Ndege iliyokuwa na ujumbe toka Ivory Coast yazuiwa kuondoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA)

Huo mkutano wa Arusha ulikuwa na viongozi wengi tu na wamekuja na ndege zao. Kwanini hii ndege ya vigogo wa Ivory Cost izuiliwe na sio hizo zingine?

Nasikia Simba hawakupokelewa vizuri huko Ko Divwaa. :thinking:
 
Kwani ameshazuia ndege ngapi toka kumekucha leo? Na kwanini ni ndege hiyo tu aizuie? Tafakari Mjomba, Unaweza kukuta kuna Kiboko au Mamba hai wa Baba Riz ameshapakiwa ndani ya hiyo ndege. Hataki kufa Ki-Maige huyo.

Nampongeza huyo msimamizi kwani uzembe na kutokuwa strict ndio kulisababisha midege ya Jeshi ya falme za kiarabu kutua na kuondoka na twiga wetu. Cha muhimu aseme ameona nini kwani ana sababu kukataa na hayuko tayari kuharibu kitumbua kwa kuogopa wakubwa.
 
There must be something wrong.Kama hiyo ndege haikufata utaratibu,mkuu wa KIA yuko sahihi kabisa.Hivi vimemo hata vingekuwa vinatoka kwa Mkuu ,ni kuvipiga chini,coz kama kuna issue mbaya inatokea mzee akawii kumruka,anamuachia msala akomae nao mwenyewe.
Mkuu huenda jamaa anafanya kazi yake. Labda ndege imekiuka masharti na inabidi wenye ndege wafuate taratibu fulani ndio waondoke. Naona unamshutumu kuwa ana kiburi; si anafanya kazi yake? Hiyo ni Arusha mkuu isije ikawa ndege ina simba ama kori bastard kesho mkaja kumuuliza kama alivyoulizwa Maige.
 
Huyo jamaa aliyeizuia ndege ana sababu za msingi labda ndege hiyo imebeba vi-pipi au Twiga wetu. Huyo jamaa atapanda cheo haraka sana.
 
Wanapenda shortcut, na wao ndio waliojazana Kilimanjaro Airport, kila idara.
Hiyo ni hukumu ya jumla siyo nzuri sana. Sidhani kama ni vyema kuwa na chuki na kundi la watu kwa jinsi hiyo. Hiyo husababisha dhambi ya ubaguzi kama alivyowahi kuiita Baba wa Taifa, huwa haiishi kinyume chake huendelea kukua kama kansa katika mawazo ya binadamu. Ni nyema sana kujitahidi kuji-control. Epuka sana generalization za namna hii katika jamii.
 
Saaafi sana! Siyo kaburi yupo kazini kwake. Akiliruhusu likadondoka kumbe bovu nani atalaumiwa. Huyo Msaidizi wa Rais ndege inamhusu nini, tuache watu wetu wafanye kazi kwa mujibu wa sheria. Tanzania mliwahi kufanya kosa la ajabu . Mwaka 1994 mliruhusu ndege moja iwabebe Marais wawili, Junenal Habyarmana (Rwanda) na Cyprien Ntaryamira (Burundi). Kifo ambachokwa kweli kilikuwa cha Habyarimana kikamkumba Ntaryamira wa Burundi. Hatujawahi kujiuliza ilikuwaje Marais wawili wapande ndege moja, kwa haraka gani, ama kulikuwa na njama? Afisa wa Uwanja wa ndege, komaa, ukimsikiliza huyo wa Ikulu utaumia! Ila nawapa pole, maana sasa mtakuwa mmempandisha hasira Drogba na Yaya Toure, na badala ya magoli manne waliyokuwa wamepanga kutufunga , wamenipigia simu sasa hivi, yatakuwa sita. Uuwiiii.......labda tuachie hiyo ndege nini, sita bila!
 
Mpaka naondoka eneo la tukio ndege hiyo ilikuwa bado haijaruhusiwa kuruka baada ya msimamizi wa uwanaja huo kutia ngumu,haikujulikana maramoja sababu ni nini ila baada ya kumhoji alisema hajui ni kampuni gani inayo husika na ndege hiyo hivyo hawezi kuiruhusu kuruka.hata baada ya msaidizi wa katibu wa raisa kupiga simu uwanjani hapo kutaka kujua sababu ya ndege hiyo kuzuiliwa kuruka bado msimamizi huyo wa uwanja aligoma katakata kuongeanae hata alipo ambiwa ni ndege iliyokuwa na wageni wa raisi msimamizi huyo hakuwa tayari kuongea na msaidizi huyo wa katibu.kwa mwonekano msimamizi huyo wa uwanja anaonekana kuwa na kiburi sana na mtu asiye jali ila inaonekana ni mwendelezo wa kukomoana.

