Ndege iliyokuwa na ujumbe toka Ivory Coast yazuiwa kuondoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndege iliyokuwa na ujumbe toka Ivory Coast yazuiwa kuondoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PISTO LERO, Jun 1, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mpaka naondoka eneo la tukio ndege hiyo ilikuwa bado haijaruhusiwa kuruka baada ya msimamizi wa uwanaja huo kutia ngumu,haikujulikana maramoja sababu ni nini ila baada ya kumhoji alisema hajui ni kampuni gani inayo husika na ndege hiyo hivyo hawezi kuiruhusu kuruka, hata baada ya msaidizi wa katibu wa raisa kupiga simu uwanjani hapo kutaka kujua sababu ya ndege hiyo kuzuiliwa kuruka bado msimamizi huyo wa uwanja aligoma katakata kuongeanae hata alipo ambiwa ni ndege iliyokuwa na wageni wa raisi msimamizi huyo hakuwa tayari kuongea na msaidizi huyo wa katibu.kwa , wonekano msimamizi huyo wa uwanja anaonekana kuwa na kiburi sana na mtu asiye jali ila inaonekana ni mwendelezo wa kukomoana.

  Chanzo ni mimi mwenyewe toka ngurudoto na uwanja wa ndege wa kilimanjaro kia
  nikipata habari zaidi nitawaletea.

  =================================
  update:
  NDEGE IMERUHUSIWA KUONDOKA
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Anataka sheria na kanuni zifatwe? au anazuia wakati sheria na kanuni zote zimefatwa? Sidhani kama atakuwa na kiburi bila kulindwa na sheria na kanuni, kuna vitu haviko sawa.
   
 3. i

  isotope JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Simu ya msaidizi wa katibu ambaye ni msaidizi wa rais. Kama kuna mambo hayako sawa, hata mimi nisingeruhu hiyo ndege iruke. Hizi simu na vimemo ndo vinavyotafuna rasilimali za nchi yetu.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyo jamaa anapaswa kuvikwa medani ...yaani ujumbe wa rais ndo nini?yaani kama hawajafuata sheria washuke waendelee kupiga koka wasubiri mkuu wa uwanja atoe go ahead
   
 5. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yawezekana ameona kasoro ndio maana amegoma
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Labda ina twiga ndani
   
 7. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani ameshazuia ndege ngapi toka kumekucha leo? Na kwanini ni ndege hiyo tu aizuie? Tafakari Mjomba, Unaweza kukuta kuna Kiboko au Mamba hai wa Baba Riz ameshapakiwa ndani ya hiyo ndege. Hataki kufa Ki-Maige huyo.
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu huenda jamaa anafanya kazi yake. Labda ndege imekiuka masharti na inabidi wenye ndege wafuate taratibu fulani ndio waondoke. Naona unamshutumu kuwa ana kiburi; si anafanya kazi yake? Hiyo ni Arusha mkuu isije ikawa ndege ina simba ama kori bastard kesho mkaja kumuuliza kama alivyoulizwa Maige.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kigogo ni medali. Haya mambo ya kupigiwa simu hayafai. Jamaa wacha akomae manake kukiwa na shida kesho ataulizwa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Nadhani huu uwanja unaendeshwa na kampuni ya nje, na sio Watanzania. Nina uhakika kwamba kuna taratibu hazijafuatwa ndio maana amegoma, na anastahili pongezi. Kumbuka miaka michache iliyopita Kenya Airways walilazimisha kuruka kutoka uwanja wa ndege nchini Cameroon wakati wa mvua kubwa, japo walikataliwa. Matokeo ndege ile ilianguka baada ya dakika tano za kuwa hewani, abiria wote wakafa.
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Hahahahaa.............hajui ndege hiyo ni ya kampuni gani....kwani ilituaje hapo??!!

  Aseme tu Mangunga wetu ashampa mtu punda milia kama zawadi!!
  Kwani hamjui Mangunga wetu kidogo...:crazy::crazy:
   
 12. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 2,461
  Trophy Points: 280
  Wawe wavumilivu,,,, ila kama taratibu hazikufuatwa ni vzr waendelee kusubiri. Simu za msaidizi wa rais zisitumike kuvuruga utaratibu.
   
 13. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Huo ndio uzalendo tunaongelea hasa kama kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi. Hawezi kuwa mjinga kuharibu kazi yake kama ndege hiyo haina makosa. Na hiyo simu angepokea angegombezwa na kuharibu kazi. Wafuate taratibu basi ndege itaondoka. Siyo aruhusu makosa halafu baadaye inakula kwake hata pamoja na simu kutoka Ikulu.

  Ndiyo maana kuna ikulu na waratibu wa ndege kwenye viwanja vya ndege.
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyo msaidizi wa rais ni nani na kwa nini anaingilia operations za KIA?
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hao ni wageni wa Rais na kama umesoma vizuri mada yeye kauliza kutaka kujuwa tatizo ni nini. Hivi wewe mgeni wako akizuiliwa kusafiri hutotaka kujuwa sababu? kweli kuna watu na viatu.
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kuna nyoka wamechukuliwa kutoka arusha snake park -tetesi
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  hata ile ndege ya kijeshi ya kutoka qatar ilipigwa simu kutoka ikulu na ni hao hao wageni wa rais wenu alhaji
   
 18. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Hapo KIA si ndo walipitishia wanyama kwenda uarabuni?inawezekana nayo imebeba mali za watanzania!
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nafikiri ni mtu mwenye busara.

  Basi huyo mfanyakazi aliyoruhusu inabidi ashitakiwe, kama hafati sheria na anafata maagizo ya simu, huyo hafai hata tone, itakuwa ni mchagga tu huyo, ndio wanapenda shortcut.

  U Al Haj wake unahusu nini? kweli kuna watu na viatu.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uarabuni ya Ivry Coast, ipo, wala hujakosea. Ikiwa sisi tunayo sishangai ikiwepo Ivory Coast?
   
Loading...