beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Makundi makubwa ya Ndege waharibifu wa mazao aina ya Kweleakwelea yamevamia wilayani Kondoa mkoani Dodoma na kushambulia kwa kasi mashamba ya Uwele na Mtama ambapo kwa siku ndege hao wanakadiriwa kula kilo 2400 ambazo ni sawa na zaidi ya tani mbili hali inayozusha hofu ya wilaya hiyo kukumbwa na baa la njaa licha ya wakulima kuitikia wito wa kulima mazao hayo kwa wingi.
Ndege hao waharibifu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 24 wamevamia wilaya hiyo na kufanya uharibifu mkubwa kwa kushambulia mashamba na kula mazao hali inayowalazimu wakulima kufanya jitihada za kuwazuia bila mafanikio huku wakishinda mashambani kwa zaidi ya saa 12 ambapo wameitaka serikali kuwaangamiza ndege hao ili kuinusuru wilaya hiyo na njaa.
Kufuatia janga hilo la Kweleakwelea inamlazimu Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba kutembelea wilaya hiyo kujionea uharibifu ambapo amesema tayari serikali imepeleka ndege ya kunyunyuzia dawa ya kuangamiza ndege hao huku pia akiagiza ifanyike tathmini ya hasara waliyopata wakulima ili kuangalia namna ya kuwapatia fidia.
Makundi hayo ya ndege waharibifu mkoani Dodoma pia yameripotiwa kufanya uharibifu katika wilaya za Chemba na Bahi na katika kipindi ambacho wakulima wa mkoa huo wameitikia wito wa kulima mazao ya Mtama, Uwele na Alizeti ambayo ndio mazao yanayostahimili hali ya hewa ya mkoa huo na kuzua hofu ya kuibuka tena kwa njaa.
Chanzo: itv