakazi kibarua ambae hajalipwa 17 months ina maana anajikimu na vipuri ama inakuwaje? Nangojea ikulu iuzwe labda ntanunua.

utasubiri sana kuuziwa! Kwani wewe ni Mwarabu? Muulize Mengi kuhusu Kilimanjaro Hotel!!
 
Nyie mnashangaa hiyo, Kuna Shirika Moja la Uma ambalo ni kati ya Mashirika Machache ya Umma yanayo fanya vizuri, wao njia wanazo tumia kujuiuzia magari mapya kabisa ni Kuya Piga Chini, Mfanya kazi akihitaji kununua gari la Shirika, hufanya mpango na Dreva ili hilo gari either Linagushwe makusudu au Ligonge hata Mti, baada ya hapo, Gari hupakiwa na baadae huuzwa,

Kuna Dreva mmoja alipiga chini Tiper Mpya kabisa iliyo tembea mwezi na baada ya wiki kadhaa jamaa akauziwa gari alilo angusha
 
NI ukweli usiopingika tembelea leo hii kwenye ofisi zote za serikali ,utajionea jinsi magari ya thamani ya aina mbalimbali yalivyotelekezwa kwa matatizo ya kiufundi yanayorekebishika lkn hakuna anayejali ,zaid zaid viongozi walipo wanapigania kupewa magari mapya yenye thamani kubwa .wakati ukifikiri kwa kina hakuna sababu ya kutoa gari jipya . viongozi wakiamua kwa uzalendo fedha ya gari moja ianaweza kukarabati magari kibao yaliyoegeshwa ktk maofisi ya umma.
 
hahahahhaa. Kiazi cherema kinatengeneza mashed potatoes?
Hujanielewa! wewe kama raia tena msomi unapaswa kuelewa code ya pesa ya nchi yako. Mbona code ya dollar, euro na paundi unazijua halaf ya nchi yako hujui unaandika TSHS?
 
As usual, exploiters at system, the vampires are sucking our blood, twafwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hiyo ndio bongo daslamu.kila mtu anatafuna anapoona panalika.sasa 500,000 ina maana wameuza screpa
 
Hujanielewa! wewe kama raia tena msomi unapaswa kuelewa code ya pesa ya nchi yako. Mbona code ya dollar, euro na paundi unazijua halaf ya nchi yako hujui unaandika TSHS?

sasa msomi wewe, are you part of the solution ama part of the problem? You are distracting me, stay on your lane. Kama una njia mbadala ya kuiandika, do or forever shutup.
 
Back
Top Bottom