Uchaguzi 2020 Ndege, barabara na flyovers vilitakiwa viwepo miaka mingi iliyopita. CCM wametuchelewesha. Tukipe nafasi chama kingine

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Baada ya kusikiliza hotuba ya Magufuli akiwa Geita inasikitisha kuona anazidi kupotosha watu.

Anasema kwamba huu si wakati wa kufanya majaribio kwa kukichagua chama kingine, mimi napingana nae. Ki ukweli, huu ndio muda muafaka wa kukipa dhamana chama kingine. CCM ilipewa dhamana zaidi ya miaka 50 lakini wamezidi kututia umasikini. Hizo ndege, fly overs, barabara n.k. tungetakiwa tuwe navyo siku nyingi sana lakini ni CCM ndiyo iliyotuchelewesha!

Amesema pia serikali yake haiingilii dini, hili pia sio kweli. Kuna viongozi wengi wa dini wanabughudhiwa kuhusu uraia wao pale wanapoikosoa serikali. Je Magufuli anasemaje kuhusu hili?

Huu ni wakati muafaka wa kukipa nafasi chama kingine. CCM ilishapewa nafasi kwa zaidi ya nusu karne ikaichezea.
 
Nafikiri ni muda muafaka wa Rungwe kuingia madarakani watu tule wali lishe..
 
CCM haitatoka madarakani kirahisi kwa sababu ya tamaa ya madaraka kwa baadhi ya wapinzani. Nafikiri vyama vya upinzani vingejitathmini kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 na kujua vimepiga hatua kwa kiasi gani na kurekebisha pale walipokwamia. Bila upinzani imara CCM haitaweza kutoka madarakani.

Mnajua kwanini CCM inafurahia vyama vingi vya upinzani? Mnajua kwanini kila siku vyama vinazaliwa na bado serikali ya CCM ipo tayari kuvipa ruzuku? Jibu ni rahisi...CCM inafurahia vyama vingi vya upinzani kwa sababu Kwenye chaguzi hizi hivi vyama vinagawana kura na kuipa ushindi kirahisi CCM bila kujua...CCM sio wajinga wa kuendelea kuwapa ruzuku makanjanja kama CCK, UDP, TADEA, TLP etc.

CCM itatoka madarakani iwapo tutakuwa na umoja. Iwapo tutakuwa na chama kimoja imara cha upinzani. ACT-Wazalendo na CHADEMA bila shaka vinapaswa kujitathmini kama vyama vikuu vya upinzani. Bado havijachelewa!!!
 
Mara miundombinu sio maendeleo mara oh mlichelewa kujenga miundo mbinu.
Which is which?
 
Wafanyakazi ( walimu, wajeda ,watumishi mbali mbali), waliofukuzwa kazi, mama ntilie, boda boda, wamachinga, waliokosa ajira na wanyonge wote hao wanawachora tu. Ila yaliyopo moyoni ni kwenye sanduku la kura , pale ambapo wananchi watakaposema hatuli fly over ndege.

Tuendelee kupiga kampeni ,. Mwaka huu mtapigwa chini kimya kimya.
 
Kabisa, tena vitu wanavyojenga sasa ni vya hali ya chini sana lakini kelele zake ni kubwa mno.
 
Nafikiri ni muda muafaka wa Rungwe kuingia madarakani watu tule wali lishe..
Sometimes unazingua ujue...kampe kura huyu basi
IMG-20200910-WA0101.jpg
 
Hatutaki mapandikizi nenda SAU
We kibaraka tu wachama huwezi nikataza kalale ukue mi ndo tayari nishachukua bendera ya chadema ila mkizingua narudi CHAUMA maana na nyinyi mnaweza amka mkasema tz kuna korona..😂😂
 
kila kitu kinawakati wake tatizo kucheleweshwa maendeleo tatizo viongozi waliopita hawakuyapa kipaumbele maendeleo ya nchi kwa ujumla zaid ya kujiangalia wao na matumbo yao tuuuh
 
Baada ya kusikiliza hotuba ya Magufuli akiwa Geita inasikitisha kuona anazidi kupotosha watu.

Anasema kwamba huu si wakati wa kufanya majaribio kwa kukichagua chama kingine, mimi napingana nae. Ki ukweli, huu ndio muda muafaka wa kukipa dhamana chama kingine. CCM ilipewa dhamana zaidi ya miaka 50 lakini wamezidi kututia umasikini. Hizo ndege, fly overs, barabara n.k. tungetakiwa tuwe navyo siku nyingi sana lakini ni CCM ndiyo iliyotuchelewesha!

Amesema pia serikali yake haiingilii dini, hili pia sio kweli. Kuna viongozi wengi wa dini wanabughudhiwa kuhusu uraia wao pale wanapoikosoa serikali. Je Magufuli anasemaje kuhusu hili?

Huu ni wakati muafaka wa kukipa nafasi chama kingine. CCM ilishapewa nafasi kwa zaidi ya nusu karne ikaichezea.
Saccos hawana hizo agenda za ndege, flyover, Nyerere hyro electric power etc. Busara ni kumwacha aliyethubutu kuanzisha amalizie, nyie subirini 2040 panapo majaliwa.
 
Back
Top Bottom