Mkurugenzi ATCL: Dreamliner haijaharibika, tunafanya marekebisho ya kawaida. Ndege bado ipo kwenye majaribio...

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,982
144,306
Hii ni habari kwa mujibu wa ITV ambayo mimi binafsi nimechelewa kuisikiliza ila ni habari inayosomeka katika maandishi yanayopita chini ya screen wakati taarifa ya habari inaendelea.

F0340491-9D24-46B7-AC61-0F7440B8E2E3.jpeg

Ni matengeno gani? Aliyesikia atujuze.
=======

Mkurugenzi wa Shirika la Ndege nchini(ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi amekanusha taarifa kuwa, ndege ya Dreamliner 787-8 ina hitilafu na kwamba ilisitisha safari yake ya Mwanza - Dar kuanzia juzi.

Amesema katika ndege nne za ATCL (3-Bombardia na 1-Dreamliner), Bombardia zinaendelea na safari bila matatizo ila Dreamliner imesimamishwa ili ifanyiwe marekebisho

Marekebisho hayo ni kama ya WIFI na mengine madogo madogo yanayohusu uendeshaji wa ndege maana safari za ndege hiyo kwa sasa ni za majaribio kwa Marubani

Ameeleza kuwa walipanga marekebisho hayo kufanyika baada ya wiki tatu baada ya kuanza safari zake, ila kilichopelekea marekebisho yafanyike sasa ni mafundi walioomba yafanyike mapema kwa kuwa wanaondoka nchini

Marekebisho hayo yaliyoanza juzi yanatarajiwa kukamilika leo na hivyo ndege hiyo kuanza safari zake kama kawaida hapo kesho

Habari zaidi, soma=>Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner imeharibika kuanzia jana jijini Mwanza abiria tumeshindwa kuendelea na safari leo - JamiiForums
 
Ndege ni chombo kinachohitaji uangalizi wa hali ya juu. Ndege kuwa mpya haimaniishi kuwa hitilafu haziwezi kutokea!
Kikubwa zaidi, Tanzania tuna ndege ya aina hii moja na kwa sababu hiyo ni rahisi sana kugundua kama haifanyi kazi lakini kwenye mashirika yenye ndege nyingi za aina moja huwezi kugundua kama kuna ndege inafanyiwa matengenezo. Kwa mantiki hii, hata safari haziathiriki kwa kiwango kikubwa ukilinganisha kama una ndege moja.

Hata Rais wa Marekani ana ndege mbili za aina moja za Air Force One ili hata kama moja inafanyiwa marekebisho, nyingine inakuwa tayari kwa kazi. Hata Helikopta za Rais ziko mbili zinazofanana.Huwezi kujua kama ndege au helikopta imeharikiba na inafanyiwa matengenezo au la.
 
Ndege ni chombo kinachohitaji uangalizi wa hali ya juu. Ndege kuwa mpya haimaniishi kuwa hitilafu haziwezi kutokea!
Comrade
Ndege ikiwa mpya kutoka kiwandani
Huwa inafanyiwa service baada ya muda mrefu kupaa hewani na sio kuwa grounded kabisa kwa sababu ya obovu wa kifaa

Hii imekuwa grounded baada ya kuharibika kwa Mfumo wake ktk moja ya kifaa chake...

Tanzania ni zaidi ujuavyo

Rais ajaye wa awam ya 6 akifukua makaburi kuna watu itabidi WANYONGWE HADHARANI
 
Imeharibika kitu gani?
 
Hii ni habari kwa mujibu wa ITV ambayo mimi binafsi nimechelewa kuisikiliza ila ni habari inayosomeka katika maandishi yanayopita chini ya screen wakati taarifa ya habari inaendelea.
.
Ni matengeno gani aliesikia atujuze.

Comment ya kustaajabisha...matengenezo ni jambo la kawaida kwa ndege...dah...wako watanzania wa ajabu mno...'ushakumbenga' unashika kasi mpaka inauudhi kwa kweli..yaani kila siku kuombea mabaya tu
 
Back
Top Bottom