Ndege mpya mbili kupokelewa Jumatatu tarehe 11/10/2021

Wazo Kuu

Senior Member
Oct 21, 2018
114
293
Ndege mpya mbili zitapokelewa Ijumaa ya tarehe 8/10/2021.

Ndege hizo zitapokelewa katika uwanja wa ndege wa Amani Zanzibar.

Tujikumbushe mambo ya Muungano.
Ukurasa wa 218 na 219 wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, unataja Mambo ya Muungano ambayo ni:-.

01. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
02. Mambo ya nje
03. Ulinzi na Usalama,
04. Polisi
05. Mamlaka juu ya mambo yanayohusu hali ya hatari,.
06. Uraia.
07. Uhamiaji.
08. Mikopo ya Biashara ya Nchi za Nje.
09. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

10. Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.

11. Bandari, mambo yanahusika na usafiri wa anga, posta na simu.

12. Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yoyote halali(Pamoja na noti) mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.

13. Leseni ya viwanda na takwimu.
14. Elimu ya Juu.
15. Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa na motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia.

16. Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za baraza hilo.
17. Usafiri na usafirishaji wa anga.
18. Utafiti
19. Utabiri wa hali ya hewa.
20. Takwimu.
21. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano
22. Uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana nayo.
MAMBO 22 YA MUUNGANO 1 .jpg


MAMBO 22 YA MUUNGANO  2.jpg
 
ATCL ni kampuni iliyokodishwa ndege zilizonunuliwa na Serikali. ATCL kama kampuni ya usafirishaji wa anga ina hub yake Dar es salaam, hivyo ndivyo inayotambulika huko IATA.

Hizi siasa kwenye biashara tete, tena ya ndege zenye ushindani mkubwa na mtaji unaopita bajeti za wizara, zingeachiwa wataalamu waziendeshe kwa faida.

Hizi siasa zitaturudisha nyuma kwenye mradi huu wa ndege..... Labda kama hii itakuwa mbinu ya kumkwepa mkulima, Asikamate Moja!!.
 
Back
Top Bottom