TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 24,750
- 24,802
Wakuu, katika pitapita zangu huku na kule; nimekutana na habari muhimu inayoifaa Tanzania. Habari hii inahusu upatikanaji wa bidhaa tunayohitaji kwa sasa kuboresha uchumi wetu. Bidhaa hii imepatikana katika soko jipya huko Mashariki ya mbali (Russia). Kwa sasa Russia wanauza ndege zinazoshindana na zile za wazalishaji wakubwa kama Airbus na Boeing.
Russia kupitia Irkut Division of the United Aircraft Corporation (UAC) group wametengeneza MC-21 ndege yenye uwezo wa kubeba abilia 150 mpaka 212 kwa mkupuo na kuwa na speed kubwa ya 870km/h ukilinaganisha na speed ya ndege za washindani wake ambayo ni 842 na 828 km/h. Bei ya ndege hiyo ni inakaribia USD 85 million tu kwa sasa ambayo ni ndogo kulinganisha na za wengine.
Irkut wanatarajia kutoa bidhaa hii kwa wingi kiasi cha ndege hamsini (50) ifikapo mwishoni mwa 2018 ama mwanzoni mwa 2019. Hivyo nashauri Tanzania tusubiri kidogo tuchukue mzigo wa maana na nafuu kutoka Russia.
=TUJITEGEMEE.