Chanzo ni mimi mwenyewe toka ngurudoto na uwanja wa ndege wa kilimanjaro kia
nikipata habari zaidi nitawaletea.
Mbona umemuhukumu bila hata ya wewe kujua sakata zima.Inaonekana sorce yako ya habari ni kutoka upande mmoja. Hapo KIA kuna uchafu unafanyika kila kukicha ,kuna ndege za Cargo kubwa mno zinatua hapo na kuondoka nishazishudia mara mbili wakati nime-land hapo na zote mbili ni za falme za kiarabu,sasa sijui kuna biashara gani na hao waarabu ili hali twajua waarabu ni wazoefu wa biashara ya pembe za ndovu tokea enzi hizo.Mengi yatajulikana Baba riz akiachia ngazi.
 
Ukiuke wewe mfanyakazi kutenda kazi zako huko airport uwasingizie CCM? kweli kuna watu na viatu.

Nina video na pia nina picha nilichopiga.Ukitaka nitakutumia.Wewe ni mmoja mnaonufaika na lidudu lenu ccm.Na mimi sina cheo lakini siachi kuisema hiyo ccm yako bila kuiogopa.Wanaofanya hivo ni hao waoga.Nimesha wahi kumkatalia Sabaya aliyekuwa mkuu wa wilaya hapa wakati huo salma alikuwa anakuja kwenye ziara bubu.Simkumtekelezea alivyotaka na meneja wangu akasema nimekosea.Lakini kama ningekosea kama alivyotaka angenishtaki.Sina ujinga huo.Wewe na ccm yako iliyounda serikali dhaifu ndio mnaokiuka sheria.
 
jamaa anastahili heshima kama kuna taratibu zimekiukwa
lazima zifuatwe.
 
By Mimibaba
Wewe ukiwa kiatu cha karatasi

Wewe cha kandambili. Kwi kwi kwi teh teh teh

Acheni utoto.. Hoja hapa ni kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za kazi zinavyotaka au ku-by pass/overlook sheria na taratibu hizo za kazi pindi vikitumwa vimemo toka Ikulu..? Yuko sahihi kucimamia maamuzi yake kama taratibu hazikufuatwa..? Kwangu mie ninaona yuko sawa kama amezuia kwa kuwa kuna taratibu hazikufuatwa..
 
Hivi mnakumbuka wakati wa Rais wa Tunisia Ben Al anakimbia Ikulu ya Tunisi kuogopa nguvu ya umma aliacha fedha lukuki na makasha ya Madawa ya Kulevya.Biashara kubwa aliyofanya Ben Al na maswahiba wake ni kutumia Ikulu kusafirisha madawa ya kulevya katika nchi za Kiarabu na Ulaya.Watumishi wa Viwanja vya ndege komaeni hata kama ni madawa ya kulevya na nyara za serikali kamateni na nguvu ya umma itawalinda
 
nampa hongera
yeye sio mjinga azuie bila sababu
lazima tujiulize kuna nn sio kujifanya wajuaji
kwani hata akipigiwa simu ikulu kwani ikulu wako juu ya sheria?
tunataka wazalendo kama hao na sio wachekea vibahasha.
 
Hiyo ni hukumu ya jumla siyo nzuri sana. Sidhani kama ni vyema kuwa na chuki na kundi la watu kwa jinsi hiyo. Hiyo husababisha dhambi ya ubaguzi kama alivyowahi kuiita Baba wa Taifa, huwa haiishi kinyume chake huendelea kukua kama kansa katika mawazo ya binadamu. Ni nyema sana kujitahidi kuji-control. Epuka sana generalization za namna hii katika jamii.

Angekuwa hana dhambi ya ubaguzi kusingekuwa na 87/13. Turudi kwenye mada.
 
Acheni utoto.. Hoja hapa ni kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za kazi zinavyotaka au ku-by pass/overlook sheria na taratibu hizo za kazi pindi vikitumwa vimemo toka Ikulu..? Yuko sahihi kucimamia maamuzi yake kama taratibu hazikufuatwa..? Kwangu mie ninaona yuko sawa kama amezuia kwa kuwa kuna taratibu hazikufuatwa..

Ki memo Ikulu mpaka Kilimanjaro Airport? kweli kuna watu na viatu.
 
Angekuwa hana dhambi ya ubaguzi kusingekuwa na 87/13. Turudi kwenye mada.
Aliyetoka kwenye mada ni wewe in the first place!
fafanua kwanza what is 87/13? Huko siyo kuendelea kutoka kwenye mada?
 
Back
Top Bottom