Ndassa kupinga Bajeti ya Kilimo, Chakula na Ushirika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndassa kupinga Bajeti ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GHOST RYDER, Jul 22, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Leo asubuhi nimemsikia Mbunge wa Sumve CCM Ricahrd Ndasa akithibitisha kuwa hataunga mkono hoja ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika endapo serikali haitapiga marufuku matumizi ya mzani wa Rula na kuidhinisha mzani wa Digital kutumika.

  Ndassa aliyefuatana na Moses Machari wa Kasulu Mjini walikuwa katika Mahojiano na Kipindi cha Tuongee Asubuhi Star TV kilichokuwa kinaongozwa na Yahya Mohamed – Mwanza na Thom Chilala – Dodoma.

  Katika hali inayoonekana kama ni kujichanganya kwa serikali, wabunge hao na wachangiaji wengine walihoji ukinyonga wa Wizara kwa kuahidi bei ya shilingi 1100 kwa kilo ya Pamba katika Mkutano wa nane wa wadau wa sekta ya pamba uliofanyika mwezi uliopita huko Mwanza na sasa kuidhinisha bei ya shilingi 800 kwa kilo.

  Maswali magumu hapa ni:
  • Nani atawafidiwa wakulima hawa kwa pungufu la bei hii ambayo serikali ina jukumu la kusimamia soko la zao la Pamba.
  • Lakini ugomvi ni hitajio la mizani 10,000 kusambazwa katika vituo vya kununulia pamba ambapo ni dhahiri hapa kuna mchezo mchafu wa Tenda na si ajabu tayari kuna bwana mkubwa kashaagiza mizani za rula ambazo zinampunja mkulima kwa asilimia 40 kwa kuwa kuna 10% hii itafumbiwa macho kama ilivyokuwa SPEED GOVERNOR.
  • Ndassa atashikilia uamuzi wake au mchezo wa Milioni 50 kama zile za Jairo zitafanya kazi kumkata kauli na aishie kuunga hoja mkono kwa asilimia 100?
  • Je aliyoyatamka moses Machali pia atayafanyia kazi kama alivyoahidi kumuunga mkono Ndassa au bahasha itafanya kazi?
  Nimevutika kwenye hoja hii kwa kutambua umuhimu wa kilimo kwa Taifa huku Ndassa akikiri kuwa Pamba ni Siasa na Pamba ni Uchumi.

  Tunasubiri Mswaada huo utakapojadiliwa


  ADIOS
   
 2. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii imetulia sana,maana wakulima wananyanyaswa sana!
   
 3. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hofu yangu ni kama watayatimiza waliyoyasema leo kumkomboa Mkulima wa kitanzania au wataishia kuzibwa Midomo
   
 4. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  SHIBUDA (Licha ya Usaliti wake) anahoji mahusiano ya kimataifa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, inawanufaishaje wakulima wa zao la Pamba
  • Kupata bei ya Uhakika
  • Soko la Uhakika
  • Pembejeo
   
 5. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Anasema MAU MAU wameruhusiwa jana kushitaki udhalimu wa ukoloni wa Uingereza

  Kwani nini MEMBE asishitakiwe mahakama ya Kimataifa kwa kushindwa kuyashitaki makampuni yaliyofunga mikataba mibovu inayoliingiza Taifa katika matatizo makubwa ikiwemo uwekezaji katika sekta ya Kilimo
   
 6. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!hilo nalo neno mkuu.
   
 7. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Imekaa vizuri,, naunga mkono
   
 8. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ahadi ya Ndassa ni Leo, Tunafuatilia mjadala wa Bunge kuweza kuona ni mikakati ipi serikali imeiweka katika kuinua kilimo cha zao la Pamba
   
 9. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Siku nzima ya jana imepita hatujasikia kauli yako kuhusu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Mh. Richard Ndassa, pengine leo kabla ya waziri kuhitimisha jioni tutakusikia kuhusu hili na ndoto za serikali za kuhamasisha Kilimo cha Mkataba ambacho kimeshindwa kupata ufanisi katika Nchi kama Zimbabwe na Malaysia baada ya kuzorota Kilimo cha Umawagiliaji.

  Hapa kwetu hata kuyavusha Maji kutoka upande mmoja wa Barabara huko njia ya Musoma kutoka Mwanza ambapo ni karibu Mita 500 tumeshindwa huku ziwa tunalitazama upande mmoja na upande wa pili mazao yananyauka, halafu tunawaza Kilimo cha Mkataba.

  Ni vema pia suala la Mizani mkatipatia ufumbuzi tujue huyu mwenye tenda ya mizani za rula ni nani ambaye kafanikiwa kushawishi Mizani hizi kuendelea kusambazwa tena katika hitaji hilo la Mizani 10000, huku Maghembe akitoa tamko huko Mwanza ambalo linapingana sasa na utendaji wa Wizara yake.

  Huu ni mzaha kama tumekusudia kuinua Kilimo Nchini.
   
Loading...