Ndayiragije kutua msimbazi kupokea mikoba ya Masoud Djuma

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,114
2,000
Kocha bora wa mwezi january na kocha mkuu wa clab ya KMC bw Etiene Ndeyiragije huenda akatua msimbazi. Kutokana na clabu hiyo kupata matokeo mabovu, mashabiki na wanachama waliomba kocha mkuu atafutiwe msaidizi. Katika kikao cha hivi karibuni cha viongozi wa Simba moja ya majina ya makocha waliopendekezwa ni huyo kocha na ananafasi kubwa ya kujiunga msimbazi.

Kutokana na simba kuwa na uchumi mzuri ikilinganishwa na KMC ni lazima tu kocha huyu atimkie huko. Bw Etienne Ndayiragije ameinoa KMC na kuipa mafanikio makubwa mpaka sasa timu hiyo ipo nafasi ya 5/20 katika msimamo.

Iwapo hilo litatokea basi tunaweza kusema R.I.P KMC maana tunauzoefu na kile kilichotokea kule Mbeya City baada ya kocha wao kunyakuliwa na Yanga. Kwa mtindo huu tusitarajie ushindani katika ligi zetu maana wakiona hatari wanadhoofisha ili waendelee wao tu. Simba na Yanga muwe mnaenda mbali kutafuta makocha na sio kuvipora vilabu vichanga vinavyokuja kwa kasi.

Barafu la moto
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom